Adult Talks: Kwa kupitia ndoa yako. Unawashauri vipi ambao hawajaoa?

Ushauri wa bure kwa vijana wa kike na wa kiume ukiwa upo katika harakati za kutafuta jiko hakikisha unaoa/unaolewa mtu ambae unaweza kuvumiliana nae na anayekubali mapungufu yako na anakukubali jinsi ulivyo(anakuheshimu).
Sasa utamjuaje mtu ambaye unaweza kuvumiliana kabla ya kuishi naye ?
 
Ushauri wangu kwa vijana wa kiume ni huu hapa kutokana na uzoefu wangu katika ndoa :-

1/ Usioe single mother....utanishukuru baadae.

2/ Usioe mwanamke asiye na shughuli yeyote ya kumuingizia kipato.... I mean usioe golikipa (utanishukuru baadae).

3/ Usioe mwanamke asiyesali dini yeyote...... utanishukuru baadae.

4/ Usioe mwanamke uliyetafutiwa au kuunganishwa nae na rafiki yako au ndugu yako yeyote yule tofauti na Mama yako mzazi....... utanishukuru baadae.

5/ Usioe mwanamke ambaye hujawahi kuishi nae (kiunyumba) japo kwa wiki moja...... utanishukuru baadae.

6/ Usioe mwanamke ambaye hapo mwanzo alikua na mahusiano ya kimapenzi na mtu wako wa karibu aidha ndugu yako au rafiki yako..... utanishukuru baadae.

7/ Usioe mwanamke ambaye kwake mitandao ndio kila kitu 24/7. Yaani yuko radhi watoto washinde njaa ila yeye apate bando!!...... utanishukuru baadae.

8/ Usioe mwanamke chapombe au mtu wa clubs na viwanja sana...... utanishukuru baadae.

9/ Usioe mwanamke usiyeifahamu background yake (wazazi na ndugu zake wachache) hata kidogo.... utanishukuru baadae.

10/ Usioe mwanamke anayekuzidi Elimu, Kipato, Cheo a.k.a mabavu..... utanishukuru baadae.
Nukta ya 2,4 na 5,umeandiks uongo wa wazi walio kinyume chake wanalia na kusaga meno.

Mimi mke wangu mkubwa nimetafutiwa,ni goli kipa na sijawahi kuishi nae kinyumba na bado tuko pamoja.

Shida yenu vijana hamjui ni watu gani sahihi wa kuwakabidhi mambo yenu.

Shukrani.
 
Mkuu huu uzi hauwezi kuisha bila mimi kutoa shuhuda na darasa kwa vijana....

Ngoja tumalizie pilika za eid el-fitir kwanza..

Nakubali mkuu Analyse
 
Nukta ya 2,4 na 5,umeandiks uongo wa wazi walio kinyume chake wanalia na kusaga meno.

Mimi mke wangu mkubwa nimetafutiwa,ni goli kipa na sijawahi kuishi nae kinyumba na bado tuko pamoja.

Shida yenu vijana hamjui ni watu gani sahihi wa kuwakabidhi mambo yenu.

Shukrani.
Mkuu according to your marriage experience, unatoa ushauri gani kwa ambao bado hawajaingia kwenye ndoa?
 
Hakuna ndoa nzuri wala ndoa mbaya bali wenye ndoa ndio wanawajibika kuifanya ndoa yao kupitia wao ionekane nzuri ama mbaya..Watu wengi wanaingia kwenye ndoa wakitegemea(kupatiwa/kupata_to get) vitu fulani fulani na sio kutoa(to give) vitu fulani fulani,ukiingia kwenye ndoa elewa kuwa UNATEGEMEWA kutoa na sio old mindset ya kutaka KUPOKEA TU__Unaweza ukasoma majarida yote unayoyafahamu kuhusu ndoa/ kwenda semina zote za ndoa/ kusikiliza shuhuda zote za ndoa lakini 'rest assured' unapaswa UJIPENDE WEWE KWANZA kabla ya KUTAKA KUMPENDA mtu mwingine,unapaswa ujielewe/ujitambue wewe kwanza kabla ya kutaka UWAELEWE watu wengine na kikubwa zaidi ufahamu UNAKWENDA KUTAFUTA NINI KWENYE NDOA(kama vyote vinavyopatikana ndani ya ndoa,wewe unaweza kuvipata nje ya ndoa)?? All together we can take BILL and MELINDA GATES kama our case study,i guess kuna mengi ya kujifunza kwenye mshusiano.
Ikitokea mtu anataka kuoa/kuolewa leo, then akaomba ushauri wako. Using your marriage as example, utamshauri nini?
 
Kila mtu aingie ili akutane nayo huko, hakuna pie katika ndoa, kila ndoa ni unique na ina experience yake tofauti na nyingine.

Ila ukiingia kwa ndoa, epuka kuongea madhaifu ya mwenzako kwa wengine, hata watu wako wa karibu.
Sawa chief
 
Watu wanaamini eti hadi uwe na nyumba, uwe na gari, sijui uwe na uwekezaji gani ndio uoe. Kwa mtazamo wangu ni mistake kubwa sana ila kwa leo wacha tumalize kwanza Idd
Idi ikiisha, uje na nondo zaidi cheif
 
Mkuu according to your marriage experience, unatoa ushauri gani kwa ambao bado hawajaingia kwenye ndoa?
Nawashauri vijana kwanza wabalishe tabia,kama wana tabia mbaya zote waziache kisha waanze kutafuta wenza wenye tabia nzuri.

Lingine vijana wawahi kuoa katika raha miongoni mwa raha za dunia ni kuoa mapema yaani katika umri mdogo.
 
Ndoa Ndoa Ndoa , nakuita hunisiniki kwa nn lakini,hapo zamani ulikuwa ukiitwa mara moja unakuja
 
Back
Top Bottom