Katibu Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu ameahidi , akipewa ridhaa na wananchi atapigania masilahi ya wakulima kwa kuhakikisha wanapata pembejeo za kilimo kwa wakati na bei nzuri za mazao yao
Akihutubia katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Baraza la Idd, Tunduru Mjini, jana Septemba 7, 2025, Ado amesema mfumo wa stakabadhi ghalani umeshindwa kumkomboa mkulima badala yake umeendelea kuwaumiza kwa kuchelewesha malipo na kushindwa kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo bora
“Wakulima wa Tunduru ndio uti wa mgongo wa uchumi wa jimbo hili. Kipaumbele changu kikuu kitakuwa kuwatetea ili wapate pembejeo kwa bei nafuu, malipo ya uhakika na kuhakikisha mazao yao yanapata thamani wanayostahili,” amesema Ado
Amesema ACT-Wazalendo itaendelea kusimama na wakulima wa Tunduru kwa kutafuta mbinu mbadala zitakazoongeza kipato chao na kuondoa changamoto zinazowakandamiza kwa miaka mingi