Adadi Rajabu naye yumo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adadi Rajabu naye yumo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ochu, Sep 24, 2008.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Adadi Rajabu, jana alitajwa kuhusishwa na vifo vya wafanyabiashara watatu na dereva teksi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe na wenzake 12.

  Adadi ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, alihusishwa katika vifo hivyo kutokana na maelezo ya mshitakiwa wa 11 katika kesi hiyo, Rashid Lema, yaliyotolewa mbele ya mlinzi wa amani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Omari Abdalah mwaka 2006.

  Akitoa ushahidi wake jana katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Omari ambaye kwa sasa ni Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni, alidai Adadi, alitaarifiwa mapema na Zombe na kwamba alitoa amri ya kuchinjwa kwa wafanyabiashara hao ambao ilidaiwa walikuwa majambazi waliopora fedha kwenye gari la Kampuni ya BIDCO, Barabara ya Sam Nujoma.

  Shahidi huyo alidai mbele ya Jaji Kiongozi Salum Masati kuwa Lema, katika maelezo yake alikiri kushiriki katika tukio la mauaji hayo, lakini alidai hakushiriki kuua.

  Huku akiongozwa na Wakili wa Serikali, Alexander Mzikila, shahidi huyo wa 33, alidai Lema katika maelezo hayo alimwambia wakiwa eneo la Sinza Barabara ya Sam Nujoma wakiwa na wafanyabiashara hao alimsikia Bageni, (mtuhumiwa wa pili ) akiwa anazungumza na simu ya upepo ‘radio call’.

  Alidai wakati Bageni, akiwa anazungumza na simu ya upepo, yeye alikwenda kwa watuhumiwa hao waliokuwa ndani ya gari na kuwauliza kuwa wana matatizo gani.

  Mmoja kati ya wafanyabiashara hao ambao kwa sasa ni marehemu alimjibu kuwa hawakujua walikuwa wamekamatwa kwa kosa gani na kwamba ni mfanyabiashara wa madini.

  Alieleza shahidi huyo baada ya Bageni, kurejea kutoka sehemu aliyokuwa akizungumza na simu aliwauliza askari wenzake kuwa wanawaonaje watuhumiwa hao, askari mmoja alimjibu kuwa hao si wahusika wa tukio hilo la uporaji.

  Baada ya Bageni kupata jibu hilo aliwasiliana tena na simu na baada ya kurejea aliwaambia askari wenzake kuwa ameambiwa na Mkuu wake, Afande Zombe kuwa watuhumiwa hao ni lazima wachinjwe.

  Shahidi huyo alidai Bageni alimsihi Zombe kuwa hao si wahusika na wasidhuriwe kwa lolote, lakini ikashindikana na kuendelea kusisitiza amri yake kuwa lazima wachinjwe.

  “Nimejaribu kadiri ya uwezo wangu kumshawishi Zombe kuwa watuhumiwa hao si wahusika, lakini ikashindikana na hivyo akatoa amri kuwa ni lazima wachinjwe,” shahidi huyo alisema sehemu ya maneno ya Bageni yaliyoelezwa na Lema kwake.

  Kutokana na maelezo hayo, watu waliokuwa mahakamani hapo walionekana kuwa wenye simanzi huku zikisikika sauti za manung’uniko.

  Katika maelezo hayo, Lema alikana maelezo yake yaliyokuwa yametolewa katika tume iliyokuwa imeundwa na Rais Jakaya Kikwete, Tume ya Jaji Kipenka ya kuchunguza mauaji hayo kwa madai kuwa Zombe alikuwa amemlazimisha kuandika maelezo hayo.

  Shahidi huyo alidai Lema, hakuridhika kuandika maelezo aliyokuwa ameelekezwa na Zombe na kuwauliza wenzake kuwa anahofu kuhusu kuandika kitu asichokijua na kuhoji itakuwaje kukitokea matatizo.

  Alidai baada ya kuuliza swali hilo aliambiwa na Zombe kuwa wamejipanga vilivyo kupangua hoja mbalimbali na asiwe na wasiwasi.

  Baada ya kukamilisha kutoa ushahidi wake, aliiomba mahakama hiyo kuyapokea kama kielelezo katika kesi hiyo.

  Hata hivyo, mawakili wa utetezi ukiongozwa na Majura Magafu, alipinga kutolewa kwa ushahidi huo kwa madai kuwa lilikuwa si ungamo, bali alikuwa anajitetea yeye mwenyewe na kujitoa katika kesi hiyo.

  Magafu, alidai Lema alitakiwa kukiri kuhusika kwake katika kesi hiyo na si kama alivyofanya katika vifungu vya Sheria ya Ungamo na kusema vitu kama hivyo havipo.

  Alidai mlinzi wa amani alitakiwa kumpa onyo mtuhumiwa huyo kabla ya kuanza kutoa maelezo yake, ili aweze kufuata taratibu za kutoa ungamo hilo na si kujitoa kama alivyofanya hapo awali.

  Hata hivyo, Jaji Masati katika uamuzi wake uliochukua takriban saa moja, alisema sheria ina uwanja mpana na hicho kilichotumiwa kupinga ni sehemu ndogo ilikuwa haijajitosheleza katika kukataliwa kielelezo hicho.

  Mahakama ilikubali maelezo ya Lema yaliyotolewa kwa mlinzi wa amani na kuyapokea kama kielelezo.

  Sehemu ya mahojiano kati ya wakili Msemwa na shahidi yalikuwa kama ifuatavyo:

  Msemwa: Uliamini maneno ya mtuhumiwa kuwa Zombe ndiye aliyetoa amri ya watuhumiwa hao kuchinjwa?

  Shahidi: Si kazi yangu kuamini au kutoamini. Kazi yangu ilikuwa ni kuandika kile alichokuwa akikisema mtuhumiwa.

  Msemwa: Uliwahi kumuuliza kuwa wenzake 14 waliwahi kusikia amri hiyo ya Zombe?

  Shahidi: Sikumuuliza na wala sikuona sababu ya kumuuliza.

  Msemwa: Uliwahi kumuuliza kama kabla ya kuja kwako kuna sehemu aliwahi kutoa maelezo?

  Shahidi: Katika maelezo yake inaonekana alishawahi kutoa maelezo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Tume ya Jaji Kipenka.

  Wakili Ishengoma: Kuna maswali ulimuuliza, lakini hukuyaandika katika maelezo haya, nani alikupa amri ya kuyaacha?

  Shahidi: Maelezo yapi, yale aliyoniambia ndiyo niliyoyaandika.

  Ishengoma: Ulimhoji mtuhumiwa kwa muda gani, mbona maelezo ni kidogo?

  Shahidi: Saa moja, inategemeana na kasi ya kuandika ya mchukua maelezo.

  Ishengoma: Kwa hiyo yale uliyoyasema kuna mengine umeyaacha?

  Shahidi: Yapi unataka niseme au ningeandika unayotaka wewe? Ulikuwapo kwenye eneo la tukio?

  Wakili Magafu: Katika maelezo yake mtuhumiwa alisema kuwa karatisi aliyopewa na Zombe hakuirudisha, alikuonyesha?

  Shahidi: Hakunionyesha na wala hakuja nayo ofisini kwangu.

  Magafu: Alikueleza karatasi hiyo ilikuwa na mambo gani?

  Shahidi: Hakunieleza na wala sikuwa na haja ya kumuuliza.

  Magafu: Baada ya kuchukua maelezo ya mtuhumiwa ulimpa nani?

  Shahidi: Niliwapa maofisa waliokuja naye mtuhumiwa huyo na mmoja kati ya maofisa hao jina nalijua, jina lake moja. Mmari.

  Aidha, shahidi wa 32 katika kesi hiyo, Mrakibu wa Polisi (SSP) Elly Nkya alionekana kuwa mbogo kutokana na wakili wa utetezi, Jerome Msemwa kumuuliza kama alikuwa na uhusiano wowote kabla ya Zombe kuwa mtuhumiwa.

  Elly alikubali kuwa na uhusiano wa kijirani na Zombe na si zaidi ya hapo, huku akiwa anaonekana kuwa mbogo kwa kumwambia wakili huyo aulize maswali ya msingi.

  Sehemu ya mahojiano kati ya wakili Msemwa na shahidi huyo yalikuwa kama ifuatavyo:

  Msemwa: Shahidi una uhusiano gani kati yako na Zombe kabla ya kuwa mtuhumiwa wakati alikuwa anakupa lifti katika gari yake?

  Shahidi: Sina uhusiano wowote, nilikuwa nafanya naye kazi na nilikuwa napanda gari lake kwa kunisaidia kuwahi kazini.

  Wakili: Umeolewa, una watoto wangapi?

  Shahidi: Nimeolewa na nina watoto wanne.

  Wakili: Je, una uhusiano gani mwingine na Zombe?

  Shahidi: Usitake kunigombanisha na mume wangu, mimi nimeolewa na nina familia yangu na Zombe ameoa na ana familia yake. Usitake kutugombanisha.

  Msemwa: Na kwa nini uliandika kwenye CD Zombe M.A wakati Zombe kwa wakati huo hakuwa mtuhumiwa?

  Shahidi: Sikuwa na maana mbaya mimi nina uzoefu wa kazi zangu kwa miaka 20 sasa, siwezi nikamuandika hivyo kwa kumfikiria vibaya, niliandika hivyo kutokana kazi hiyo ilihusisha ofisi ya Zombe.
   
 2. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  damu hii isiyokuwa na hatia iliyomwagika itawarudia kwenu wote na vizazi vyenu. haki inaweza isitendeke hapa duniani lakini mbinguni itatendeka tu
   
 3. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,786
  Likes Received: 1,963
  Trophy Points: 280
  Bado tunangoja kutajwa MAHITA kwani nasikia alikuwa mlezi wa majambazi ndio maana baada ya tukio hilo alimuhamisha kitua cha kazi Zombe ili kumwokoa
   
 4. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Askari wetu wanatakiwa wajifunze kuto kuwa waoga. Hadi wanaandika maelezo huku wakijua ni ya uongo, je kama si Mh Rais kuunda tume tungejua waliandika maelezo ya kuelekezwa na Zombe? Kuna haja ya kuwachukulia hatua kwa kosa hilo.
   
 5. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  inasikitisha kujua kwamba raisi na tume yake walidanganywa
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ama kweli penye ukweli .Hapa kuna kazi kubwa .Hivi Adadi anaweza kuitwa mahakamani kujibu haya ?
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ..........hii ni mbaya sana...........watu wanaadhibiwa kwa sababu za kibinafsi za viongozi wa sehemu mbali mbali za serikali ili kutimiza UOVU wao...........cha ajabu hata vijana waliofundishwa maadili nao wamekuwa mafundi kuongopa........ili kusaidia viongozi walio na roho za kishetani.............hivi angalia sasa..........watu "claimed innocent" wamekufa...............

  .......adhabu zenu hata kama si hapa duniani.........mujue kuwa Mola "sio wa Athumani pekee"............
   
 8. M

  Masatu JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hii habari ina mapungufu, "kutajwa" kwa Adadi kuna nasibishwa kwa namna moja au nyingine na kushiriki. Lakini ukisoma kwa makini utaona kutajwa huku ni routine procedure ilitumika kumpa habari ya tukio DCI.

  Mwandishi kwa sababu anazozijua mwenyewe anataka msomaji a conclude kuwa Zombe ame collide na Adadi!
   
 9. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ...Ndio mbinu za kuuza magazeti hizo.
   
Loading...