Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Chama cha ACT-Wazalendo kinaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iweke hadharani orodha ya majina ya wagombea wetu wote wa Ubunge na udiwani ambao walikata rufaa kwake.
Hitaji hilo linatokana na taarifa ya NEC kwa umma iliyotolewa jana Septemba 8, 2020.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Wilson Mahera Charles ilisema kwamba, Tume hiyo imekubali rufaa 15 za wagombea Ubunge na kuwarejesha katika orodha ya wagombea na imekataa rufaa 15 za wagombea ambao hawakuteuliwa na pia imekataa rufaa 25 za kupinga walioteuliwa.
ACT-Wazalendo tunasema taarifa hiyo ya NEC haijitoshelezi, ina walakini na upungufu mkubwa kwa sababu haikuweka bayana majina na hata majimbo ambayo rufaa hizo tayari zimezifanyiwa kazi.
Huu ni muda muafaka kwa NEC kufanyakazi kwa weledi na uwazi mkubwa kwa kuyaweka hadharani majina yote ya wagombea waliokata rufaa, sambamba na majimbo husika ili yajulikane mapema na chama kiweze kuendelee na shughuli zake za kampeni kama tulivyopanga.
Aidha kuendelea kukaa kimya au kutokutoa taarifa zilizojitosheleza na kwa wakati kunaonyesha kuna kila dalili kwamba NEC ina nia ovu na mahsusi ya kukibeba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa gharama ya ACT -Wazalendo.
Kwakuwa uchaguzi ni mchakato wa haki, demokrasia na utawala bora, ni kazi ya NEC sasa kuonyesha kwa vitendo kwamba wanalinda haki hiyo kwa kuendesha mchakato wa uchaguzi ulio wazi, huru na haki bila upendeleo.