Adhabu za wanajeshi

Mataifa ambayo yana amani ndio utasikia hizi habari za adhabu Kali za RAIA kutoka kwa wanajeshi na hii ni sababu watu wamekuwa trained mda mrefu mambo ya kivita na bila kuiona vita yenyewe kwa hiyo watu wanakuwa na kihemu hemu cha demonstrate waliyojifunza .Dawa pekee ya kuondoa hii ni serikali kuhakikisha wanajeshi wenye balehe ya uwanajeshi wanashiriki utunzaji Wa amani katika katika mataifa yenye machafuko ya kisiasa.
 
Jeshini unapotoka mafunzoni kunakuwaga na kimuhe muhe flani na munkari wa kijinga, usipojizuia unaweza kuleta madhara uraiani hasa unapochokozwa.

Rafiki zangu wawili waliwahi fanya ukatili sana.
Mmoja alimkata kibaka vidole vya mkono.
Mwingine alimvunja kijana mtukutu mguu.
Lakini kwasasa ni wapole sana na wana rank...nzuri so wametulizana
 
Huo waliofanya huwezi kuuita ukatili kaka. Huyo vibaka na huyo kijana mtukutu huwezi kujua walitaka kumdhuru vipi huyo jamaa yako. Vijana watukutu na vibaka ni washenzi mno kwenye anga zao, ilikuwa ni haki yao kufanywa waliyofanywa. Usiuite ukatili mkuu.
 
Huna unachojua usijidai mjuaji
 
Wewe kila kitu unabisha,ulipitia malezi mabaya,wazaz wako wanashida mahala
 
Mie mwenyewe sikubali mtu anizalilishe kisa eti ni mjeda na Kuna wajeda wengine huzalilisha Hadi watu umri wa kuwazaa kabisa eti kisa mjeda. Jamani Mimi sifanyi adhabu yoyote tuone ka wataniua
Ukigoma kupewa adhabu hawakufanyi lolote, maana watahisi wewe ni mzaliwa wa mjini, unajielewa na unafahamu haki zako na pengine unajua sheria kabisa.

So wataishia kukupiga piga mkwara fulani mwisho wa siku watakuacha uondoke kwa kukupa onyo kwamba siku nyingine usirudie kufanya kosa ulilolifanya siku hiyo.

Wakuja akiona gwanda tu anakimbilia kulia na kumshika miguu mjeda mwenyewe kwamba amsamehee, na mjeda akiona hivyo ana take advantage ya kumuonesha kwamba yeye ni nani kwa kumpa adhabu ambazo zipo kinyume na sheria.
 
Mjeda unafurahia jinsi mnavyowahenyesha raia.
 
Kumbe inawezekana kuwashtaki kunawale wa kututishia tidhia kutukosesha amani dawa Yao n ipi😀
Wanajeshi wengi huwa hawajui sheria atakunyanyasa akikutana na wewe ambae umelelewa kwenye misingi ya uoga uoga ila ukikomaa nae mwisho huwa wanaomba radhi na hata fidia unalipwa maana anajua kazi yake inaenda kuharibika

Kuna askri mmoja wa jwtz private ndugu yake aligongwa na pikipiki baada ya kugongwa na pikipik kesi ilienda hadi mahakamani kesi ikaisha kwa maamuzi ya mahakama lakini aliegongwa akawa bado anaendelea na matatibabu.

Jamaa huyo private wa jwtz akiwa likizo alichoamua kukifanya akiwa yupo likizo akaenda kumkamata yule jamaa aliemgonga ndugu yake na baada ya kumkamata akaenda kumfungia kwao hilo Ni kosa la kwanza alifanya kinyume na sheria(utekaji)

Kosa la pili akiwa anamuhoji akampiga yule jamaa akishinikiza kuwa jamaa amuhudumie mgonjwa wao hilo ni kosa la pili (shambulio la kudhuru mwili) kilichotokea hapo ni kuwa ndugu wa yule ndugu yao ambae amefanyiwa hivyo walikua wanajua haki zao wakakusanya ushahidi wote na mashahidi wakawepo ndugu yao alivyoaachiwa tu akiwa na majeraha wakaenda kuchukua pf 3 polisi ikaenda kuthibishwa na daktari kuwa jamaa kweli kashambuliwa na kapata madhara (hapa tayari shahidi wa 3 ambae ni daktari kapatikana)

Baada ya kutoka hospitali Sasa wakaenda kufungua kesi ya shambulio polisi kwakua ushahidi wote upo polisi ikabidi waende kumkatamta katika kumuhoji kumbe kweli alikua ni Askari wa jwtz, kilichotokea hapo taarifa ikatumwa kikosini kwake, utaratibu ulivyo ni kuwa Askari yeyote hapelekwi mahakama za kawaida kwa makosa ya jinai hadi kwanza apitie mahakama za kijeshi na afukuzwe kwanza kazi ndo apelekwe akiwa kama raia wa kawaida

Hali ilipofikia hapo na ndugu wa yule mwanajeshi wakaona kibarua cha mtoto wao kinaenda kuharibika ikabidi wajishushe wakaenda kuomba msamaha kwa yule alieshambuliwa wakabembeleza sana ili aifute hiyo kesi mwisho jamaa alikubali akapokea fidia lakini muda huo yule private wa jeshi kashakaa lockup ya polisi siku 6 maana utaratibu ilikua kikosini kwake ndo waje wamchukue lakin hawakuja kwa siku zote 6

Baadae kesi ilifutwa lakin Kama jamaa wangekomaa nae alikua anaenda kufukuzwa kazi kwasababu ameiingilia hadi mahakama kwa kesi ambayo ilishatolewa maamuzi,lakin pia alifanya makosa ya jinai kuteka na kushambulia

Sasa watu wanatakiwa wajue haki zao na siyo kutishwa tishwa wanakua Kama kondoo mwisho wa siku tunakua na taifa la wajinga
 
We jidanganye, kwa taarifa yako hayo yana badaka za wakubwa hayo.
 
Akiwa Askari eneo la kazi na wewe umeenda ndivyo sivyo eneo hilo hata kesi ifike wapi hakuna litakalofanyika
 
Sa kilometa 50 sinaishilia huko huko ata hivyo mi sifanyi nawaambia nipelekeni mahakamani kama hamtaki niueni mnile na nyama kabisa
 
Kingekuwa kijiwe cha kawaida siyo wangesumbuliwa tu Kama ulivyoandika,bali pia wangewekewa Hadi vipisi vya bangi mifukoni na mitama wangechezea na kwenye difenda mngepanda.

Mimi nilishawahi kuchanganywa kwenye kundi la wazurulaji kisa tu nilikuwa napita njia naelekea stendi,huko chochoroni polisi wakawakurupusha wahuni,ile kimbizana wakamchanganya kila mtu waliyekutana naye mbele Hadi mpita njia,Mimi nikiwemo. Ile siku nilimind vibaya mno,nikakunjana na Askari ila akaja afande mmoja akasema "afande sogea nimshuti huyo jambazi aliyetuvamia tusifanye kazi yetu". Nikawa mpole na mikono juu ila jamaa hakuridhika,akanitia kibao Cha sikio shadi nikawa sisikii.

Ile siku nililala chang'ombe polisi nikaja kutolewa asubuhi na fine 50k ya uzurulaji. Askari wa bongo waonevu na wanateteana Sana,nashangaa wanaopigizana kelele humu eti sababu wabongo hatujui haki,Askari akikuletea za kuleta unamchukulia hatua za kisheria.
 
Nenda kauze Vitumbua Jeshini..Alafu uviite vitumbua vya kijeshi
Au jeshi lenye vitumbua
..Utakuja kusimulia hapa
 
Nimecheka Sana asee.
 
Huna unachojua usijidai mjuaji
Wewe unajua nini ulichoandika kipo kwenye CPA na imeelezwa vizuri Kanuni ya Adhabu pia imeelezea adhabu zipi zitolewe kwa wanaoenda kinyume na sheria zilizowekwa kwa ulinganifu na CPA, unapoelezea sheria ujue na statue zake sio kukariri tu kwenye Kibanda Cha kashata na kahawa ukisikia hili umenasa km sumaku

CPA ni Criminal Procedure Act [R.E 2002]

Nisije nikawa nakuchanganya ubongo
 
Mie nimekosea sitaki kuzalilishwa waniadhibu kiutaratibu na ikiwa mwanaume namgeuzia kesi kabisa yakutaka kunibaka kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…