Adui wa Taifa kwa sasa ni mmoja tu Uchawa.

Adui wa Taifa kwa sasa ni mmoja tu Uchawa.

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,310
Reaction score
3,629
Nini maana ya uchawa?

- UCHAWA ni UPUMBAVU kwasababu tafsiri ya UPUMBAVU ni kuujua ukweli lakini ukaupindisha.

-UCHAWA unatokana na Mtu kuwa MCHAFU hivyo anatafuta Watu kwa gharama zozote zile wawe wanamsafisha.
 
Hakika
 
Naunga mkono hoja!Kuna jamaa mmoja mtaani kwetu anajiweza kipesa!Sasa akiingia tu bar,kama kawaida Chawa wanajitokeza na yeye Hana baya anawapa mvinyo!
Sasa jamaa akishalewa anakuwaga muongeaji sana,hata aongee upumbuvu,hakuna Katika waliomzunguka anaweza kusema hapa umeboronga!
Yaani ni kuunga mkono tu Kila anachotamka!
Wenye akili Huwa wanakaa naye,wanazipiga za ofa chap chap kabla jamaa hajalewa!Akishaanza kuongea tu,Wanajua tayari!Wanaanza kupokea simu za uongo na kuhama viwanja!Hapo anabaki na machawa OG!
 
uchawa ili uishe nilazima usafi wa kibinafsi(kwa viongozi wetu) kwa maana chawa wanakaa mahali pachafu,

Pia kufanya usafi wa mazingira yanayokuzunguka(Jamii kwa ujumla ifundishwe kuacha kukaa kimya kwenye ubaya kisa tu unanufaika na ubaya unaofanyika
 
Chawa ni matokeo tu, swala ni watu wenye nguvu kuingilia mifumo ya utawala na watawala kukubali kuingiliwa maana kwa wao hakuna wanachopoteza kwa maono yao na wanavyoamini.. utawala unashindwa kuamua pale wenye nguvu walipopashika.
 
Nini maana ya uchawa?

- UCHAWA ni UPUMBAVU kwasababu tafsiri ya UPUMBAVU ni kuujua ukweli lakini ukaupindisha.

-UCHAWA unatokana na Mtu kuwa MCHAFU hivyo anatafuta Watu kwa gharama zozote zile wawe wanamsafisha.
Uchawa ni janga kwa taifa, uchawa ni mojawapo ya signs za watu wenye mtindio wa ubongo. Uchawa ni utaahira, uchoko na upumbavu. Uchawa ni uhanithi.
 
Mimi siwezi kuwa chawa wa binadamu mwenzangu. Bora nife masikini.
Tatizo la kimfumo,makuzi ya kijamaa yamechangia dhana ya uchawa kukua kwenye akili za vijana,sasa zama zinapobadilika dhana ya uchawa inaingia kwenye aina nyingine,kama ni zama za kidikteta basi uchawa utainuka kuutetea udikteta,kama ni zama za Uzalendo,uchawa utainuka kuutetea uzalendo,kama ni zama za ufisadi uchawa utainuka kuutetea ufisadi.
 
Kwa hiyo Umaskini, maradhi na ujinga vilisha ondoka? Huo uchawa unaousema ni manifestation ya ujinga tu. Kwa hiyo bado tupo kwenye circle Ile Ile.
 
Back
Top Bottom