Acting Presidaa

Acting Presidaa

Majoja

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
612
Reaction score
189
Ku-act ni kuigiza.
Leo hii tuna waigizaji wengi sana nchini, na mabo machache yanafanyika kiukweli.
Tuanze na Mkuu wetu wa Nchi-Presidaa
Acting Presidaa daima yuko safarini, ana act kuwa presidaa, na huko Mjengoni Magogoni sijui nani ana Act nafasi yake daima anapokuwa hayupo.
Siku ana zokaa ofisini na kufikiria mambo magumu zinahesabika-Acting Presidaa.

Acting PM, Mtoto wa Mkulima,daima ana act kufuatilia hili na lile.La Kilimo Kwanza ndo haswaa!Ana act wakulima watawezeshwa na power tiller, mwisho wanaofaidika ni suppliers wa power tiller-wahindi to be exact.Machinga ndo wamekuwaa ni jeshi la vijana wasio na kazi.Acting Pm hapa.

Waziri Nishati Ngeleja ndo usiseme.Acting kwa kwenda mbele.Umeme utakuwa historia imekuwa act ya kila wiki.Toka mwaka 2006 hii act inaendelea, mwisho wake hauonekani.

Wizara ya Sheria, hapa ndo kuna bonge la act.EPA,KAGODA,RICHMOND na hata RADA havikuwahi kuwepo, hii act kali.Waingereza wamesema mmeibiwa, sisi tuanadai hatujui nani katuibia lakini turudishie kilichoibiwa.ACT hapa hatujui kilichoibiwa kilitokatokaje.
Bonge la act.
Bungeni ndo usiseme.Kuna act za kulala,act za kutoa nakurudisha shilingi, halimradi burudani tupu.

Wananchi nao haturudi nyuma, du tuna act.Kuvaa masuti ndani ya mashangingi na kuelekea makazini toka saa 11 asubuhi na kufika kazini saa 3.Bonge la act, utafikiri tuko bize.Posho kede kede

Mswahili wa mtaani na mlala hoi yeye hana act.Jua na vumbi siyo act.Ile njaa ya mchana toka kwa mkulima hadi mmachinga si act.
Akiugua hapo maisha ni ya wasi wasi si act hilo-anaweza kufa na uchungu hapo hauna act.

Du! hili act kiboko
 
wana jf nao wana act eti wanataka mapinduzi, wakati ni waoga sana. Watu wa Dar nao wana act eti wanavision wakati nao ni wanafiki na waoga sana! Duh! Kila sehemu kuact sana, na wewe pia una act eti una uchungu na nchi! Duh! Full miaction.
 
wana jf nao wana act eti wanataka mapinduzi, wakati ni waoga sana. Watu wa Dar nao wana act eti wanavision wakati nao ni wanafiki na waoga sana! Duh! Kila sehemu kuact sana, na wewe pia una act eti una uchungu na nchi! Duh! Full miaction.
Tuna act kulipa kodi
Tuna act suala la maadili
Tuna act kuwa tuna uelewa wa kinachoendelea nchini
Tuna act suala la kuvua magamba, kumbe gamba bado lipo
Tuna act, tuna act, .. tuna act.........
 
Tuna act kulipa kodiTuna act suala la maadili Tuna act kuwa tuna uelewa wa kinachoendelea nchiniTuna act suala la kuvua magamba, kumbe gamba bado lipoTuna act, tuna act, .. tuna act.........
zinga la acapela,.uko juu..!!
 
usipo act haiwezi kutokea utakuwa unaangalia tu
 
Tuna-act tunapenda kwenda peponi, lakin reality tukiambiwa tufe kwanza tunaogopa.
Tuna-act kupenda umeme reality kuandamana tunaogopa,
Tuna-act kuichukia 'Gamba' na mbona kura hatupigi?
Tuna-act tuna ishi, wakat reality kesho hatujui tutakula nini,
Tuna-act kukamua sana kimasomo chuon, reality ajira zenyewe vigogo washagawana.
'Acting' ni wimbo mzuri, lakin reality ni nani wa kuuimba hadharani?
 
Ofcn Nina Act kuwa Busy ile mbaya kumbe niko JF Masaa yote.
 
Ofcn Nina Act kuwa Busy ile mbaya kumbe niko JF Masaa yote.
Safi sana,wengine wana-act uongoziwa chama wakati siasa wameanza juzi.Wengine acting m'bunge wakati hawajui hata tofauti ya Polisi na TISS.Mwengine acting waziri wakati hajui tofauti ya kiti anachotumia bungeni, ofisini na kitanda anacholalia nyumbani.Acting boss, wakati vyeti vyote feki.Acting baba, wakati mtoto umesingiziwa.Acting msomi, kumbe elimu yenyewe ya kuunga unga.
 
Ma MODS naona mna-ACT
Mmenitoa SIASA, kunipeleka MMBO MCHANGANYIKO, sasa nipo CHIT-CHAT
Hii nayo ni ACT
 
Acting Mod, halafu umejiegemeza kwenye BAN tu,
Acting JF Member, so why unatetea Ufisadi?
Acting Guest, si ujiunge tu moja kwa moja?
Wabongo tunapenda sana ku-act bila kujijua
 
Acting Mod, halafu umejiegemeza kwenye BAN tu,Acting JF Member, so why unatetea Ufisadi?Acting Guest, si ujiunge tu moja kwa moja?Wabongo tunapenda sana ku-act bila kujijua
Umeona tunapenda sana ku-act bila kujijua, kumbe na wewe una-act pale unapojijua una-act nini, bahati yako hahahahhahahaa!
 
Wanafunzi vyuoni hawataki ku act kwenda mafunzo ya practical
Wafanyakazi hawataki ku act kuwa mishahara inawatosha
Machinga hawataki ku act kwamba lazima wawe na sehemu maalum
Wakulima hawataki ku act kuwa mwaka huu watavuna na kupata mazao mengi
CDM hawataki ku act kuwa wanaipenda CCM
Siye noma tunapenda ku act
 
Back
Top Bottom