Adui wa Saddam Hussein ajutia alichokifanya

Kataskopos

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
16,014
2,000
Huyu bwana anaitwa Kadhim Al-Jabouri,
Anaiambia BBC kwamba alikuwa hampendi Saddam Hussein kwasababu aliua ndugu zake kama kumi na watano. Anaendelea kusema siku ambayo Marekani na Uingereza wanavamia Iraq alishangilia sana na akawa wa kwanza kuchukua nyundo na kwenda kuvunja sanamu la Saddam Hussein.

Anakiri kwamba alihisi kuwa atapata amani na wazungu walitengeneza Propaganda chafu sana na binafsi akazimeza: Lakini tangu kuanguka kwa Utawala wa Saddam Hussein anasema hajawahi kupata amani moyoni mwake na nchi ile imeharibika imerudi kwenye sifuri.

Amesema anajutia sana alichokifanya na kama angekuwa na Uwezo angejenga upya sanamu ya Saddam Hussein pale lakini anashindwa anaona aibu sana na anaogopa kuuwawa. Amesema wanaotawala sasa ni wabaya 1000 zaidi ya Saddam. Angalia hapa chini:

CC: izzo , Dotworld, Bukyanagandi
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,518
2,000
Bado nina kitu kuwa sikufurahia mauaji ya Saddam na Ghadafi, hata tangu waanze kusumbuliwa sikufurahi. Kwa sababu nilijua wananchi wataishi vibaya zaidi. Na ndivyo ilivyo, na inasikitisha. Wazungu hawataacha kuwa wachochezi na waongo kwa kupata wao faida ya wanachotaka. Ila wengine wa Iraq maisha yanaendelea hivyo hivyo na kupenda ya sasa...ni ngumu shaaaaa kila mtu na lwake
 

ISIS

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
91,521
2,000
Bado nina kitu kuwa sikufurahia mauaji ya Saddam na Ghadafi, hata tangu waanze kusumbuliwa sikufurahi. Kwa sababu nilijua wananchi wataishi vibaya zaidi. Na ndivyo ilivyo, na inasikitisha. Wazungu hawataacha kuwa wachochezi na waongo kwa kupata wao faida ya wanachotaka. Ila wengine wa Iraq maisha yanaendelea hivyo hivyo na kupenda ya sasa...ni ngumu shaaaaa kila mtu na lwake
Mzungu kaa naye kwa HEKIMA NA BUSARA! Ukifunga jicho tu anakumaliza! Lakini hakuna kinachomshinda MAULANA!
 

izzo

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,817
2,000
Katika jamii 4 ambazo kwa pamoja ndizo zinaunda Dunia
1 Caucasian race
2 Mongolians (Chinese&Japanese& Koreans)
3 Semitic { Arabs&Indians&Jews}
4 Blacks
Katika jamii zote kuna jamii mbili ambzo zinafanana kuanzia kitabia na kimatendo na hii inatokana na ukaribu wa kijografia au kimuingiliano wa kitamaduni jamii hizo ni Arabs & African Blacks nimeweka African kwa sababu Black ni race si eneo au rangi na wapo blacks ambao hata Africa hawapajui pia ndani ya Africa wapo wazungu ambao wanajiita ni waafrica na wanapassport za nchi za Africa mfano makaburu na pia wapo watu ambao ukiwaangalia kwa macho si blacks lakini wanaitwa blacks kwa vile mzazi mmoja ni black . Sasa Arabs na African blacks ni jamii ambazo zinafanana na ndizo jamiii ambazo zimekosa Democrasia ya kweli japo kuna chaguzi lakini hakuna Democrasia. Democrasia si uchaguzi tu uchaguzi ni kama slice kwenye keki ya Democrasia

Kitendo cha kukosekana Democrasia ya ukweli kinafanya wananchi wanakuwa na visasi mioyoni mwao na hasira zinapozidi na hakuna pa kupunguzia hasira hizo zinasababisha chuki na chuki inazaa uhasama kati ya viongozi na wananchi sasa kunapotokea nafasi au kitundu cha kutolea hasira zao huwa zinatoka kwa nguvu na kasi ambayo inachukua muda mrefu kupungua ndio maana unaona zile nchi za kiarabu zilizoanza mapigano mpaka leo hakuna amani pia ukiangalia nchi za Africa zilizo pigana wenyewe kwa wenyewe hakuna amani ya kweli bali kuna utulivu tu na bahati mbaya kuliko zote jamii hizi haziwezi kujenga kwa maana zimekuwa design kutegemea jamii zingine katika kutatua matatizo yao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom