Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,777
Akizungumza katika uchambuzi wa Bajeti Kuu ya Serikali 2025-2026 uliofanywa na ACT Wazalendo, Mwenyekiti wa chama hicho Dorothy Semu amesema,
"Kwa mwaka mwengine tena tunaenda kwenye uchaguzi tukiwa hatuna matumaini makubwa ya haki na msingi ya demokrasia kuzingatiwa. Tumeamua kuingia kwenye uchaguzi tukiwa na ari ya mapambano; mapambano yetu ni kulinda thamani ya kura na kuhakikisha ustawi wa wananchi.
ACT Wazalendo tunasisitiza kwamba, hatutaki fedha zetu zitumike kuumiza wananchi; hatutaki fedha hii itumike kupora maamuzi ya wananchi, tunataka uchaguzi huru na wa haki abapo vyama vyote vitapata haki na uwanja sawa wa kueleza wananchi nini cha kufanya bila bughudha.
Tunasisitiza na kueleza kwamba haya yanayoitwa mabadiliko ya sheria ya Tume ya Uchaguzi hayaridhishi na hayatoi nuru na mwanga wowote wa kuchochea mabadiliko ya kweli yatakayo hakikisha kufanyika kwa uchaguzi wa haki, kweli na wenye kuaminika.
Hivyo, ACT Wazalendo tunasisitiza madai yetu sita kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025:
Makamishna wa tume huru ya Taifa ya Uchaguzi wapatikane kwa ushindani, tume iitishe mchakato wa usaili sasa kama inavyotamkwa na sheria
Wakurugenzi wa halmashauri wasiwe wasimamizi wa majimbo, Tume iajiri watumishi wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi.
Mawakala wafanye shughuli zao bila bughudha na wasizuiwe
Wagombea wote wasienguliwe, wananchi wapewe nafasi ya mwisho kuamua viongozi wanaowataka.
Pasiwe na Kura Feki, Fedha zetu kama nchi zisitumike kuchapisha na kupitisha kura feki vituoni.
Vyombo vya ulinzi na Usalama visiingilie mchakato wa Uchaguzi.
ACT Wazalendo tunatoa angalizo na onyo kali kwa serikali kutokujihusisha na matendo yanayolenga kupora na kukiuka haki zetu katika uchaguzi huu. Tunasema, Tume ya Uchaguzi sio mali ya CCM na fedha za umma hazipaswi kutumika kuibeba CCM bali kutenda haki iliyokusudiwa."