Adam Chagulani (Diwani aliyetimuliwa CHADEMA) aanza kufunguka...

Haya yote yapatiwe ufumbuzi kwenye katiba, kama m2 anashindwa kuheshimu matakwa ya chama aachane nacho. Unapokubali kuwa chini ya uongozi lazima ukubali kuwa kuna wakati utatofautiana na wenzako ila ukiona umeshindwa basi jipime. Mimi wasiwasi wangu mkubwa ni vijana wanaoingia kwenye siasa bila kuandaliwa kimaadili kwa maana ya uongozi na namna ya kuzikabili challenge za leadership.
 
....

Kwa kukusaidia tu... huenda ni kweli humfahamu vizuri kijana huyu Chagulani ila kwa ujumla alikuwa ni pasua kichwa ndani ya CDM Mwanza na CCM (Hususan wanachama wake matajiri waliopo Mwanza wakishirikiana na Mbonea Wilson Kabwe) walifikiri kwamba kwa kupitia kwa Matata na huyo Kijana Chagulani wangeweza kuipasua CDM Mkoani mwanza lakini maskini wa mungu usaliti wao kwa chama umeishia kupasuliwa wao.

Kumbuka kabla hata ya ule uchaguzi wa awali wa meya Manyerere kulikuwa na Information leakeage kwamba kuna madiwani wawili wa CDM wamepanga kusaliti na kumpigia kura mgombea umeya kupitia CCM..Madiwani wale wawili ndio hao ambao leo wanaonyesha true colours zao.
Na kama unakumbuka vizuri Zitto Kabwe ndio alipewa jukumu la kusimamia mchakato ule wa uchaguzi kwa upande CDM na alifanikiwa kirahisi kuwashawishi madiwani hawa ambao walikuwa wameshanunuliwa.

Ni uamuzi mzuri sana wa kamati kuu ingwa umekuja kwa kuchelewa.
 

Eti huyu nae great thinker.
Kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi!!
 

Wewe itakuwa una matatizo ya Akili Nenda jamii doctor kwa msaada zaidi
 
Eti huyu nae great thinker.
Kwi kwi kwi kwi kwi kwi kwi!!

Mbona unajichekesha chekesha kama mwenyekiti wako, au si-riziki??? Okay, mtabadili sana IDs, mara 'mchuzi wa kuku' mara 'zombe'... Lakini mwisho wa siku lazima tuwachomeke vijiti... Afterall, nimesahau, kamjulishe Nape kuwa ule mpango wake/wenu wa kuwatoa wachangiaji nje ya mada hasa kunapokuwa na mada moto au 'critical' tumeustukia, mwambie akajipange upya...
 
Hata yule diwani rasta wa arusha alifunguka na kutoa machozi mithili ya mshiriki aliyeenguliwa kwenye mashindano ya bongo star search ila mwishoni akakaa kimya.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 


Ukweli ni kuwa,ujumbe uliotumwa na CDM taifa haukutaka kuutafuta UKWELI. Ila nafasi bado ipo, tafuteni UKWELI kwani sikuzote ukweli unatabia ya kujidhihilisha hata usipotafutwa. Kwahili la CDM, Mwanza, Mh sana DR SLAA, Kiukweli umeteleza
 
Eti anaomba mungu wasipate nafasi nyeti yaani dr.Slaa.... Jamaa Inaonyesha jinsi gani alivyo mbinafsi na mpenda madaraka.hajui kama chadema ni taasisi.!
 
Kamati kuu ndiyo nini wenye maamuzi ni Mbowe na Dokta Slaa, pamoja na Lema, siyo mbunge lakini yumo kwenye kamati. Hawa ndiyo wenye chama.

nani aliyekwambia kamati kuu ni ya wabunge tu? Ulimuona yule mhindi kwenye picha? Ni mbunge wa wapi? Watanzania tunapenda sana kukosoa vitu tusivyovijua! Acha uvivu,tafuta muda usome katiba ya cdm na uisome na kuelewa.
 
Wameamua kudili na madiwani, ila jeshi la mtu moja tu Shibuda wamemshindwa...
 
Kaka subiri matokeo ya uchaguzi 2015 kama tutakuwa wazima tutaona saizi mapema sana kusema matokeo ya kufukuza madiwani.
Ni bora mara mia chama kikabaki na madiwani pia wabunge wachache wenye kujua wajibu wao kuliko kuwa na madiwani wengi wa aina ya Chagulani wanaodhani bila wao Chama hakipo. Ulimwengu wa hujuma na fitina tuwaachie CCM kwani wao ndio mabingwa kwa uovu.
 

haaah haaah umeua!
 
Ivi mtu anapokiri kosa na kujutia na kuomba kurudi kundini inakuwaje? Au ndo bas tena.....kama fursa hii ipo basi asamehewe wakuu. Inaonesha dogo ni jembe.
Dogo ni Jembe tena Sana tu. Watu ambao wamefanikiwa Kuona kash kash zake kwenye vikao vya halmashauri na Jinsi alivyo Makini huwezi thubutu kukubaliana na hii taarifa ya kumwagwa.
Mbaya ni Kuona watu wanamshitumu tu Adam kwa kosa la kubumbiwa na lenye fitna ndani yake.
Alafu
 

Melody hii sasa ina pitch kuliko kawaida Chagulani kama ni msomi wa chuo kikuu angejua kwamba matatizo haya suluhishwi kwa kudivide na kuwaona baadhi ya members wa kamati kuu kwamba ndio wamekusaliti na wengine wamekuonea ,anataka kutuaminisha kwamba swala la kumuengua diwani linaweza kuwa la mtu mmoja bila Mwenyekiti,Naibu Katibu Mkuu,Mshauri wa chama ambao nao ni wajumbe wa Kamati ,hii inadhihirisha kwamba huyu yuko kwenye mission ya kumchafua adui wa CCM no 1 Dr Slaa,
Nadhani amue tuu kujiunga na chama kingine akipendacho
 
Ivi mtu anapokiri kosa na kujutia na kuomba kurudi kundini inakuwaje? Au ndo bas tena.....kama fursa hii ipo basi asamehewe wakuu. Inaonesha dogo ni jembe.
Dogo ni Jembe tena Sana tu. Watu ambao wamefanikiwa Kuona kash kash zake kwenye vikao vya halmashauri na Jinsi alivyo Makini huwezi thubutu kukubaliana na hii taarifa ya kumwagwa.
Mbaya ni Kuona watu wanamshitumu tu Adam kwa kosa la kubumbiwa na lenye fitna ndani yake.
Alafu watu wanakubaliana na info kutoka juu hata Kama hazina tija wala haki kwa ADam
Lazima watu wawe wanapima Kama vitu ni sawa sio kila linalotolewa na uongozi wa chadema ni sawa na watu wana buy them na kufanyia kazi. Hatuwezi kwenda popote. Kabla ya kamati kuu ilitakiwa lipitie ya wilaya kisha mkoa. Sasa hii shuttuma direct to kamati kuu na hapo hapo maamuzi kutolewa uanachama. Hakuna first warning last warning wala nini?watu wa chadema ni perfect tupu Hakuna makosa! Duuu
 
Imekuwaje Kamwagwa basi nadhani alidhani kuwa jembe bila nidhamu za kiutendaji ingemsaidia hawajifunzi yaliyowapata akina Kafulila leo wameondolewa platform ya KIsiasa magazeti TV na radio zilizompamba kumwalika kwenye mijadala mbalimbali wamembwaga hayuko tena kurasa za mbele za magazeti

Chagulani kama unapenda chama chako na unaona umeonewa fuata taratibu za kukata rufaa hutasaidiwa na maandiko ya mitandaoni historia imeonyesha njia hii hata madiwani wa Arusha waliifanya sana na hawakuweza kushinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…