GE2025 Ado Shaibu anatoa msimamo wa ACT, leo Julai 10, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975

POLISI WAACHE KUINGILIA MCHAKATO WA UCHAGUZI
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea taarifa kuwa Jeshi la Polisi kupitia Makamanda wa Polisi (OCD's) na Maofisa wengine waandamizi wa Polisi wameanza kufanya mawasiliano na viongozi wetu kuwataka kuwasilisha majina ya wagombea wa Ubunge na Udiwani. Tumeelezwa kuwa kwenye baadhi ya maeneo, Wakuu wa Wilaya pia wamekuwa wakiwapigia simu viongozi wetu kuhitaji taarifa hizo.

Maeneo yaliyoripotiwa kwa Jeshi la Polisi kuhitaji taarifa za watiania wa Ubunge na Udiwani ni Kilwa, Kigamboni, Kinondoni, Magu na Tarime.

Hatua hii ya Jeshi la Polisi ni kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi. Hakuna popote kwenye sheria za uchaguzi ambapo Chama cha siasa kinawajibika kuwasilisha kwa Jeshi la Polisi au Mkuu wa Wilaya taarifa za watiania wa vyama vya siasa. Hatua pekee ambayo Chama cha siasa kinapaswa kuwasilisha utambulisho wa wagombea ni kwa Tume ya Uchaguzi wakati wa kuchukua fomu.

ACT Wazalendo inaamini kuwa hatua hii ya Jeshi la Polisi haina nia njema kwenye mchakato wa uchaguzi. Ni hatua ambayo inalenga kuwatisha au kuwalaghai wagombea wetu.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA
1. ACT Wazalendo tumemuandikia Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Wambura kumtaka kusitisha zoezi hilo haramu linaloendelea nchi nzima. Ni imani yetu kuwa ili kujiepusha kuingilia mchakato wa uchaguzi, Jeshi la Polisi litasitisha mara moja hatua hii.

2. ACT Wazalendo tumemuandikia Msajili wa Vyama vya Siasa kulalamikia hatua hii ya Jeshi la Polisi na Wakuu wa Wilaya na kuomba hatua ichukuliwe kuzuia vitendo hivi.

3. ACT Wazalendo kimewaandikia viongozi wake nchi nzima kuwataka wasitekeleze wito wa Jeshi la Polisi wa kuwasilisha taarifa za wagombea kwa Jeshi la Polisi.

4. ACT Wazalendo tumeiandikia Tume ya Uchaguzi nchini (INEC) kuitaka kutoa tamko kwa Jeshi la Polisi kutoingilia mchakato wa uteuzi wa ndani ya vyama vya siasa.

WITO NA MSIMAMO WETU
1. ACT Wazalendo tunalitaka Jeshi la Polisi kuacha zoezi lake la kuwasiliana na viongozi wetu majimboni kuhitaji taarifa za wagombea kwa sababu zoezi hilo ni kinyume na sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.

2. Viongozi wa ACT Wazalendo wameagizwa kutotoa taarifa kwa Jeshi la Polisi zinazohusu wagombea wa ACT Wazalendo.

3. ACT Wazalendo tumeamua kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 tukipambania mageuzi hadi dakika ya mwisho. Hatutaacha kuzikumbusha na kuziwajibisha mamlaka mbalimbali katika kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu unakuwa huru, wa haki na wa kuaminika. Tutafanya hivyo bila hofu.

ACT Wazalendo, Taifa kwanza leo na kesho.
Imetolewa na;
Ado Shaibu
Katibu Mkuu ACT Wazalendo
10 Julai, 2025.

1752150893852.png

1752150911958.png
 
Huyu Ado Shaibu tangu ajidhalilishe mbele ya wabunge wa CCM akidhani watamchagua kuwa Mbunge wa Bunge la Africa Mashariki huwa namuona kama msaka tongue. Akawalamba miguu wabunge wa CCM halafu kwenye kupiga kura wakampiga Chini. Bado hajajifunza.
 
POLISI WAACHE KUINGILIA MCHAKATO WA UCHAGUZI
Chama cha ACT Wazalendo kimepokea taarifa kuwa Jeshi la Polisi kupitia Makamanda wa Polisi (OCD's) na Maofisa wengine waandamizi wa Polisi wameanza kufanya mawasiliano na viongozi wetu kuwataka kuwasilisha majina ya wagombea wa Ubunge na Udiwani. Tumeelezwa kuwa kwenye baadhi ya maeneo, Wakuu wa Wilaya pia wamekuwa wakiwapigia simu viongozi wetu kuhitaji taarifa hizo.

Maeneo yaliyoripotiwa kwa Jeshi la Polisi kuhitaji taarifa za watiania wa Ubunge na Udiwani ni Kilwa, Kigamboni, Kinondoni, Magu na Tarime.

Hatua hii ya Jeshi la Polisi ni kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi. Hakuna popote kwenye sheria za uchaguzi ambapo Chama cha siasa kinawajibika kuwasilisha kwa Jeshi la Polisi au Mkuu wa Wilaya taarifa za watiania wa vyama vya siasa. Hatua pekee ambayo Chama cha siasa kinapaswa kuwasilisha utambulisho wa wagombea ni kwa Tume ya Uchaguzi wakati wa kuchukua fomu.

ACT Wazalendo inaamini kuwa hatua hii ya Jeshi la Polisi haina nia njema kwenye mchakato wa uchaguzi. Ni hatua ambayo inalenga kuwatisha au kuwalaghai wagombea wetu.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA
1. ACT Wazalendo tumemuandikia Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Wambura kumtaka kusitisha zoezi hilo haramu linaloendelea nchi nzima. Ni imani yetu kuwa ili kujiepusha kuingilia mchakato wa uchaguzi, Jeshi la Polisi litasitisha mara moja hatua hii.

2. ACT Wazalendo tumemuandikia Msajili wa Vyama vya Siasa kulalamikia hatua hii ya Jeshi la Polisi na Wakuu wa Wilaya na kuomba hatua ichukuliwe kuzuia vitendo hivi.

3. ACT Wazalendo kimewaandikia viongozi wake nchi nzima kuwataka wasitekeleze wito wa Jeshi la Polisi wa kuwasilisha taarifa za wagombea kwa Jeshi la Polisi.

4. ACT Wazalendo tumeiandikia Tume ya Uchaguzi nchini (INEC) kuitaka kutoa tamko kwa Jeshi la Polisi kutoingilia mchakato wa uteuzi wa ndani ya vyama vya siasa.

WITO NA MSIMAMO WETU
1. ACT Wazalendo tunalitaka Jeshi la Polisi kuacha zoezi lake la kuwasiliana na viongozi wetu majimboni kuhitaji taarifa za wagombea kwa sababu zoezi hilo ni kinyume na sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi.

2. Viongozi wa ACT Wazalendo wameagizwa kutotoa taarifa kwa Jeshi la Polisi zinazohusu wagombea wa ACT Wazalendo.

3. ACT Wazalendo tumeamua kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 tukipambania mageuzi hadi dakika ya mwisho. Hatutaacha kuzikumbusha na kuziwajibisha mamlaka mbalimbali katika kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu unakuwa huru, wa haki na wa kuaminika. Tutafanya hivyo bila hofu.

ACT Wazalendo, Taifa kwanza leo na kesho.
Imetolewa na;
Ado Shaibu
Katibu Mkuu ACT Wazalendo
10 Julai, 2025.

Uyu ndungu hakutakiwa awe ACT, chama kinamuangusha japo anapata maokoto
 
msiamamo unajulikana watalinda kura
 
Makamanda wa Polisi (OCD's) na Maofisa wengine waandamizi wa Polisi wameanza kufanya mawasiliano na viongozi wetu kuwataka kuwasilisha majina ya wagombea wa Ubunge na Udiwani. Tumeelezwa kuwa kwenye baadhi ya maeneo, Wakuu wa Wilaya pia wamekuwa wakiwapigia simu viongozi wetu kuhitaji taarifa hizo.
Kwani Shaibu alikuwa hajui kama policcm ni idara ya chama?

ACT ni chawa, hawaaminiki. Hiko kilio itakuwa sinema ya kupumbaza watu tu.

No Reforms No Election..
 
Nyie ACT Wazalendo nyie, ina maana hamjatambua tu kuwa RCs, DCs, DEDs, TCDs, CCDs, RPCs na OCDs chini ya mfumo huu wa uchaguzi unaotakiwa kubadilishwa, virtually nao ni sehemu ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa..?

Nyie ACT WAZALENDO ina maana mpaka leo hamjui dhana, maana na lengo la NO REFORMS NO ELECTION? Kama mlikuwa hamjui, maana yake ndiyo hii sasa ambako kabla hamjafikia robo ya safari ya kuifikia siku ya uchaguzi, CCM wanatamba kuwa tayari wameshinda kwa 99.99%...

Hata mlinde kura mkitumia uchawi wa Kigoma na Sumbawanga kote, hamtaweza kupata hata kito kimoja cha ubunge au udiwani unless otherwise muuze roho na utu wetu kwa CCM wawape chochote...!!
 
Back
Top Bottom