Adhabu ya kifo hadharani nchini Saudi Arabia

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
26,267
2,000
Saudi Arabia ni moja kati ya nchi nne pekee ambazo bado zinatekeleza adhabu ya kifo hadharani. Nchi nyingine ni Iran, Korea Kaskazini na Somalia.

Nchini Saudi Arabia, serikali ya kifalme inatekeleza adhabu hii kwa msimamo kwamba wanatekeleza shari'ah kama ambavyo imeelekezwa katika Qur'an Tukufu.

Hivyo basi ikitokea raia amefanya kosa ambalo linapaswa aadhibiwe kifo, adhabu hii inatekelezwa kwa mtu huyo kuchinjwa hadharani kwa upanga.

Jambo hili limekuwa linaleta shida sana kati ya Saudi Arabia na watu wa haki za binadamu. Kuna makosa ambayo raia wa Saudi Arabia wanachinjwa hadharani ambayo hata wanazuoni wengi wanaamini kwamba hayako sawa kidini bali ni juhudi za Ufalme wa Saudia kuwaziba midomo raia 'vimbele mbele'.

Kwa mfano moja ya utata mkubwa kuhusu adhabu hii ya kifo hadharani ikitokea baada ya polisi wa Saudi Arabia kuwakamata vijana wawili walioitwa Ali al-Nimr na rafiki yake Dawoud al-Marhoon kwa kosa la kuandamana mwaka 2011 kupinga utawala wa Kifalme nchini Saudi Arabia. Kipindi vijana hawa wanakamatwa walikuwa na miaka 17 pekee.

Siku chache baadae alikamatwa muhubiri wa kiislamu maarufu nchini humo kipenzi cha vijana anayeitwa Sheikh Nimr al-Nimr (mjomba wake Ali al-Nimr) kwa kosa la kutoa mawaidha yenye maudhui ya kupinga serikali.

Wote hawa walikamatwa mwaka 2011 na 2012, na mpaka kufikia mwaka 2015 wote walikuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo kwa kuchinjwa hadharani.

Hukumu hii iliamsha hasira kubwa ya mashirika ya binadamu mpaka kufikia hatua utekelezaji wa adhabu kwa watuhumiwa hawa watatu ukasogezwa mbele, lakini bado wangali gerezani wakisubiria kuchinjwa siku yoyote ile.

(Sheikh Nimr al-Nimr walichinjwa mwaka jana, January 2, 2016 pamoja na raia wengine 47 kwa pamoja). Lakini kila hii haimaanishi kwamba hakuna watu wanaochinjwa kila siku kwa amri ya serikali ya Saudi Arabia.

Tumezoea kuona vyombo vya habari vikiripoti kuhusu ukatili wa kikundi cha ISIS kutokana na kuwachinja mateka wao wakiwa wanawarekodi, lakini uhalisia ni kwamba serikali ya Saudi Arabia inachinja watu wengi zaidi kuliko ISIS.

Pengine habari za ukatili huu unaotekelezwa na serikali ya Saudi Arabia haukemewi sana kwenye vyombo vya habari kutokana na uswahiba wa serikali hiyo na mataifa ya kimagharibi yakiongozwa na Marekani.

Mfano mwaka 2011 inakadiriwa kuwa watu 26 walichinjwa hadharani.
Mwaka 2013 zaidi ya watu 78 walichinjwa hadharani.
Mwaka 2015 jumla ya zaidi ya watu 158 walichinjwa hadharani.
Mwaka 2016 zaidi ya watu 153 walichinjwa hadharani, ambapo watu 47 kati ya hao walichinjwa kwa pamoja (mass beheading) siku ya January 2, 2016.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,108
2,000
Umeitaja Qur'an Tukufu. Tafadhali weka nukuu ya Qur'an yenye "Sharia" hiyo uisemayo.
"Nchini Saudi Arabia, serikali ya kifalme inatekeleza adhabu hii kwa msimamo kwamba wanatekeleza shari'ah kama ambavyo imeelekezwa katika Qur'an Tukufu".

Hiyo sentensi wewe unavyoiona hayo ni maneno au madai yake mpaka umdai athibitishe kwa kuonyesha aya kutoka kwenye Quran?
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,323
2,000
"Nchini Saudi Arabia, serikali ya kifalme inatekeleza adhabu hii kwa msimamo kwamba wanatekeleza shari'ah kama ambavyo imeelekezwa katika Qur'an Tukufu". Hiyo sentensi wewe unavyoiona hayo ni maneno au madai yake mpaka umdai athibitishe kwa kuonyesha aya kutoka kwenye Quran?
Naam. maana si kila wafanyalo Saudia ni Sharia, zingine ni sheria.

Tunaomba huu uthibitisho kutoka Qur'an kwa kuwa kaitaja Qur'an.

Au kila lifanywalo Vatican limeamrishwa na biblia?
 

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,108
2,000
Naam.maana si kila wafanyalo Saudia ni Sharia, zingine ni sheria.

Tunaomba huu uthibitisho kutoka Qur'an kwa kuwa kaitaja Qur'an.

Au kila lifanywalo Vatican limeamrishwa na biblia?
Kwa maoni yangu mimi nadhani ungemdai aonyeshe ni wapi Saudia waliwahi kutoa kauli hiyo. Maana maelezo yake yanainyesha yeye hajainukuu Quran bali kawanukuu Saudia.
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
26,267
2,000
Naam.maana si kila wafanyalo Saudia ni Sharia, zingine ni sheria.

Tunaomba huu uthibitisho kutoka Qur'an kwa kuwa kaitaja Qur'an.

Au kila lifanywalo Vatican limeamrishwa na biblia?
Katika mahojiano ya nadra sana ambayo aliyafana na Arab News mwaka 2003 al-Beshi aliwahi kueleza kuwa yeye si mtu katili kwa sababu ya kazi anayoifanya, kwani anajisikia fahari kufanya kazi hiyo ya mchinjaji kwa kuwa anaamini anafanya kazi ya mwenyezi Mungu kama ilivyoagizwa kwenye vitabu.

Pia anaendelea kujitetea kwamba kazi yake haimtengi na jamii kwa kuwa ana marafiki wengi msikitini na mtaaani, pia ana ndugu na jamaa ambao wanampenda na kumuelewa juu ya chaguzi yake hiyo ya ajira.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
26,267
2,000
Umeitaja Qur'an Tukufu. Tafadhali weka nukuu ya Qur'an yenye "Sharia" hiyo uisemayo.
Nchini Saudi Arabia, serikali ya kifalme inatekeleza adhabu hii kwa msimamo kwamba wanatekeleza shari'ah kama ambavyo imeelekezwa katika Qur'an Tukufu.

Hivyo basi ikitokea raia amefanya kosa ambalo linapaswa aadhibiwe kifo, adhabu hii inatekelezwa kwa mtu huyo kuchinjwa hadharani kwa upanga.

Makosa ambayo yanaweza kupelekea mtu kuhukumiwa kifo ni pamoja na Kuua, usagaji, ushoga/ngono kinyume na maumbile, ubakaji, uzinzi, biashara ya mihadarati, ukahaba, uasi wa dini au kisiasa, kuabudu sanamu, ujambazi wa silaha, wizi wa kawaida (akiiba mara nne), kukufuru, uchawi na ulozi.

Japokuwa kumekuwa Ufalme wa Saudi Arabia umekuwa ukijitetea kuwa wanatekeleza hilo kwa mujibu wa maagizo ya vitabu vitukufu, lakini watu wengi wamekuwa wakitafsiri adhabu hizi za kuchinja watu hadharani kama njia ya kujenga hofu mioyoni mwa wananchi ili waweze kutii kila jambo ambalo linaamuliwa na mfalme wa Saudi Arabia na wasiweze kuhoji chochote.

Wajuzi zaidi wa elimu ya dini wanaweza kutujuza zaidi kuhusu hili, lakini binafsi kwa kadiri nilivyotafiti, nilichokiona kwamba hukumu nyingi za watu nchini Saudi Arabia juu ya kuchinjwa hadharani, japo zinatolewa kwa mtazamo wa kidini lakini zinaegemea zaidi katika upande wa aina za hukumu za Tazir badala ya Hudud.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kakamkubwa

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
1,182
2,000
Mkuu, kwani kuna sehem umeona nimeuliza swali??
Ama kuna nukuu umesoma niki demand nitakavyo mimi??

Sent using Jamii Forums mobile app
Jibu swali langu kama lilivyo mkuu,kwa chapisho ulilokuja nalo lipo kwa mtindo wa nukuu. Ila mpaka umekuja nalo hapa jukwaani inaonekana unakubaliana na tuhuma zilizotajwa juu ya serikali ya Saudi Arabia. Au wewe ulitaka tumuulize nani wakati chapisho umelileta wewe?
 

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,108
2,000
Sky Eclat na mpiga debe wako anaejiita Consigliere tunataka mtupe wa ushahidi wa hili uliloandika post namba moja...

"Allah address the human race by saying… “Verily, we have honored the sons of Adam, they will be a commodity that is bought and sold like mules”.

Wapi yamesemwa hayo na "Allah"?
Sijamuona Sky Eclat kwenye uzi huu, sasa sijui unamdai vipi ushahidi wa kile unachodai ameki post humu. Pia, mimi mwenyewe nahisi kama umenikosea kunidai ushahidi wa jambo unalonihusisha nalo ambalo wala sija post.
Kingine, mimi sijawahi kuwa mpiga debe wa Sky Eclat labda kama umegundua kuwa nafuatilia sana michango yake ni sababu ni michango yenye tija na mashiko, pia, kupitia michango yake nimeona kwamba she is substantive woman.
Mwisho, mbali ya kwamba nina kukukubali wewe sana, pia kumbuka wewe ni wangu tu, hivyo usimjengee wivu wa bure Sky Eclat
Misingi ya dini unayoisimamua hahitaji hoja bali kuamini tu, ukiweka dini pembeni mbona kichwa yako ipo njema sana tu.
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
26,267
2,000
Jibu swali langu kama lilivyo mkuu,kwa chapisho ulilokuja nalo lipo kwa mtindo wa nukuu. Ila mpaka umekuja nalo hapa jukwaani inaonekana unakubaliana na tuhuma zilizotajwa juu ya serikali ya Saudi Arabia. Au wewe ulitaka tumuulize nani wakati chapisho umelileta wewe?
Mtume Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam amesema: “Si halali (kumwaga) damu ya Muislamu isipokuwa kwa matatu; Nafsi kwa nafsi (Aliyeua auwawe), na mzinzi
'thayyib' (aliyekwishaoa au kuolewa) na aliyeacha dini akafarikiana na kundi." [al-Bukhaariy na Muslim]

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
2,018
2,000
Baadh ya hizi dini ni hatri hata kuzidi Corona, ni hatari kwa taifa la kisasa bado kuendelea kuendeshwa kwa dini ya chuki.
Wanakuambia ndio Dini inayokuwa kwa kasi zaidi Duniani. Ndio maana nawakubali sana China hawakubali hii cancer nchini kwao. Eti wanakosolewa haki za binadamu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom