ADC yavunja Ngome ya CUF Zanzibar, Wanachama zaidi wajitoa

anaanzisha thread halafu yeye mwenyewe ndio mchangiaji mkuu teh teh teh.Namuunga mkono yule aliyesema akili za kigala bhana biskuti wanasema ni mwili
Ukitaka kuua nyoka PIGA kichwani.....Aluta continue, bado Pemba sasa na itawadia tu! Just a matter of time.
 
Hakuna ndoa ya kweli na CCM ikatimia, kuna hatari maalim Seif akaishia kubaya. Sema tu aliteuliwa na Rais, na anaweza kufukuzwa na Rais wakati wowote nguvu zikimuishia kabisa.
 
Kuchinjwa lazima iwe ni shingo, mkia ni kukata. Hakuna kazi yoyote kuwajua Wapemba na Wazanzibari, mtandao ni ulimi au sikio tu, ubaguzi, wivu na choyo ndio zao. Hakuna kazi ati kuwajua watu hawa, wanajionyesha wazi. Bila Tanganyika hakuna Zanzibar, tena nawaonea huruma kwa jinsi mnavyolelewa bila Tanzania meshakwisha. Sijapata kuona kanchi kana viongozi wengi kama SMZ, jimbo kama kata kule bara lina Mbunge na Mwakilishi, wote ni walaji tu wakisubiri huruma ya Tanzania kuwalea. Usitake tuseme yote

Mimi nahitaji watu angalau kama wewe ili nipate kuweka 'NONDO' zangu. Wachangiaji wengine wote wanachangia utumbo tu; hakuna cha maana hata kimoja, kuwajibishana na watu kama hao ni sawa na kunoa kisu kikali ambacho unakusudia kukichinjia ng'ombe na badala yake kisu hicho ukakijaribu kwa kukatia migomba!
 
Mimi nahitaji watu angalau kama wewe ili nipate kuweka 'NONDO' zangu. Wachangiaji wengine wote wanachangia utumbo tu; hakuna cha maana hata kimoja, kuwajibishana na watu kama hao ni sawa na kunoa kisu kikali ambacho unakusudia kukichinjia ng'ombe na badala yake kisu hicho ukakijaribu kwa kukatia migomba!

Mpemba mbishi;
Usijiabishe bure Zanzibar inanufaika sana na muungano huu hata Maalim Seif analifahamu hili ndio maana hawezi hata siku kudai kuuvunja muungano; kabla haujamwaga hizo nondo zako fanya ziara sehemu za Tanga na mikoa mingine ya bara utaona ni jinsi gani muungano huu unavyowalea wazinzibar; inaeleweka wazi mpo wachache wenye hulka ya kutaka tamaduni za kiarabu ihali hata huo uarabu wenyewe hamuujui; wenye haki ya kupiga kelele za muungano ni sisi wabara lakini kutokana na ustaarabu wetu tumenyamza kimya tunawaona nyie ni ndugu zetu wa damu; mpo vijana mnaotumiwa na mabwana zenu waliopo uarabuni lakini je hivi ni kweli waarabu wanawathamini kama nyie mnavyojikomba kwao?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
anaanzisha thread halafu yeye mwenyewe ndio mchangiaji mkuu teh teh teh.Namuunga mkono yule aliyesema akili za kigala bhana biskuti wanasema ni mwili

Cdhani kama ni makosa kuchangia thread yako mwenyewe, halafu pita kwny wall yangu utajua kwa nini nachangia in such extent.
 
bado wapemba au na MZEE WA SAWASWA mwenyewe

Safari ni hatua, naamini itafika tu huko Pemba kwani muasisi mwenyewe wa ADC ni wa hukohuko nina hakika lazima atataka iwe ngome yake.....sasa akifanikisha hili sijui ngome ya hao CUFitna itakuwa ipi? Nimepata fununu na Mara huko/Musoma wanaTIMKA.....hii yote ni ADC hii, Dah!
 
hiki adc naona pia ni chama cha wazanzibar,
naona wanakuja kwa mtindo uleule-na tabia zile zile tu
 
Safari ni hatua, naamini itafika tu huko Pemba kwani muasisi mwenyewe wa ADC ni wa hukohuko nina hakika lazima atataka iwe ngome yake.....sasa akifanikisha hili sijui ngome ya hao CUFitna itakuwa ipi? Nimepata fununu na Mara huko/Musoma wanaTIMKA.....hii yote ni ADC hii, Dah!

"Sio kila Mpemba anayetoka Pemba Wapemba hua wanamkubali, Wapemba wana mtu wao. Hauwezi tu kumuokota mtu yeyote ukawapelekea Wapemba na eti ukawaambia kua mtu huyu ni Mpemba mwenzenu munatakiwa mumkubali, katu Wapemba hawana sifa ya kufanya hivyo". Haya ni maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere!
 
Mpemba mbishi;
Usijiabishe bure Zanzibar inanufaika sana na muungano huu hata Maalim Seif analifahamu hili ndio maana hawezi hata siku kudai kuuvunja muungano; kabla haujamwaga hizo nondo zako fanya ziara sehemu za Tanga na mikoa mingine ya bara utaona ni jinsi gani muungano huu unavyowalea wazinzibar; inaeleweka wazi mpo wachache wenye hulka ya kutaka tamaduni za kiarabu ihali hata huo uarabu wenyewe hamuujui; wenye haki ya kupiga kelele za muungano ni sisi wabara lakini kutokana na ustaarabu wetu tumenyamza kimya tunawaona nyie ni ndugu zetu wa damu; mpo vijana mnaotumiwa na mabwana zenu waliopo uarabuni lakini je hivi ni kweli waarabu wanawathamini kama nyie mnavyojikomba kwao?

Chama
Gongo la Mboto DSM

Mkuu nikitembelea UK, Amerika, Canada, Dubai, Oman, Brazil nk na kuwakuta Wapemba wapo kule wanafanya biashara kwa mkururo na pia wamo Serikalini na katika ajira binafsi nisemeje? Hii sio hoja ya hata kidogo na tena inaweza kukushushia hadhi yako; Wapemba wanaweza kuishi na kufanya kazi popote (hata kama hawajaungana na nchi hizo) kama walivyo watu wengine katika dunia hii almuhimu wafute sheria na taratibu za nchi/sehemu husika.
 
"Sio kila Mpemba anayetoka Pemba Wapemba hua wanamkubali, Wapemba wana mtu wao. Hauwezi tu kumuokota mtu yeyote ukawapelekea Wapemba na eti ukawaambia kua mtu huyu ni Mpemba mwenzenu munatakiwa mumkubali, katu Wapemba hawana sifa ya kufanya hivyo". Haya ni maneno ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere!

Wapemba wale wa mwl. Nyerere si hawa wa leo, japo CUF wameonyesha dhamira yao ya kutaka kuendeleza usultani, nimeona post yako moja unazungumzia namna walivyo ji'expose nje ya Pemba, ni kweli na percent kubwa ya wananchi wa pemba kwa namna moja ama nyingine wanawezeshwa na ndugu na jamaa zao walo nje kama Uk, Arabuni na hata America. Tamaduni yao haiwezi kufa just like that lakini exposure wanayopata walotoka ndio huplay role kubwa kwa changes zinazotokea leo.
Usultani hauna nafasi tena na ndio maana CUF wanaweweseka hii leo. Mfano mdogo ni hapo jana Viongozi wa Juu kabisa wa cuf walipotumia Power yao kuzuia ule mkutano wa kujitoa kwa Wanachama usifanyike katika ukumbi wa Bwawani Hotel. End of a day mkutano ukafanyika tena katika ukumbi mzuri zaidi ya ule wa Bwawani.
Tukubaliane kwamba sio kila mpemba ni Mwanachama wa CUF hivyo basi
 
Wapemba wale wa mwl. Nyerere si hawa wa leo, japo CUF wameonyesha dhamira yao ya kutaka kuendeleza usultani, nimeona post yako moja unazungumzia namna walivyo ji'expose nje ya Pemba, ni kweli na percent kubwa ya wananchi wa pemba kwa namna moja ama nyingine wanawezeshwa na ndugu na jamaa zao walo nje kama Uk, Arabuni na hata America. Tamaduni yao haiwezi kufa just like that lakini exposure wanayopata walotoka ndio huplay role kubwa kwa changes zinazotokea leo.
Usultani hauna nafasi tena na ndio maana CUF wanaweweseka hii leo. Mfano mdogo ni hapo jana Viongozi wa Juu kabisa wa cuf walipotumia Power yao kuzuia ule mkutano wa kujitoa kwa Wanachama usifanyike katika ukumbi wa Bwawani Hotel. End of a day mkutano ukafanyika tena katika ukumbi mzuri zaidi ya ule wa Bwawani.
Tukubaliane kwamba sio kila mpemba ni Mwanachama wa CUF hivyo basi

Tatizo si Upemba,
ni uelewa Rate This Hii ni makala
niliyoiandika wiki
iliyopita kujibu makala
ya mwandishi Abdul-
Ghaffar Idrissa katika
gazeti la Nipe Habari la tarehe 20 Novemba
2009 kwa jina la “Je,
tatizo ni huu Upemba
wetu?” Na Mohammed Khelef
Ghassani Itakuwa kosa la
kimantiki ikiwa makala
ya Abdul-Ghaffar Idrissa
‘Je, tatizo ni huu
‘Upemba’ wetu?’
iliyochapishwa na gazeti hili wiki iliyopita,
haikuchangiwa. Na,
kwa hakika, si
kuchangiwa kwa
sababu ya ushindani,
bali kwa lengo la kuweka rekodi sawa ili
wafuatizi wetu waone
pande zote mbili za
shilingi. Nitajitahidi, kadiri
niwezevyo, kuongelea
kilichozungumzwa na
sio kumuongelea
mwandishi wa makala
hiyo. Hata hivyo, kwa kuwa ninachangia kitu
ambacho mimi
mwenyewe
ninahusiana nacho, ni
vyema nikatangaza
kabisa maslahi yangu kwacho. Kwanza, mimi ni
Mzanzibari mwenye
asili ya Pemba ambaye
ninakiamini Chama cha
Wananchi (CUF) si kwa
sababu ya Upemba wangu (maana wako
Wapemba ambao si CUF,
kwa mfano, kama
unavyoweza kumsoma
Abdul-Ghaffar katikati
ya mistari yake), bali kwa kuwa nakubaliana
na kile
kinachosimamiwa na
CUF, yaani mabadiliko
ya kweli katika nchi
yangu ya Zanzibar na Jamhuri nzima ya
Muungano. Pili, na muhimu zaidi,
makala hii inakuja
katika wakati ambao
Wazanzibari
wanaongea wakiwa
wamekaa juu ya daraja linalowakutanisha na
sio tena kupitia nyuma
ya kuta
zinazowatenganisha.
Kwa hivyo, huu ni muda
ambao tunatakiwa, kwa maslahi ya nchi
yetu tukufu, kuangalia
wapi tunakutana na sio
wapi tunatengana. Hata hivyo, kwa
maslahi hayo hayo ya
umoja wa nchi yetu,
lazima tuukane uongo
wote unaosemwa dhidi
ya nchi hii na watu wake (au kundi fulani la
watu hao) kusudi
tukubaliane kuwa
tunakotokea kulikuwa
siko na, hivyo, kwa
pamoja tuione hoja na haja ya kwenda palipo
ndipo. Ni hili tu ndilo linalonipa
uthubutu wa
kuichangia makala
husika, nikiamini
kwamba si watu wa
kundi la kina Abdul- Ghaffar wala wa kundi
langu, ambao
tumefaidika na hali
ilivyokuwa, bali sote
tutafaidika ikiwa
tutakubali mabadiliko katika nchi yetu
tunayoiamini na
kuipenda. Baada ya
dibaji hiyo, ufuatao
ndio mchango wangu. Kwanza, kusema
kwamba serikali za
Chama cha Mapinduzi
(CCM) ziliruhusu mfumo
wa vyama vingi kwa
lengo la kufungua milango ya demokrasia
nchini, ni kuwa
mdhahania zaidi kuliko
kuwa mhalisia. Ni rahisi
zaidi kutoa mifano hai
ya kuthibitisha kuwa serikali hizo
hazikuruhusu mfumo
wa vyama vingi kwa
dhamira njema, bali tu
kwa kuelemewa na
kuzidiwa na shinikizo la ndani na nje. Kwa
hakika hasa, kama
nilivyowahi kuandika
miaka nane iliyopita
kwenye gazeti la Rai,
”Uvyama Vingi wa Tanzania ni Uchama
Kimoja Uliohalalishwa”,
nikimaanisha kuwa
mfumo wetu wa vyama
vingi umewekwa tu
kuhalalisha chama kimoja kushikilia na
kuendelea kubakia
madarakani, na si
vyenginevyo. Si Serikali ya Muungano
(SMT) wala ya Zanzibar
(SMZ), zote zikiwa chini
ya CCM, ambazo
zimewahi kuwa tayari
kwa ajili ya mfumo huu. Hilo limethibitishwa
mara kadhaa kwa kauli
na vitendo vya wenye
mamlaka kwenye
serikali hizo. Wacha
nidondoe mifano michache kuthibitisha
hoja yangu: Mfano
mmoja ni wa kuuawa
kwa mtu wa mwanzo
kabisa kule Shumba
Mjini, wilaya ya Micheweni, Pemba,
wakati akipachika
bendera ya CUF mwaka
1992, na kosa kubwa
likiwa ni hilo la
kupachika bendera halali katika tawi halali
la chama halali cha
siasa. Mfano mwengine ni
kauli ya aliyekuwa
Waziri Mkuu wa SMT
baina ya 1990 hadi
2005, Fredrick Sumaye,
ambaye akiwa Arusha aliwaambia wazi
wafanyabiashara
kwamba anayetaka
mambo yake
yamnyookee na asipate
matatizo kwenye biashara, basi aiunge
mkono CCM. Maana yake
ni kuwa
mfanyabiashara
asiyeiunga mkono CCM
ataharibikiwa. Na huo ndio ukweli! Mfano wa tatu ni kauli
za wawakilishi wawili
wa CCM kwenye Baraza
la Wawakilishi la
Zanzibar katika kipindi
cha 1995 – 2000, Hafidh Ali Tahir na Asha Bakari
Mtama, ambao kwa
nyakati tafauti wakiwa
ndani ya chombo hicho
walisema kwamba
Serikali ya Zanzibar ilipatikana kwa
Mapinduzi, hivyo
haitochukuliwa kwa
vikaratasi,
wakimaanisha kuwa
kura za wananchi katika chaguzi haziwezi
kuiondoa CCM
madarakani. Na huo
ndio umekuwa ukweli
tangu 1995, 2000 hadi
2005 ambapo si kura za wananchi zilizoamua
nani ashikilie na nani
asikamate madaraka ya
nchi! Mfano mwengine ni
kauli ya aliyekuwa
mwenyekiti wa CCM na
Rais wa SMT baina ya
1995 hadi 2005,
Benjamin Mkapa, ambaye alisema
kwamba angelitumia
nguvu zake binafsi na
za dola kuhakikisha
kuwa CCM inaendelea
kubakia madarakani. Na hivyo ndivyo
alivyofanya mwaka
2000 na akarudia
mwaka 2005 kwa
kumwaga vikosi vya
majeshi na silaha nzito nzito kwenye visiwa
vya Zanzibar kama
kwamba nchi iko
kwenye vita. Matokeo ya kauli zote
hizo yalionekana katika
vitendo vilivyofanywa
na vyombo vya dola,
vikosi vya SMZ na
makundi ya vijana tunaowatambua hapa
Zanzibar kama
Janjaweed, ambapo
kwa pamoja wameua,
wamenajisi,
wameharibu na kuiba mali na pia kupiga na
kutesa wananchi wasio
na hatia ndani ya
Unguja na Pemba, baina
ya mwaka 1992 hadi
2005. Lengo ni kulinda Mapinduzi! Nihitimishe nukta hii ya
kwanza kwa kusema
kwamba, serikali
ambayo imeleta mfumo
wa vyama vingi kwa
minajili ya kuwapa watu fursa ya kuchagua
wanaowataka
kuwaongoza, kamwe
isingekuwa ya mbele
kuwafanyia watu hao
vitimbi vya kuwazuia kuitumia haki hiyo. Pili, kusema kwamba
watu wa kisiwa cha
Pemba waliupokea
mfumo wa vyama vingi
kiupotofu ni zaidi ya
kuwadharau. Kwa hakika, kilichotokea
hasa ni kuwa watu
walipelekewa mfumo
wa vyama vingi
uliopotoshwa kama
inavyoonesha mifano ya hapo juu, na hata
hivyo wakajitahidi
kuishi nao kama ulivyo.
Kwamba Wapemba
waliamua kuishi na
mfumo huu kwa kuikataa CCM
kiujumlajumla, huko
hakumaanishi hata
kidogo kwamba
walipotoshwa na
kuzungwa na mmoja wa kiongozi wa CUF,
Maalim Seif Sharif
Hamad, kama
inavyoelekea kuwa hoja
ya Abdul-Ghaffar! Katika Jamhuri hii ya
Muungano wa Tanzania,
si Pemba pekee ambako
watu wameutumia
mfumo huu dhidi ya
chama tawala. CCM imewahi kukataliwa
kijumlajumla kwenye
maeneo ya Uchaggani
mwaka 1995.
Wachagga hawa, kama
ilivyokuwa kwa Wapemba, hawakuwa
wameemewa wala
kughumiwa. Walikuwa
wanaamini kwamba
miaka 30 ya
kutawaliwa na CCM ilishatosha. Sasa
walitaka mabadiliko na
kura zao, waliamini,
zingeweza kuleta
mabadiliko hayo. Hata hivyo, hakuna siku
imewahi kuandikwa
kwamba Wachagga
walikuwa wamezugwa
na Augustine Mrema
kama vile inavyoandikwa dhihi ya
Wapemba wamezugwa
na Maalim Seif. Kwa
nini? Ni kwa kuwa
Mrema ni Mchagga na
Maalim Seif ni Mpemba? Tatizo, kwa hivyo, si
Upemba wa Wapemba,
bali ni mawazo mgando
yasiyoona mbali ya
wachambuzi wa
mambo wasiojuwa mambo. Niliwahi kuandika
kwenye gazeti la Dira
Zanzibar mwaka 2003,
kwamba kuwajua
Wapemba na
wanachokiamini kuna ulazima wa kuvivaa
viatu walivyovivaa wao
na kujuwa wapi na
wapi vinabana. Si suala
tu la kuwa na kutokuwa
Mpemba, bali ni suala la kuwa tayari kuisafisha
akili kusudi iweze
kuupokea uhalisia.
Nihitimishe nukta hii ya
pili kwa kusema
kwamba, Wapemba ni walimu na sio
wapotofu wa siasa. Tatu, kusema kwamba
mfumo wa vyama vingi
umewafanya Wapemba
waache shughuli za
kujiletea maendeleo
kama vile kilimo, kwa kujiona wana jukumu la
pekee la kukiingiza
chama chao cha CUF
madarakani ili
kiwabadilishie hali, ni
zaidi ya kuwasemea uongo. Labda tushuke
chini moja kwa moja
kuuangalia uhalisia hata
kwa mifano mepesi na
rahisi. Mimi, kwa mfano, kwa
sasa si mkaazi wa
Pemba, lakini
nimekuwa
nikitembelea nyumbani
mara kwa mara. Ninachokishuhudia
huko ni kuwa, hata
mama yangu mwenye
zaidi ya miaka 60 hivi
sasa, bado anashinda
shamba kwenye mpunga, muhogo na
migomba yake. Na
nikiondoka lazima
anifungie shehena ya
kuchukua. Ninapopanda
meli kurudi hapa Unguja ninapoishi, meli
huwa zimesheheni kila
aina ya mazao ya
chakula yanayolimwa
Pemba, ambayo ama
huwa ni zawadi kama ninayopewa mimi na
mama yangu au ni
biashara inayokwenda
sokoni
Mwanakwerekwe. Kwenye karafuu nako,
licha ya SMZ kuendeleza
ukiritimba wake wa
kuwa mnunuzi pekee
wa zao hilo, hivi
ninavyoandika makala hii vijana wa Kipemba
wamefunga makambi
katika milima ya
Mkoani, Mtambwe na
Pandani wakichuma
karafuu. Kwengineko kote katika Jamhuri hii
ya Muungano,
tunawaona vijana hao
hao wa Kipemba
kwenye pirika zote za
maisha. Abdul-Ghaffar akiwa mmoja wao,
utawakuta wamejaa
Kariakoo (Dar es
Salaam), Darajani
(Unguja), Namanga,
Tunduma, Arusha, bali hata Ulaya, Marekani na
Arabuni. Wako kwenye
kazi za kujiajiri,
kuajiriwa na wengine
wamewaajiri wenzao.
Wako kwenye kazi vyuoni wanasoma na
wanasomesha, wako
viwandani wanaunda
na kuzalisha. Wamo
mashambani wanalima
na kuvuna. Hivi Wapemba wawe
wachapakazi vipi tena
ili mwandishi aridhike
kwamba jamaa zake
hawakukaa kuisubiri
CUF tu iingie madarakani ili iwajazie
mapesa mifukoni
mwao? Nimalizie nukta hii ya
tatu kwa kusema
kwamba kuwa kwao
CUF hakujawahi
kuwafanya Wapemba
kulegea au kulemaa wakisubiri wajazwe
mapesa mifukoni
mwao na Maalim Seif.
Hali ya maisha ya
Pemba ni ngumu, lakini
wenyewe wamekuwa wakifanya kila mbinu
kujinasua nayo. Ni kweli
wana matarajio sana na
CUF, kama walivyo
Watanzania wengine
pia, lakini matarajio hayo ni kupata serikali
ambayo inajenga
mazingira bora ya
wananchi kujiletea
maendeleo bila vikwazo
vilivyopo sasa. Nne, si kweli kwamba
wabunge – wawe wa
chama tawala au wa
upinzani – wana
jukumu na au uwezo la
kuleta maendeleo katika maeneo
wanayotokea. Kwa
kumnukuu Rais Jakaya
Kikwete katika hotuba
yake ya mwisho
Bungeni, ”wabunge hawawezi kutoa
breakfast, dinner na
lunch kwa wapiga kura
wao. Wanachoweza
kufanya ni kuchochea tu
huduma za maendeleo zielekezwe kwenye
majimbo yao.” Labda mwandishi
akipata fursa atueleze
kile ambacho kimeweza
kufanywa na wabunge
wa Upinzani katika
maeneo ambayo Upinzani unaongoza
upande wa pili wa
Muungano, kama vile
Karatu na Kigoma
Kaskazini. Atusaidie pia
namna SMT inavyowachukulia
wapinzani akilingalisha
na SMZ. Mwisho
atubainishie yapi
yaliyofanywa na
wabunge wa CCM hapa Unguja. Hapo tutaweza
kuona namna ambavyo
wabunge wa Upinzani
kutoka Pemba
walivyoshindwa kabisa
kuisaidia Pemba kimaendeleo. Katika
taaluma yetu ya habari
huwa tunasema
kwamba ”asiyetafiti
hana haki ya kuandika”.
Kwa hili, nadhani mwandishi amekiuka
mipaka yake. Nimalizie nukta hii ya
nne kwa kusema
kwamba, ikiwa Pemba
imeshindwa kupata
maendeleo yoyote yale
kwa miaka yote hii 17 ya vyama vingi, si kwa
kuwa Wapemba
wamewapeleka
Bungeni wapinzani, bali
ni kwa kuwa sera za
maendeleo zinazosimamiwa na
serikali za CCM hazijaipa
kipaumbele Pemba. Kwa hakika, kuna
mifano kadhaa ambapo
wabunge kutoka
Pemba wamejitutumua
kuikaba SMT ipeleke
maendeleo Pemba, lakini tukubaliane
kwamba kuna mambo
mawili yanayotanza
hapa: Kwanza, muundo
wetu wa Muungano
unayaweka mambo ya ndani ya Zanzibar kama
elimu, afya, barabara,
maji na umeme kuwa
yasimamiwe na SMZ, na
hivyo mbunge si eneo
lake. Pili, kuna makosa makubwa ya kisiasa
ambayo Wazanzibari
tuliyafanya. Upande
mmoja SMZ ilijisahau
kwamba ni serikali ya
wote. Ikajikita makusudi kwenye
misingi ya kibaguzi
dhidi ya wananchi
wake. Upande
mwengine wapinzani
hawakutaka kuipa SMZ heshima yake ya kuwa
serikali. Wakajizoesha
kuishi bila ya
kuutambua wala
kuuhisi uwepo wa
serikali. Lakini nimalizie kama
nilivyoanza kwa
kusema kwamba, huu
ni wakati ambao
Wazanzibari tumeamua
kuzika tafauti zetu. Tumeamua kubadilika
na kuibadilisha nchi
yetu. Tumeamua
kusema basi tena kwa
yale yote ambayo huko
nyuma yalituumiza na kuumiza mustakabali
wa nchi hii na vizazi
vyetu. Katibu Mkuu wa CUF,
Maalim Seif, ameamua
kunyoosha mkono wa
maridhiano na
utangamano wa kitaifa
kwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Amani Karume.
Maalim Seif
hakusukumwa na
chochote chengine
isipokuwa kwa maslahi
ya Zanzibar. Dkt. Karume naye
ameupokea mkono huo.
Imani yetu ni kwamba,
naye Rais Karume
ameongozwa na
maslahi ya Zanzibar pia. Kwa hivyo, tupeane
nafasi ya kuthibitisha
mapenzi yetu kwa
Zanzibar. Na kwa hilo,
hatuna la kupoteza hata
moja, isipokuwa tuna mengi ya kupata ndani
ya Zanzibar Mpya! And
Yes, We Can!
 
Back
Top Bottom