Afande KOVA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afande KOVA

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Inkoskaz, Jun 6, 2011.

 1. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Mkuu ZPC
  najua katika utendaji wa kazi za kipolisi kuna minor cases na Sensitive cases ambazo handling zake pia ni tofauti,hoja yangu inajikita kwenye case Nyeti zinazohitaji umakini wa utekelezaji wake
  1. Je kila order itokayo juu ni shurti itimizwe hata kama utekelezaji wake una utata na vingi viulizo?
  2.Je Jeshi la polisi linaruhusiwa kusHahabikia mitizamo ya vyama vya siasa
  3.ukiangallia jinsi ulivyonawa mikono sakata la Mwenyekiti wa CDM inatia shaka kwamba ule mtiririko wa GPO haukufuatwa bali ni msukumo wa kisiasa ambao wewe kwa wadhifa wako ungeweza kuukataa ama kutafuta njia ya busara kuumaliza badala ya kujimaliza wewe na hao wanaokutuma.
  Ni vema polisi kujiridhisha na hizi orders na si kukimbilia utekelezaji ambao uko biased,msijitenge na raia,ninyi ni watz wenzetu ambao siku moja tutakuwa wote uraiani,kama ni kufuata sheria tufute bila upendeleo na pia tuzitafsiri kwa usahihi..iweje kesi hii ndogo itumike nguvu kubwa wakati kesi kubwa hata hazitumiki nguvu hizo?hati ya yule broker wa radar Vithlan mnayo miaka mingapi?mbona hamjatuma private jet kumfuata London?
  Nawasilisha!
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu Inkoskazi ukienda kuifanya hiyo kazi ya upolisi-hasa hapa DSM, si utapendeza?
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Asante sana,what ur saying nilisema kwenye mtandao wa mwananchi
  how mafisad hawawatreat lyk that
   
 4. h

  hans79 JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  hatuna jeshi polisi tz,hata walipoongea leo na wanahabar aibu tupu kazi yao kubwa kesi bandia na kufanyakazi kwa ndoto
  warudi tena shule kusoma tena chekechea
   
 5. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Mkuu nachelae kusema watanifukuza kazi iwapo utendaji ni kufuata orders pasipo kuzipembua ama hata kuhoji,police force role yake ipo wazi sana haihitaji ugumu wakufikiri kama madaktari,lakini hapa kwetu inapoteza mashiko kabisaa
   
 6. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  utakuwa chini ya ulinzi, naomba ufute hii post
   
 7. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  It is true..kama ni kweli mnatekeleza maagizo kwa mujibu wa sheria,basi mengine msiyaogope...
   
 8. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Mkuu umeisoma katiba wewe? Binafsi mshipa wa woga sina kwa matendo ya kidhalimu lakini kwa dhambi nitaogopa
   
 9. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  hilo ni onyo, sirudii tena though mimi ni CHADEMA lakini naomba ufute hii post....period
   
 10. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  kova na chagonja hawakuwa na haja ya press conference kuelezea blunder waliyoifanya.....silence could mean a lot to them!!
   
 11. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Upo sahihi kwa ushauri mzuri mkuu lakini ukweli lazima uwekwe mezani hata kama ni mchungu kumeza..kama ni hivyo magazeti na redio nyingi zingetakiwa kukamatwa kwanza..nina imani hata hao waliotekeleza hayo nafsi zinawasuta na tusiposema watajuaje wamekosea? Kinadharia kule Zbr walifuta azimio la arusha na ujamaaa na kujitegemea hivyo tupo katika era nyingine ya uwazi na
  ukweli.mimi nikikamatwa hakuna maandamano wala ulinzi wa kutisha but finaly nitaenda kuonana na hakimu ndiye muamuzi na sio polisi..hata hakimu nae ana msahafu,akienda arijojo kama yule aliyemhukumu Dibagula wakina Kiwanga wapo
   
 12. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Umenena...kukaa kimya ni busara! Japo mimi nimeongea
   
 13. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Mods will rate the topic and decide
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Haya mapovu yote kwa kuwa Mbowe kawekwa kizuizini na polisi na akapelekwa mahakamani on time.

  Wakulaumiwa ni Mbowe, mbona wenzake ilipotolewa amri ya kufika mahakamani walifika na wakaongezewa dhamana? sasa yeye kwa kuwa ni kiongozi wa upinzani basi mahakama imekuwa chini yake?

  Hakimu na ma polisi wameonesha mfano mzuri sana, huyu Mbowe ni mmoja katika hao watunga sheria sasa ikiwa mtunga sheria halafu sheria zake hataki kuzifata ni nani wakutolewa mfano wa hizo sheria?

  Hongera mahakama, hongera Kova.
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Katika mkutano huo na waandishi yule Commissioner wa operations Chagonja alimkandia sana Mbowe na kumuita kila aina ya majina - kwamba hafai kuwa rais, ana majivuno, mbinafsi etc etc. Mwandishi mmoja aliyekuwapo hapo alinidokezea kwamba wakati anayasema hayo alikuwa hajui kama Mbowe alikuwa kisha achiliwa!

  Nadhani baadaye aliposikia Mbowe kaachiwa Chagonja aliona aibu kubwa sana.
   
 16. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  uamuzi wa busara ungewapa shavu san TPF..kwa leo nathubutu kumpa pongezi ACP Akili Mpwapwa kwa kuhakikisha no triggering at arusha wakati mwenyekiti wa CDM alipoachiwa na wafuasi kuingia mtaani kumpeleka hotelini KIBO Palace
   
 17. N

  Nguto JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,652
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  Mbona wamemuwachia wakati wametumia gharama nyingi? Kwa hili unasemaje FaizaFoxy?
   
 18. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  sm1 is already assigned to follow up your steps.
   
 19. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Mkuu karibu nipo
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0  Kova ni mshabiki sana wa siasa na ndiyo maana matatizo mengine ya msingi kuhusu vituo vyake vya polisi hapa Dar hana habari kabisa. Kwa mfano:

  Jana jioni majira ya saa 2 usiku nilikuwa maeneo ya Ilala kumtembelea rafiki yangu mmoja aishie Mtaa wa Utete. Nikakuta hakuna umeme maeneo hayo – biula shaka kutokana na mgao.


  Nilipita mtaa wa Pangani na nilishtuka sana nilipoikuta ile police station ya mtaa huo iko kwenye giza totororooo.

  Hakuna hata mshumaa ulikuwa unawaka kutoka ndani. Hiyo ni station kubwa – siyo police post. Yaani hakuna hata jenereta?

  Jamani hii si hatari hasa katika kipindi hiki cha wasiwasi hapa nchini? Wavamizi wangeweza kuvamia amory na kuondoka na silaha, askari wangewazuia vipi?

  Aidha mtu aliyeumizwa vibaya atapataje fomu ya P3 kwenye giza. Ripoti zitaandikwaje kwenye RB gizani?

  Jamani tunacheza na haya mambo. Komanda Kova – unalielewa hili? Au unakazania tu kutimiza amri za mahakama za kuwakamata viongozi wa upinzani?

  Hebu fikiria scenario hii: Mtu anakwenda kuripoti majambazi yameonekana mahala fulani yanapanga njama zao. Akifika hapo wakati huo haoni kitu, ni giza tupu! Atajua ofisi gani ya kuingia? Au klwanza polisi wakaanunue mshumaa duka la jhirani? Halafu bila shaka gari iliyopo hapo itakuwa haina petroli!

  Hii nchi imefikia hali mbaya sana – Kova na Chagonja wanachojua ni kupambana na upinzani kwa kutoa kauli za hovyo lakini masuala haya ya msingi ya kuboresha vituo vya polisi hawana kabisa habari nayo.

  Ni aibu tupu kwa jeshi letu na kwa wakuu wanaloliongoza. Nyumba ya tatu kutoka kituo hicho cha polisi cha Pangani kulikuwapo jenereta inafanya kazi.

  Yaani tuseme siku hizi wananchi wana hela kuliko serikali? Ndiyo matunda ya ufisadi?
   
Loading...