Adam Chagulani (Diwani aliyetimuliwa CHADEMA) aanza kufunguka...

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
  • Chagulani Adams

    Chagulani Adams
    Nipenda kutumia fursa hii kuwataarifu wapenzi wa mageuzi na wakweli wote kuwa sina mpango wa kujiunga na Chama cha Mapinduzi kama maadui zangu wa kisiasa wanavyozusha kwenye mitandao ya kijamii kuwa nina mpango wa kujiunga na CCM ,

    niseme hivi sijawahi kuwa mwanaccm na kamwe sitakuwa mwanaccm mimi bado ni mwanachadema kindakindaki najipanga jinsi ya kuitafuta haki yangu nawaheshimu sana viongozi wangu wa chama hasa mwenyekiti F.Mbowe,Zitto kabwe Dr.Kitila ,na wote wanaopenda ukweli na siyo wafanyia kazi majungu HUKU WAKITAKA NAFASI NYETI NCHINI nimuomba MUNGU KUANZIA SASA WASIPATE NAFASI HIZO MAANA kama wanayafanya haya hawajawa na uhakiki wa amri kwa vyombo vya ulinzi vipi?

    wakijua wanausalama wanawalinda sipati picha MUNGU aepushe bali na balaa hilo,niseme binafsi nimesikitishwa na kuhusihwa na majungu kuwa nimeshiriki vitendo vya kifisadi na kukihujumu chama changu nilichokipigania siki zote tangu nikiwa chuoni hadi sasa nitaandika waraka mwingine kueleza kilichojiri na nini hatua inayofuta baadae tuko pamoja ukombozi wa taifa hili ni lazima kwa njia yeyote ile
 
Ujana maji ya moto unapaswa kuuoga kwa tahadhari sana.Adam ajiangalie
 
Ninaamini kwamba kama kweli anakipenda chama chake CDM, asingeleta malalamiko yake humu ndani ya JF, ambamo hayawezi kupatiwa ufumbuzi zaidi ya kujadiliwa tu.

Ashakum si matusi, lakini hii ni sawa na mtu aliyemfumania mwenzi wake, badala ya kuyamaliza kimya kimya kama bado anampenda, anaamua kuita watu waje washuhudie kisha wanaondoka wote na mwenzi wake kurudi nyumbani kulala eti wamepatana!!?? Ni aibu.
 
Unafiki tu ndio unaosumbua. Kamati Kuu ni chombo makini. CDM inafanya kile ambacho kamati kuu zingine wanashindwa na kubakia 'wajipime'.... Uongozi unahitaji 'NIDHAMU' na 'UTII', kinapokosekana kimojawapo huyo mtu hafai...
 
Hivi hili litoto bado tu linataka kupimana uzito na Rasi wetu Dr.slaa? Hebu lijipime kwanza na unafiki wake na linazani eti lenyewe ni pekee ndani ya chama na wakati wapo wengi tu yani sasa hivi hakuna kubembeleza kwani ukileta ujuha CHADEMA inakupoteza tu.......kwani nilikuwa nalikubali sana that time kwenye siasa za Daruso mpaka nilikuwa naliamini kipindi kile litakuja kuwa sio linafiki lakini leo limeshavuta za magamba.
 
Tuache kuropoka,maamuzi ni ya Kamati Kuu si ya Mbowe wala Slaa. Binafsi namfahamu Adam ila niyajuayo kumhusu si mahali pake kuyasema.Ajiulize na kujisahihisha pale alipopotoka

Ajisahihishe wapi kakosea wapi? Yaani kumkosea Meya wa Jiji la Mwanza ni makosa, mbona Mwanza nzima wanajua Chagulani, kafukuzwa udiwani kwa msimamo wake wa kupinga ufisadi ndani ya halmashauri ya Jiji la Mwanza.
 
Unafiki tu ndio unaosumbua. Kamati Kuu ni chombo makini. CDM inafanya kile ambacho kamati kuu zingine wanashindwa na kubakia 'wajipime'.... Uongozi unahitaji 'NIDHAMU' na 'UTII', kinapokosekana kimojawapo huyo mtu hafai...
Kwa hiyo maana nyingine ya umakini huo ni mwana CDM kutetea madhambi ya kiongozi wa CDM kwa gharama yoyote ile?

Mbona naona kma hatua ya Kamati Kuu ya CDM ni hasira kwa DIWANI wake kushiriki kumg'oa Meya asiyekubalika ,na ni fisadi.

CDM ikiacha kutetea uadilifu basi itakuwa haina tofauti na vyama vingine vyenye nia tu ya kutaka uongozi, hata kwa misingi isiyo faa.
 
Unafiki tu ndio unaosumbua. Kamati Kuu ni chombo makini. CDM inafanya kile ambacho kamati kuu zingine wanashindwa na kubakia 'wajipime'.... Uongozi unahitaji 'NIDHAMU' na 'UTII', kinapokosekana kimojawapo huyo mtu hafai...

Kamati kuu ndiyo nini wenye maamuzi ni Mbowe na Dokta Slaa, pamoja na Lema, siyo mbunge lakini yumo kwenye kamati. Hawa ndiyo wenye chama.
 
Huyu dogo ana matatizo! ni mpu.uzi tu.sina cha kuongeza zaidi ya hicho.
 
Chagulani mi nakujua sana ache kujidhalilisha usiombe radii, maana slaa ameapa lazima wakumalizie chini ili wenje spite bila kupingwa 2015' nenda cuf au ccm au ccm . Tukupe ubunge. Achana na chadema Chama cha wachaga na wamburu. Ungekuwa MCHAga usinge fukuzwa. Nakufahamu ulivyokuwa mwancdm mtiifu lakini Ndio hivyo tena basi tena, kawasalimu, chezea Chaga na mbulu wewe .
 
Ivi mtu anapokiri kosa na kujutia na kuomba kurudi kundini inakuwaje? Au ndo bas tena.....kama fursa hii ipo basi asamehewe wakuu. Inaonesha dogo ni jembe.
 
Chagulani mi nakujua sana ache kujidhalilisha usiombe radii, maana slaa ameapa lazima wakumalizie chini ili wenje spite bila kupingwa 2015' nenda cuf au ccm au ccm . Tukupe ubunge. Achana na chadema Chama cha wachaga na wamburu. Ungekuwa MCHAga usinge fukuzwa. Nakufahamu ulivyokuwa mwancdm mtiifu lakini Ndio hivyo tena basi tena, kawasalimu, chezea Chaga na mbulu wewe .

feki wewe unapombe ya ukabira mpaka leo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom