ADC yavunja Ngome ya CUF Zanzibar, Wanachama zaidi wajitoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ADC yavunja Ngome ya CUF Zanzibar, Wanachama zaidi wajitoa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hasan124, Feb 29, 2012.

 1. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Chama cha Wananchi CUF, leo hii kimepata PIGO kubwa baada ya kile wanachojivunia kuwa NGOME yake kuu kuvunjwa na wanachama zaidi kujitoa katika kile wanachodai "chama kukosa muelekeo wa kisiasa na kukithiri kwa Usultani".

  Wanachama hao wakiongozwa na Viongozi waandamizi wa chama kipya kilichoomba Usajili kwa Mhe. Tendwa cha ADC, Mhe.Saidi Miraji (mwenyekiti wa muda) na Mhe. Lucas Limbu(katibu mkuu) waliopokea kadi zilizorudishwa, wameonyesha kukereka mno na namna viongozi wa CUF taifa wamekuwa wakijiamulia mambo kiholela.

  Baadhi ya matukio yaliyowasukuma kujitoa ni pamoja na uongozi wa cuf kushindwa kujibu hoja zilizotolewa na Mhe. Hamad Rashid za matumizi mabaya ya fedha za chama, badala yake wakapitisha maamuzi ya kumtimua. Pia lugha ya kibaguzi aliyotumia Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Mhe. Ismail Jusa ya ati Ubara na Ukristo ndio chanzo cha Cuf kushindwa uchaguzi jimbo la Uzini na kadhalika.

  Haya yote yametokea Mjini Zanzibar katika Hotel ya Grand Palace maarufu kama Turki, ambapo wanachama zaidi ya 80 walikusanyika na kutoa tamko lao hilo kwa niaba ya wenzao.

  Baadhi ya wanachama waliojitoa leo hii ni pamoja na Viongozi Waandamizi wa CUF kama Kamanda wa Oparation wa Zanzibar (blueguard) Abdullah A. Shamte, Mkurugenzi (w) Kaskazini Mselem, Bi. Khadija Abeid, Mlinzi wa Makamu Mwenyekiti Taifa Mzee Machano na wanachama wengine.

  Hili limekuwa pigo kubwa zaidi kwa CUF kwani Zanzibar ndio sehemu waliowekeza nguvu zao kubwa na kitendo cha kuvunjwa ngome yao hii inaashiria kifo chake hakiko mbali.

  Je, CUF wataweza kurudisha imani yao kwa wanachama wake? Ni suala la kusubiri na kuona.
   
 2. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  R.I.P CUF wadini na wapemba tulikupenda sana lakini kifo kimekupenda zaidi.
   
 3. m

  mubi JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Ukihukumu nawe utahukumiwa.
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Dhambi ya ubaguzi ni sera rasmi ya CUF sera hii imeanza kuwatafuna wenyewe hakuna wa kumlilia.Hongera Jussa nilikuwa sijui CUF ni kwaajili ya wazanzibar na waIslam.
   
 5. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ****!!!!!!!!!!! Same shit, different day!
   
 6. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kabisa, Dhambi ya Ubaguzi ndio inawaponza......Viongozi wa aina ya Jusa hakika hawahitajiki katika taifa hili changa lenye wananchi wengi ambao hawajaelimika vya kutosha. Wanatumia uelewa wao kuwavuruga wananchi wa kawaida kwa manufaa yao binafsi, waonekane wasemaji na walio mstari wambele kutetea haki za wanyonge ilhali hali halisi haiko hivyo.
   
 7. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #7
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yah Yah! Same sh***t. As a matter of fact it disgust....but there is nothing we can do rait now, rait Zion like Lion? They just decide to leave the party and thats it.:ballchain:
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  haya ni mafanikio makubwa sana kwa chama cha mapinduzi...hongera ccm kwa kuisambaratisha cuf
   
 9. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #9
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Vp! Tathmini yako inasemaje, Hao magamba wanaweza wakawageukia na kuisambaratisha CDM?
   
 10. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #10
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwani wewe unafikiri CDM ni changudoa wa kisiasa kama CUF?
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Feb 29, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  CCM wataisikilizia CHADEMA kwenye bomba
   
 12. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #12
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa kweli msafi yeyote hawezi kujoin kisiasa na magamba naamini hii ni moja kati ya kero zilizopelekea cuf kugawanyika, kwani mpinzani wa kweli hawezi kukubali kuitwa ccm B lakini Jamaa wameuchuna tuuuu, yani wako comfortable kweli na Uccm B wao. Ndio maana kina HR, Doyo wakakisanua.
   
 13. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #13
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Jusa na Mtatiro,CUF iliyo imara ndo hii?
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  CUF wamemaliza kazi yao kama walivyomaliza wa kabla yao NCCR, kazi ya chadema bado inahitajika kwa sasa na ikifikia kikomo nayo itakuwa historia. Hiyo ndio system iliyopo.
   
 15. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #15
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila jambo na wakati wake. Kafu kilipitia wakati wa kuitwa chama makini kumbe kikiwa kimebeba agenda kubwa ya siri, ambayo hatimaye wakashindwa kuitunza mioyoni mwao, wakaiweka hadharani,
  watu wamewakataa saas, cheki wanavyojishuku hovyo utafikiri wamejinyea.
  Juzi tu hapa wamejitoa kwenye uchaguzi mdogo wa aurumeru, wakaondokewa na vigogo tukasema 'ni bara'. Sasa ngomeni wamejinyonga hivyo? Maaaaaalim, mzee wa madevu, upoooooooooooooooooooo?
  mwombe radhi HR ulinde kitumbua chako, la si hivyo utakimbiwa na wawakilishi, chaguzi zitarudiwa na hata aslimia 5 hutapata, utaondolewa ikulu kwa aibu.
  Nyoa madevu hayo.
   
 16. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #16
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Zimwi likujualo halikuli........................... Au Ganda la Mua la jana...........................CCM wana akili saanaa.na CUF walisahau maana ua upinzani wakakubali ndoa zaidi.
  Ila laana waliyoitoa wabunge wa CUF kule bungeni dhidi ya Chadema walipotoka nje ya Bunge itawatafuna mpaka dakika ya mwisho.
  Na sasa sijui kama kuna sababu ya kujivunia kuitwa mbunge kwa Chama cha CUF.
  The time is over and next will follow after which is CCM.
  Wasalimieni muendako....
   
 17. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #17
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Watanganyika kwa uchonganishi! Ingekua ndio kipimo cha maendeleo mungekua mbali kuliko Wachina!
   
 18. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #18
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ukitaka kuua nyoka PIGA kichwani.....Aluta continue, bado Pemba sasa na itawadia tu! Just a matter of time.
   
 19. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #19
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hao ni watoto wamelilia wembe wameshapewa wacha tusubiri matokeo yake!
   
 20. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #20
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Johmbaaaa umeshawahi kuona ng'ombe akichinjwa mkiani? Kuwajua Wapemba/Wazanzibari kunataka UACHE KAZI UFANYE KAZI; sio kubwabwaja mitandaoni tuuu!
   
Loading...