Ado Mapunda RAS-Arusha alitumbuliwa Kateuliwa tena RAS- Mara

Ado Mapunda RAS-Arusha alitumbuliwa Kateuliwa tena RAS- Mara

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Posts
2,282
Reaction score
1,253
Sikuamini macho Na masikio yangu Juu ya kuteuliwa tena Kwa Bw.Ado Mapunda kuwa Ras Mara wakati alikwisha tumbuliwa.Ninapata shaka kuwa inawezekana wasaidizi wa Rais walimdanganya wakati anamtumbua au wamemdanganya hivi sasa wakati anamteua tena.Ni vema Ikulu ikawa makini katika teuzi zake kwani kumteua MTU uliyemtumbua Na Kumrudisha tena ktk nafasi ile ile kunahitaji ufafanuzi.
 
Pole Sana Mkuu Nadhani Unatakiwa Kuielewa Awamu Hii Vizuri Pia Huyo Asikushangaze
Subiri Sana Uje Usikie Ya Dg Mstaafu Wa Nssf Ndg Dau
Ambaye Anangoja Kwenda Job Huko Walikomkataa Kwa Tetesi

Hivyo Ni Viwanda Mkuu
 
Tulikesha usiku kucha tunapitia majina yote ya watakao teuliwa, Mleta Uzi usinijaribu, Mimi ni tofauti, sijaribiwi
Nchii Lazima Iende Endeleeni Kuniombea Sana
 
Hii Nchi Iko Tambarare Kama Ujio Wa Masihi
Kwenye Mlima Pashushe Kwenye Bonde Pajazwe Ili Mambo Yaende Tumelegeza Mashavu Tunangoja Viwanda
Lazima muambiwe ukweli, Msema kweli ni mpenzi Wa Mungu. Ndoto ni usiku tuu, mchana kazi.
 
Asilimia kubwa ya waliotumbuliwa wamesharudiahwa makazini kimya kimya.Nchi kuongozwa kisiasa
 
Mama Malechela sijui zamu yake lini.
 
Mara ni kituo cha mwisho kwa ajira ya kuteuliwa, akumbuke ya Malongo aende akiwa amejipanga.
 
Hakuna binadamu aliye kamilika kila mwenye kutubu nakuombea msamaha husamehewa
 
Sikuamini macho Na masikio yangu Juu ya kuteuliwa tena Kwa Bw.Ado Mapunda kuwa Ras Mara wakati alikwisha tumbuliwa.Ninapata shaka kuwa inawezekana wasaidizi wa Rais walimdanganya wakati anamtumbua au wamemdanganya hivi sasa wakati anamteua tena.Ni vema Ikulu ikawa makini katika teuzi zake kwani kumteua MTU uliyemtumbua Na Kumrudisha tena ktk nafasi ile ile kunahitaji ufafanuzi.
Wale ma RAS, DAS, DED wote aliowatumbua pamoja na watendaji wengine wanaendelea kula mishahara kama kawaida. Ndiyo maana pamoja na kuondoa watumishi hewa bill ya salary imeongezeka badala ya kupungua sasa kujikosha inabidi awateue tena aliowatumbua ili kupunguza maumivu ya gharama. Maana kagundua hamna alichofanya kwenye kubana matumizi kwani kila teuzi mpya ina gharama mpya na wakati huo huo kila teuzi aliyoitumbua inaendelea kula salary kama kawaida.

Hii serikali ni sawa na comedy show. Kila siku kituko kipya
 
Tunamsubiri yule mkuu wa mkoa wa Morogoro aliyelia , pia kusamehewa
 
Back
Top Bottom