Adult Talks: Kwa kupitia ndoa yako. Unawashauri vipi ambao hawajaoa?

Analyse

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
16,381
41,370
Achana na ile misemo ya mtaani, kwamba kama unapata kila kitu kwenye mahusiano, basi ndoa haina umuhimu. Au wale wanaosema ukishamuweka ndani basi anaota mapembe.

Ukweli ni kwamba huwa inafikia point in this life unahitaji kusettle down. Kwamba hata kama ni kichomi au kivuruge unaamua tu kutulia nae, maana ushazurura sana. Sometime changamoto zinajitokeza mbeleni kabisa, ila wengine wanaanza nazo hizo changamoto, ila baadae zinapotea na wanatulia kwa amani.

Kuna nyumba moja niliwahi kupanga, yule baba mwenye nyumba alikuwa peace sana. Kwenye lile eneo ana nyumba mbili kubwa, moja anakaa na familia yake yenye watoto watano, nyingine ndio tulikaa sisi wapangaji. Kuhusu kodi ya nyumba, alimuachia mkewe ndio awe anachukua ili zimsaidie katika mahitaji ya nyumbani. Yeye Mzee alikuwa anasimamia gharama za uendeshaji mashamba yake na kusomesha watoto. Huyu mama mwenye nyumba alikuwa hapendi kabisa wapangaji wakike. Sometime hata kama kuna chumba kipo wazi, alikuwa anawaambia hapangishi. Alikuwa ni mlevi sana, ikitokea hujalock mlango, unaweza mkuta kajilaza chumbani kwako, hii huwa inatokea sometimes hata kama hajalewa.

Kuna siku nilikuwa napiga story na baba mwenye nyumba, akaniambia kitu kimoja "Jitahidi usije ukakosea kuchagua, kama nilivyofanya mimi baba ako"

Ofcourse mifano ipo mingi, nina broh mtoto wa baba mkubwa ambae alipataga demu kwenye harusi ya binamu. Huyo dem alikunywaga pombe mpaka akazima, ila kabla hajazima alifanya sana vituko. Broh alimsaidia at the end wakawa lovers, siku anatangaza kutaka kumuoa familia nzima iligoma, maana wanajua alipomtoa na vituko alivyofanyaga ambavyo kwa mwanamke ni fedhea. Jamaa alifosi ndoa, ila wakamwambia yakikukuta utajua mwenyewe. Leo hii ndoa yao ina zaidi ya miaka 13, wale waliokuwa wanajiona wamechagua pazuri, washaachana acha wengi tu, plus vikao vikao daily.

BACK TO THE TOPIC

Ningependa kusikia kutoka kwenu dada zangu na kaka zangu mlio kwenye ndoa. Kwamba kwa kutolea mfano ndoa yako, unawashauri nini ambao bado hawajaoa?

Share na wadogo zako, hii elimu ambayo hawatoweza ipata darasani.

Feel free to express anything, walau tuweze jifunza. Real life experience huwa ni mwalimu mzuri sana.

Thanks.

Regards.

Analyse
 
Nipo napitia pitia hivi vitabu.
IMG_20210514_134733_1.jpg
 
Nipo napitia pitia hivi vitabu. View attachment 1784351
Ninachofahamu mimi ni kwamba, kila mwanamke (mwanadamu) ana changamoto zake lakini mke mwema ni yule ambaye unaweza kubebeana changamoto zenu. Kama hauwezi kuzibeba changamoto zake achana naye huyo sio ubavu wako.

Kama unamjua tangia kipindi cha uchumba kwamba yeye ni mvivu/mchoyo lakini unaweza kuvumilia uvivu/uchoyo wake, basi huyo ndio size yako, mchukue kaa naye.

Yangu mimi ni hayo tu kaka mkubwa.
 
Ushauri wa bure kwa vijana wa kike na wa kiume ukiwa upo katika harakati za kutafuta jiko hakikisha unaoa/unaolewa mtu ambae unaweza kuvumiliana nae na anayekubali mapungufu yako na anakukubali jinsi ulivyo(anakuheshimu).

Muhimu kati ya yote upendo uwe nanga kuu.

Mkiwa katika mahusiano be yourself's usijifanye kila kitu kiwe perfect kuridhisha upande mwengine (fake personality) show your true selfbeing.Hakuna aliyekamilika ila mwenye upendo wa dhati atakukubali jinsi ulivyo.
 
Ni kuomba Mungu akupe wa ubavu wako.mambo huwa mserereko sana.hata inapotokea kuna changamoto za hapa na pale inakuwa rahisi kutatulika.

Ukimpata wa upendo wa dhati, atakuheshimu,atakuvumilia,na ni rahisi kukusamehe pale utapokosea, na pia atakua muaminifu kwako.

Ukioa ubavu wa mwingine sasa... hakuna rangi utaacha kuiona... shida juu ya shida..

Kwangu mimi nimepata wa ubavu wangu,mapungufu yapo ya hapa na pale ,lakini huwa hayachukui muda mrefu kutatulika, hatujawahi kukaa kikao cha upatanishi kwa miaka yote 10+ .
 
Ninachofahamu mimi ni kwamba, kila mwanamke (mwanadamu) ana changamoto zake lakini mke mwema ni yule ambaye unaweza kubebeana changamoto zenu.

Kama unamjua tangia kipindi cha uchumba kwamba yeye ni mvivu/mchoyo lakini unaweza kuvumilia uvivu/uchoyo wake, basi huyo ndio size yako, kaa naye. Yangu mimi ni hayo tu kaka mkubwa.
Ni sahihi unachokisema mkuu. Hapo kwenye uvumilivu nadhani ndio backbone ya ndoa, maana unavumilia for the rest of life, not only for few years.
 
Ushauri wa bure kwa vijana wa kike na wa kiume ukiwa upo katika harakati za kutafuta jiko hakikisha unaoa/unaolewa mtu ambae unaweza kuvumiliana nae na anayekubali mapungufu yako na anakukubali jinsi ulivyo(anakuheshimu).

Muhimu kati ya yote upendo uwe nanga kuu.

Mkiwa katika mahusiano be yourself's usijifanye kila kitu kiwe perfect kuridhisha upande mwengine (fake personality) show your true selfbeing.Hakuna aliyekamilika ila mwenye upendo wa dhati atakukubali jinsi ulivyo.
Nimekuelewa sana mkuu hapo kwenye faking personality or trying to be perfect. Kwenye mahusiano mengi huwa tunajaribu kufanya baadhi ya vitu vilivyo nje ya uwezo wetu ilimradi kumplease your partner, kumbe hiyo ni mistake?
 
Ni kuomba Mungu akupe wa ubavu wako.mambo huwa mserereko sana.hata inapotokea kuna changamoto za hapa na pale inakuwa rahisi kutatulika.

Ukimpata wa upendo wa dhati, atakuheshimu,atakuvumilia,na ni rahisi kukusamehe pale utapokosea, na pia atakua muaminifu kwako.

Ukioa ubavu wa mwingine sasa... hakuna rangi utaacha kuiona... shida juu ya shida..

Kwangu mimi nimepata wa ubavu wangu,mapungufu yapo ya hapa na pale ,lakini huwa hayachukui muda mrefu kutatulika, hatujawahi kukaa kikao cha upatanishi kwa miaka yote 10+ .
Thanks mkuu. Ni kwa namna gani mmeweze kuishi 10+ years of marriage bila kashkash kubwa za kuitikisa ndoa yenu? I mean how do u avoid kuchokana, visirani n.k. Nini kinachowaweka pamoja na upendo kubaki as if ndio mmeoana?
 
Ni sahihi unachokisema mkuu. Hapo kwenye uvumilivu nadhani ndio backbone ya ndoa, maana unavumilia for the rest of life, not only for few years.
Lakini uvumilivu unaweza kuchoka kama hakuna upendo wa dhati,upendo wa kawaida huisha muda fulani,ila ule wa dgati hubakia,hauna mwisho.upendo wa dhati hubeba kila kitu na kufanya mambo kuwa mepesi.( ya mahusiano).
 
Mpaka watu wanaoana, au tuseme mpaka mwanaume anaamua kumuoa mwanamke fulani, huwa naamini upendo ndio sababu ya kwanza. Ila still ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika, na zilizopo zinalega lega.
 
Bible kwenye Mithali 5 nadhani kuna mistari inasema hivi "heri kuwa wawili kuliko mmoja maana wapata ijara njema kwa Bwana, tena walalapo wawili wanaweza kupata joto, ni rahisi kuvunja kijiti kimoja kuliko vitano" haya maneno hayako hivyo ila yapo kwa mtindo huo.

Hivyo basi, nawashauri sana sana Vijana waoe au waolewe at their early 20's. Ni mateso sana una miaka 40 mtoto ana mwaka mmoja. Na mke anakuaga kivuruge, na ukumbuke kipindi hicho hata performance inaanza kupungua! Kwahio ni stress juu ya stress.

Ukioa ukiwa na 20's ni rahiisi sana kumsoma mwenzio, mkajirekebisha na kuzoeana! Ndoa ni nzuri sana maana at least kuna mtu/watoto wa kukufanya ufanye kazi na uache ujinga ujinga!

Hakuna kitu kinaitwa Mke mwema au Mume mwema, ni suala la kuvumiliana na kumheshimu Mungu! Jishushe na Kubali kukosolewa!
 
Nimekuelewa sana mkuu hapo kwenye faking personality or trying to be perfect. Kwenye mahusiano mengi huwa tunajaribu kufanya baadhi ya vitu vilivyo nje ya uwezo wetu ilimradi kumplease your partner, kumbe hiyo ni mistake?
Big mistake unatakiwa ufanye vitu ambavyo unaweza kuvimaintain ili baadae isilete mtafaruku ukiwa huvifanyi ndio unaonekana muongo kwasababu rangi zako za ukweli zinaanza kuonekana!Kwenye mahusiano yote nashauri watu wawe wakweli na wawazi iwezekanavyo!
 
Back
Top Bottom