Uchaguzi 2020 Mimi Leslie Oscar Mbena ninayejulikana pia kama Msemakweli Chakubanga, natangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Morogoro Mjini

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
MIMI LESLIE OSCAR MBENA NINAYEJULIKANA PIA KAMA MSEMAKWELI CHAKUBANGA, NATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KATIKA JIMBO LA MOROGORO MJINI.

Leo 20:30pm 02/07/2020


  • Imani yangu kwa Rais John Pombe Magufuli,Imani yangu katika Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mimi Leslie Oscar Mbena ninayejulikana kama Msemakweli Chakubanga katika mitandao ya kijamii,Natangaza nia ya Kugombea Ubunge katika Jimbo la Morogoro Mjini,
  • Mjumbe wa halmashuri ya Tawi UVCCM kwenda Chama, Kimara Baruti .
  • 2016-2020 nimesaidia katika ujenzi imara wa tawi la Kimara Baruti na kuongeza idadi kubwa ya wanachama.
  • Ushiriki na kugombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ubungo 2017.
  • Ushiriki na kusambaza sera na taarifa za wagombea wetu katika mitandao ya kijamii kusaidia chaguzi ndogo jimbo la kinondoni na Ukonga.
  • Kushiriki katika majukumu maalumu ya uchaguzi wa serikali za mtaa wilaya ya ubungo 2019 niliyopewa na viongozi wangu na kuyafanikisha.
  • Uandaaji wa maandiko Katika mitandao ya Kijamii, WhatsApp, JamiiForums kuonyesha kazi kubwa anayoendelea kuifanya Mh. Rais John Pombe Magufuli na Serikali ya CCM na kujibu hoja za upinzani mitandaoni 2015 mpaka sasa.
  • Nimeendelea kusaidia tawi langu la chama Kimara Baruti katika masuala mbalimbali ya kujenga chama chetu.

MCHANGO WANGU KATIKA MAENDELEO YA TAIFA
  • Nimeandika utafiti wangu wa kimasomo kuhusu faida za mikopo ya taasisi za kibenki katika kupunguza umasikini kwa Wananchi wa Tanzania,
  • Nimeendelea kushiriki katika masuala mbali mbali ya maendeleo katika ngazi ya jamii maeneo mbali mbali kitaifa na katika wilaya ya Ubungo.

ELIMU YANGU
  • Elimu ya chuo kikuu Shahada ya uzamili katika Utawala na Uongozi, Mzumbe
  • University Dar es Salaam.
  • Shahada ya Kwanza katika Utawala na biashara za kimataifa: Open University of Tanzania.
  • Kidato cha sita, St Francis de Sales Seminary, Morogoro.
  • Kidato cha nne,S t Peter's Junior Seminary, Morogoro.
  • Elimu ya Msingi, Shule ya Msingi Bungo: Morogoro.

KAZI / KIPATO
Afisa wa Benki.

SERA YANGU NIPATAPO NAFASI YA KUHUDUMIA KAMA MBUNGE WA MOROGORO MJINI
  • Ni furaha yangu leo nimeiandika historia ya Morogoro nikielekea kuchukua form ya Ubunge, Morogoro Mjini, kwetu Uluguruni.
  • Nimezaliwa Kichangani, Morogoro, Ninaijua historia ya Morogoro, Kiongozi yeyote katika Mkoa wa Morogoro ni lazima ujue historia ya Morogoro kuweza kujua ilipotoka Morogoro na unapotakiwa kuipeleka Morogoro.
  • Kama Mbunge wa Morogoro nina fahamu nina deni la kuitoa Morogoro katika umasikini wa kipato na kuwapatia Wananchi wa Morogoro fursa za kuingiza kipato katika nyanja za biashara,kilimo na shughuli nyingine ikiwemo ajira za Viwandani,Nina jukumu la kuipeleka mbele Morogoro iliyokuwa Mji toka Mwaka 1928 lakini hadi leo 2020 Morogoro bado ni Mji ule ule.
  • Morogoro ilikuwa Halmashauri Mwaka 1928 kabla ya Dar es Salaam,mpaka leo Morogoro ilitakiwa iwe imeshatoka kwenye Uhalmashauri na kuwa Jiji,Mh Rais Magufuli alisema Viwanda vya Morogoro vifanye kazi lakini hadi leo ni Miaka mitano bado Viwanda vya Morogoro havifanyi kazi na vingi vimeshikiliwa na Mbunge wa sasa wa Morogoro Mjini.

NITAIFANYA MOROGORO KUWA KAMA KARIAKOO

  • Wazambia, Wamalawi, Wazimbabwe, Wamsumbiji, Wakongo, Waburundi, Warwanda, Waganda, Wakenya wanapita hapo Morogoro wanakuja Kariakoo kununua viatu, nguo, mikoba, na bidhaa nyingine. Je, Morogoro mmeshindea kutengeneza hub iwe kama Kariakoo ndogo mkichukua vitu vyote vya Kariakoo vipatikane hapa Morogoro Mjini.
  • Mbunge wa sasa wa Morogoro Mjini alipaswa aitangaze vilivyo Morogoro kibiashara, kwamba Morogoro ni Kariakoo ndogo na hakuna sababu ya kupita Morogoro kwenda Dar es Salaam kilomita 300 wakati vitu vyote vinapatikana Morogoro, huku ni kuwakosesha fursa Wananchi wa Morogoro.
  • Mimi Leslie Mbena nitaitangaza Morogoro kibiashara,Nitaweka matangazo ya biashara zote zinazopatikana katika Soko Kuu la Morogoro katika stendi zote za Treni ya Umeme na Stendi ya Msamvu, Morogoro,
  • Nitawaleta wafanyabiashara Wazambia, Wamalawi, Wazimbabwe, Wamsumbiji, Wakongo, Waburundi, Warwanda, Waganda, Wakenya wanaopita hapo Morogoro kuja Kariakoo kununua viatu, nguo, mikoba, na bidhaa nyingine.
  • Wageni awa wakilala Morogoro,wakinunua bidhaa katika Soko la Morogoro,wataacha pesa ambayo itaongeza mzunguko wa pesa katika Jiji la Morogoro na kuongeza kipato cha Mwananchi mmoja mmoja katika Mkoa wa Morogoro.
  • Wananchi wa Morogoro watakuwa wamepata dola,hivyo biashara ya fedha ya kigeni itashamiri Morogoro kubadili dola kuwa shilingi na shilingi kuwa dola, hakuna biashara hapa Kariakoo inayowatajirisha watu haraka kama biashara hiyo ya dola.

MOROGORO SIO KIJIJI WALA SIO MKOA MASIKINI WALA SIO MAHALI PA MWANANCHI KUKOSA HELA YA KULA NA KUWEKA ZIADA

Tukiweza kuwapata awa Wazambia, Wamalawi, Wazimbabwe, Wamsumbiji, Wakongo, Waburundi, Warwanda, Waganda, Wakenya wanaopita hapo Morogoro kuja Kariakoo kununua viatu, nguo, mikoba, na bidhaa nyingine.

Tutakuwa tumeleta mzunguko wa fedha katika Jiji la Morogoro naamini hakuna kijana atakayekosa kazi, naamini kila kijana jioni atakunywa bia moja na kununua kuku kupeleka nyumbani kwa ajili ya familia Mke na watoto, Miaka ya nyuma Morogoro ilipata kuwa hub ya kikazi na kibiashara,People were flocking from all over East Africa coming to Morogoro.

Hii ilisababishwa na Uwepo wa kivutio cha muziki bora katika East Afrika, mziki ulioongozwa na Mbaraka Mwishehe na bendi maarufu kabisa za Cuban Marimba na Morogoro Jazz.

Hii ni changamoto yangu ya kwanza kuitatua kama nitapata ridhaa ya kuwahudumia Wananchi wa Mkoa wa Morogoro kama Mbunge wao kiongozi katika Mkoa wa Morogoro, Kama kiongozi katika Jimbo la Morogoro nitafanyia kazi kila tatizo linalogomesha Mwananchi kupata kipato cha shilingi 5,000 hadi 10,000 kwa siku.

Nitaenenda katika Utamaduni, Jiografia, Mazingira, Wakati, na mipaka ya Kiuchumi. Kwa maana kila jambo hufunzwa na falsafa yake, mathalani italeta Maendeleo na tija kwa Taifa la Tanzania.

Daima nitaheshimu mila na desturi katika Jiji la Morogoro, Daima nitafuata ushauri wa Kiongozi wetu, Chifu Kingalu na Wazee wa Mkoa wa Morogoro.

Kwa pamoja tunaweza, Morogoro inarudi katika Zama zake.

Nikiishia hapa, Mimi ni Mbunge wenu Mtarajiwa, Leslie Oscar Mbena. Najulikana pia kama Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam
0755078854

Bachelor of Business Administration in International Business.
Master's in Leadership and Management.

Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Hata mimi natangaza nia yangu ya kugombea urais wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ama ACT au CHADEMA, yaani chama chochote kitakachonikubali bila hata kujali sera zake.

Nikishinda hata sijui nitafanya nini kwa sababu sina sera yoyote ila tu nachukizwa na serikali iliyopo madarakani. Sana sana nitapiga trip za nje nyingi kutafuta wafadhili kusudi watu wale bata.
 
Hivi uzamili ndo digirii mbili au ni tatu?

Ungeenda huko ziwa Victoria kuanzisha kilimo cha umwagiliaji nasikia maji ya kule yameoshwa yanafaa kutumika.

Huko morogoro yule brush aliyeweka mizizi hadi imeota utamtoa au utaishia kuumizwa na kupoteza hela zako.

Go, jaribu.
 
Hukuwa na haja ya kuongea mengi sana, tambua kazi za mbunge, subiri sehemu sahihi ya kuyasema, pia zifahamu changamoto za morogoro ipasavyo. Mikwamo ya mipango ya kimkakati ya manisapaa ya Morogoro. Na wengine watangaza nia utulivu wa akili na maarifa ni muhimu sana
 
Unafahamu fika hutaweza kumuangusha kwenye kura za maoni huyo Aziz Abood kutokana na ushawishi wake hapo Moro. Unachokifanya ni kutaka tu uonekane ili Mzee wa kuteua akupe ulaji siku za usoni.

Tangu mlipoufahamu udhaifu wake, mnamtumia kweli kweli pasipo kujua hivyo vyeo mfano DED, DAS, RAS, nk ni mali ya Watumishi wa umma waliojitoa kufanya kazi kwa maslahi ya Nchi kwa miaka mingi, na siyo kwa ajili yenu nyinyi mlioshindwa kura za maoni kwenye chama chenu.
 
Leslie Oscar Mbena. Hongera kwa uthubutu! Ukoo wenu Mbena Malumbi!?

Waluguru watataka kujua je utatoa mabasi kwenye misiba?

Kama siku zone umekuwa ukisaidia tawi lako la Kimara, hujawahi kusaidia Morogoro mjini watakufahamu vipi?

Mwenzako mwarabu anawapatia misaada SANA, huwa anagawa vya bure Morogoro mjini siyo Kimara.

Mfano: Janga la moto Msamvu, aligawa madawa. CORONA, aligawa barakoa na akamwaga ndoo za maji na sabuni stendi.

Everyday is Saturday...:cool:
 
Back
Top Bottom