Haya ndiyo niliyojifunza katika utawala wa Awamu ya Tano, vijana igeni

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,368
Awali ya yote, naomba niweke wazi kabisa yakuwa mimi ni mwanasiasa kijana na nilijiunga na Chama cha Demokrasia na Maemdeleo Mwaka 2009, nikiwa Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar.

Nakumbuka kadi yangu ya kujiunga ilisainiwa na Marehemu Regia Mtema na aliyenikabidhi ni John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema kwa sasa.

Sikuwa peke yangu. Nilikuwa na Peter Lijualikali, Mbunge kwa sasa Ifakara; Keneth Goliama, mkulima na mjasiriamali na mkurugenzi wa kampuni; Chacha Amosy Nyaigoti, sasa ni Askari Polisi. Kwakweli tulikuwa wengi.

Baada ya kujiunga kama wanachama tulilazimika kufungua Tawi la Chadema Chuo Kikuu cha Tumaini na tulifanikiwa kufanya hivyo. Mlezi wa hilo tawi nakumbuka alikuwa Mh. Halima Mdee, ni kupitia ulezi wake aliwahi kujitolea kutusafirisha viongozi na wanachama kwenda mkoani Dodoma Bungeni kujifunza masuala ya Bunge, na ilikuwa mara ya yangu ya kwanza kuiingia Bungeni. Hakuishia hapo, nakumbuka alitupa ofa ya kuingia Club 84 Dodoma enzi hizo.

Humo nilishuhudia mauno ya wabunge balaaa na kula sana gambe.

Sijui kama tawi hilo bado vijana wasomi wa TUDARCo wanaliendeleza au lilikufa.

Niseme ukweli, baada ya kujiunga na Chadema sijawahi kufikiria kukihama chama hicho hata siku moja na sitowaza, ingawa marafiki zangu baadhi wameanza kufikikiria kukihama.

Nimeeleza historia yangu ili nitakapoingia kwenye agenda yangu nisje ishia kuitwa kada wa Chama cha Mapinduzi. Niseme ukweli sijawahi na sitowahi kukipenda chama hicho na aliyenifanya nikichukie ni Wakuu wa mikoa Dar es Salaam na Iringa, kwa sasa Ally Hapi na Paul Makonda. Ipo siku nitaeleza walichofanya na wenzao enzi hizo tukiwa Ukumbi wa Karimjee, wakati wa mjadala wa Katiba mpya enzi hizo.

Kutokana na hilo huwa sipendi niitwe mwanaCCM na huwa siwapedi hata hao waitwao hivyo (mnisamehe maana humu mpo wengi)

Zaidi ya yote wizi wa Mali za umma unaofanyika Tanzania, kati ya majizi kumi, name unayakuta na kadi za uanachama wa CCM. Kama munabisha, subirini muone, Kangi na wenzie 15 hakuna hata upinzani mmoja mule.

Niende kwenye hoja.

Utawala wa Awamu ya Tano, umenifunza mengi na ninaushukuru sanaaaa!

Kwanza, kuhusu kujiajiri

Hili nimelitelekeza kwa vitendo. Utawala wa Kikwete mimi nilikuwa mwajiriwa wa benki fulani ambayo nilifkia mpaka ngazi ya meneja, hakuna nilichonufaika nacho zaidi ya kukopeshwa gari. Kutokana na historia ya maisha yangu nilijikuta natumikia benki kwa akili zangu nyingi na muda wangu wote, nilipoteza vitu vingi sana.

Katika utawala huu nilimua kujiajiri na nimeweza na mafanikio nayaona sana, yani kujiajiri ndiyo kila kitu.

Pili, ni kuajiri wengine

Hii ni sehmu ya mafanikio ninayojivunia, ila hapa changamoto ni kubwa yani vijana wa Kitanzania hawaaajiriki, yaani ni mizigo, wapo nilioajiri wakaishia kuniibia, na mengine mengi.

Kama unaitaji kuajiri ni bora uajiri Mkenya na Mganda ila vijana wa Kibongo ni mizigo kama gunia la kinyesi, yaani hawajitumi, majungu mengi, wanatambia vi-degree vyao. Ukiwapa kazi, impact inakuwa hovyo kabisa.

Tatu, ni nidhamu ya pesa

Utawala huu hakika umenifunza kuwa na heshima ya pesa ninayoipata. Asente sana!

Nne, kujituma kufanya kazi

Hili nalo hakika umenifunza utawala huu, asante sana!

Tano, hakuna malipo bila kufanya kazi

Ndugu zangu, kutokana na majukumu niliyonayo au huduma ninazozitoa, mimi natoa huduma malipo ni baadaye. Yani utawala huu umenifunza kuwa pasipo kufanya kazi hakuna kula, hakika kwa hili mimi nalismamia vyema. Asanteni sana!

Je, wataka kujua nilijiajri vipi?

Ni kuwa, nikiwa benki nilismamishwa kazi. Baada ya hapo ndiyo kilikuwa kipindi cha uchaguzi; mimi nilichukuwa ilani ya vyama vyote vya siasa nikazisoma vizuri sana, nikaangalia fursa zilizomo humo.

Nikajiandaaa kwa chama chochote ambacho kingeshinda na kuunda serikali, mimi ningepeleka ombi kwa serikali si kuniajiri bali ni kuomba kufanya nayo kazi kama mtu binafsi na serikali kupitia kakampuni kangu.

Huwezi amini baada ya uchaguzi CCM ilishinda. Mimi kupitia ilani yao niliona fursa ya jambo fulani nikaenda ofisini kwa waziri husika akapokea ombi langu tukafanya makubaliano akanipa kibali cha kufanya kazi hiyo, kwa maana cha kunitambulisha kuwa ananifahamu na kampuni yangu inazo sifa za kufanya kazi hizo. Basi sasa hivi mimi napiga kazi na mafanikio ni makubwa sana kuliko kuajiriwa.

Nawaasa vijana mliopo mitaani, igeni. Nisingependa niseme mafanikio niliyopata ila kwa kifupi utawala huu umeniwezesha hata kujenga nyumba mbili jijini Dar es Salaam, ila wa Jakaya ulinifunza hata sana hapo New Africa kula Ijumaa. Nadhani mumenielewa.

Sasa vijana nawambieni kuna fursa nyingi kwenye ilani za vyama vya siasa. Someni na mmuungane mpeleke business idea. Utawala huu unataka solution, onesha changamoto na tafuta jinsi ambavyo unaweza itatua utafanikiwa sana.

KARIBUNI SANA

Tukutane uchaguzi ujao. Mimi nshajipanga, njoo tuongeze nguvu fursa ni nyingi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi nimeguswa na hilo la wabongo wengi kutoajirika. Uko sahihi sana. Watu badala ya kuwaza kuzalisha thamani, wanawaza kupiga pesa kimagumashi mwishowe badala ya kuwa faida wanakuwa changamoto. Yaani ukiajiri unajikuta unatakiwa kutumia akili ya ziada kufikiri utafanya nini mwajiriwa asikuibie na kukufilisi badala ya kuwaza utaendelezaje biashara.

Kuna watu wengi tu wana mitaji ila wanaogopa kuwekeza na kuajiri wapongo kwa kuhofia hayo.Na kuna wengine wanaweza kukuibia hata katika level ya interview kama wakipata fursa ya kufanya hivyo, sasa hebu vuta picha hapo. Ni bora tukajitathmini.
 
Suala la kujiajiri nalo ni la kuishukru serekali badala ya kumshukuru Mungu ambaye amekupa akili na nguvu za kufanya kazi, mtaji umetafuta wewe mwenyewe kwa msaada wa Mungu, kazi unafanya wewe mwenyewe kwa msaada wa Mungu,kwa waziri umeenda wewe kwa miguu yako mwenyewe kwa msaada wa Mungu,badala ya kumshukuru Mungu unaishukuru serekali ambayo hata ukifirisika haikujui zaidi ya Mungu, na viongozi wote waliopo serekali hawataki watoto wao wakajiajiri wanapeana ulaji wao kwa wao, wanaoambiwa wakajiajiri ni watoto wa masikini baada ya serekali kushindwa majukumu yake ya kuajiri.
 
Ni kweli, waajiriwa wa kibongo wengi (sio wote ) ni mizigo, niliwahi kufanya kazi sehemu fulani na wahindi hapo ndipo nilipogundua sisi wabongo ni wavivu na miyeyusho, wale jamaa wanapiga kazi kama mashine, tena wana nidhamu na uaminifu uliotukuka. lunch break ni dakika 20 tu na kila mtu anakuja na hotpot ya chakula toka kwake, story ni baada ya kazi.
 
akili zako ni mbovu na ni mbovu kuliko mbovu
Suala la kujiajiri nalo ni la kuishukru serekali badala ya kumshukuru Mungu ambaye amekupa akili na nguvu za kufanya kazi, mtaji umetafuta wewe mwenyewe kwa msaada wa Mungu, kazi unafanya wewe mwenyewe kwa msaada wa Mungu,kwa waziri umeenda wewe kwa miguu yako mwenyewe kwa msaada wa Mungu,badala ya kumshukuru Mungu unaishukuru serekali ambayo hata ukifirisika haikujui zaidi ya Mungu, na viongozi wote waliopo serekali hawataki watoto wao wakajiajiri wanapeana ulaji wao kwa wao, wanaoambiwa wakajiajiri ni watoto wa masikini baada ya serekali kushindwa majukumu yake ya kuajiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom