PostGE2025 ACT Wazalendo: Siku ya Uhuru watanzania hawakuwa na uhuru

PostGE2025 ACT Wazalendo: Siku ya Uhuru watanzania hawakuwa na uhuru

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kuadhimisha Siku ya Uhuru tarehe 9 Desemba 2025 hakukufanana na dhana ya uhuru kwa Watanzania kwani Watanzania hawakuwa huru

Kupitia taarifa rasmi ya Makamu Mwenyekiti Bara wa Chama hicho, Isihaka Mchinjita, ACT imesema hatua zilizochukuliwa na serikali kudhibiti uwezekano wa maandamano yaliyotangazwa na wanaharakati, zilipingana na maana halisi ya uhuru.

“Jana, Desemba 9, 2025, ilikuwa siku ya kusherehekea miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika. Hakika siku ambayo inapaswa kuashiria uhuru lakini Watanzania hawakuwa huru kufuatia hatua zilizochukuliwa na dola kudhibiti uwezekano wa kutokea maandamano yaliyotangazwa na wanaharakati. Hakika, NOT YET UHURU! Maandamano ya amani yalipangwa kote nchini ili kudai haki kwa waathiriwa wa ghasia baada ya uchaguzi na uwajibikaji kwa waliohusika. Hata hivyo, Serikali ilipiga marufuku, ikituma vikosi vya usalama. Vitendo hivi vinathibitisha woga wa Serikali kwa sauti ya wananchi". Imeeleza taarifa hiyo

Taarifa hiyo pia imesisitiza kupinga Tume ya Uchunguzi wa Ghasia zilizotokea baada ya Uchaguzi Mkuu, iliyoundwa chini ya uongozi wa Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande, kwa kudai kwamba tume hiyo inakosa uhuru, uwazi, na ushirikishwaji mpana wa jamii.

Aidha, ACT Wazalendo imehimiza kuingilia kati kwa mashirika ya kimataifa kama Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU) na Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC), ili kufanikisha uchunguzi wa kuaminika wa uchaguzi na ukiukaji wa haki za binadamu.

Chama hicho pia kimehimiza kuanzishwa upya kwa mchakato wa #KatibaMpya, ili kuunda mfumo unaohakikisha demokrasia ya kweli, ulinzi wa haki za wananchi, na uwajibikaji wa viongozi.

ACT imehitimisha kwa kuwataka Watanzania, asasi za kiraia na jumuiya za kimataifa kuungana pamoja ili kutimiza matarajio ya wananchi na kuijenga Tanzania yenye heshima na haki kwa wote.
1765366203369.jpeg
 
Siku ya kufungiwa ndani kama mfungwa


 
🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮🚮

IMG-20250924-WA0051.jpg
 
Back
Top Bottom