Aende kumzika baba mkwe?

Aende kumzika baba mkwe?

Mudundo

Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
38
Reaction score
9
Niaje wadau wa Jf. Kuna Rafiki yangu ameghafilika hajui afanyeji. Ali funga uchumba na Binti fulani lakini hajaenda kule nyumbani kwa yule mchumba wake wa kike. Kwa ufupi hajaonana na wazazi wake. Sasa yule babake mchumba wake alikufa juzi, saa hii yuko kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. Je, huyu rafiki ambaye babake mchumba wake amekufa, Je.aende kumzika au asiende?
 
Kufunga uchumba ndio nini?

Halafu kwani kuhudhuria msiba ni hadi uwe na uhusiano wa kifamilia na marehemu au wafiwa?
 
aende tena haraka sana kama hana vikwazo visivyoepukika,uchumba gani huo usioshirikiana na majonzi ya step heart mweh akamfariji mwenzake.
 
Niaje wadau wa Jf. Kuna Rafiki yangu ameghafilika hajui afanyeji. Ali funga uchumba na Binti fulani lakini hajaenda kule nyumbani kwa yule mchumba wake wa kike. Kwa ufupi hajaonana na wazazi wake. Sasa yule babake mchumba wake alikufa juzi, saa hii yuko kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. Je, huyu rafiki ambaye babake mchumba wake amekufa, Je.aende kumzika au asiende?

Hata kama wangekua ni marafiki tuu ilimpasa kwenda kumfariji rafiki yake sembuse mchumba?
 
msiba hauna mwenyewe kwa utamaduni wetu, ndio hatua nyingine ya kuwafahamu ndugu zake huyo aliyefunga chumba sijui, au anaweza kulia kwa sauti baba mkwe umeondoka kabla ya ndoa? aende tu ila awe na mchango wa maana.
 
aende kama rafiki wa kawaida wa binti sio mchumba maana uchumba wake haujatambulika
 
kwani kwenda msibani nayo mpaka uwe na uhusiano na wafiwa au upate kibali cha mjumbe? aende akazike bwana
 
Tangu juzi hadi leo hajafika? Anajishauri nini huo ni msiba hata ingekuwa vipi kwenye msiba hakuna mila za kukataza muoaji asifike labda kama umekatazwa na matehemu. Pia ukifika ndo nzuri kuonekana kuwa unajali. Usimpa pole mchumbako na shemeji zako watarajiwa wakati huu wa msiba utakuwa umepoteza pointi kubwa kwenye uchumba. Hata kama huna hela akope afike tena haraka.
 
Ukijibu haya maswali utakuwa umepata jibu....
  • Kwenye msiba watu huwa wanakwenda sababu ya aliyekufa peke yake au hata waliofiwa... ?
  • Wewe ukifiwa unaotegemea wakifuraji na kukusaidia ni wale wanaotambulika kwenu au watu wa karibu yako?
 
Back
Top Bottom