Valentina
JF-Expert Member
- Oct 12, 2013
- 24,633
- 28,635
Aise!Ndoa bhana ni kitu tata sana wakuu!!!!mtu aoe kwa matakwa yake na si kulazimishwa.
Mimi nimeishi na mwanamke kwa miaka 8 ila nimemuacha yapata miezi 3 sasa na siku 4.tulibahatika kupata watoto 2(ke/me),ila changamoto mi nilikuwa nazo tangu mwanzo huku mwisho uvumilivu ukanishinda ikanibidi kila mmoja achukue hamsini zake.
Mwanamke hakuna unachompa akafanikiwa.ni lazima afeli,hajui kujisimamia ila haya yote niliyakubali sababu ni chaguo langu mwenyewe sikulazimishwa na mtu.
Nimemuacha sababu ya kunipangia masharti ya kurudi nyumbani kuzidi,na kuninyima unyumba kupindukia.
Nikaona tunakozidi kwenda kutakuwa kubaya zaidi,kiroho safi kaniachia wanangu na uzuri hajawahi hata kuwaandaa kwenda shule ni majukum ambayo nilikuwa na ninayafanya mwenyewe nikaona poa tu.
Niko na wanangu miezi mitatu sasa hawajawahi kuuliza mama yao yuko wapi wala anarudi lini.tunaishi nafurahi nao safi kabisa.
Cha ajabu na nilichokuja kujua nilikuwa naishi na kichwa box leo hii kaenda kuwa house maid sehemu daah!!! Kaacha wanae ambao hajawahi kuwaanda kwenda shule,kaenda kuwaandaa wa mwanamke mwenzie.
Wakuu kuoa ruksa ila angalieni mnapooa/kuolewa.hii taasisi ni pana na ngumu mno.