meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,464
- 4,830
kwa wale wakazi wa maeneo ya kaskazini hasa Arusha na Moshi mtakubaliana na mimi kuwa pamoja na kuipinga ccm,miundo mbinu yake na rasilimali watu iliyonayo bado Lowassa alikuwa anapata sympathy kutoka kaskazini hasa baada ya kikundi fulani cha UVCCM kutamka rais wa 2015 hatatoka kaskazini.
kuna baadhi ya watu waliiona kauli hii ni ya kuwatenga watu wa kaskazini hivyo kujiweka tayari kwa kuunga mkono upinzani(CDM) au ikishindikana kabisa bora liende wamuunge mkono Lowassa.
kwa hivi karibuni tunamuona mzee huyu akiongeza nguvu za kampeni kupitia makundi mbalimbali ya kijamii.Tunamuona akipigana kufa na kupona ikiwa ni mapema kabisa ili kujijengea mtandao.
Nimeshangazwa sana na kitendo cha mzee huyu kujihusisha na mtu anayetuhumiwa na jamii kwa matendo maovu ya kingono na kikatili.
Jambo hili limempunguzia imani aliyoanza kuirudisha na ni pigo kubwa kwake.
mfano :kitendo cha kinyama alichofanyiwa mbunge wa Arumeru Mashariki huko makuyuni kimelaaniwa sana hasa hasa huko meru ambapo Lowassa ni wa asili ya huko na bado alikuwa na influence kwa kiasi kikubwa.
Je kuna mtu nyuma ya Mwigulu kaliyemtuma kuja kumuharibia Lowassa?