Uchaguzi 2020 ACT Wazalendo: Mgombea Ubunge wetu jimbo la Ruangwa avamiwa na kutekwa akiwa nyumbani kwake. Apatikana akiwa ametupwa porini Mkuranga

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
609
1,540
UTEKAJI UMERUDI NCHINI

TAARIFA KWA UMMA

TUMECHOSHWA NA UNYAMA HUU

Chama cha ACT-Wazalendo kimepokea kwa mshutuko taarifa za kuvamiwa, kutekwa akiwa nyumbani kwake na baadaye kupelekwa kusikojulikana mwanachama wetu, Joackim Gerion Ng’ombo na watu ambao hawajafahamika.

Ng’ombo ambaye alishika nafasi ya pili katika matokeo ya ubunge kupitia chama chetu, alitekwa na watu wasiojulikana saa 5 usiku wa kuamkia leo Agosti 13 akiwa nyumbani kwake, Kijiji cha Nangumbu, Kata ya Malolo wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi.

Watu hao walifika nyumbani kwa Nang’ombo usiku huo wa saa 5:00 ambapo walimtaka mpwa wake amuamshe ili wazungumze naye, lakini alipotoka walimkamata, kumpiga na kumburuza kisha kutokomea naye kusikojulikana. Mpaka sasa hajapatikana.

Tukio hili ambalo limeripotiwa polisi kwa RB na RUN/896/2020 nila pili kutokea katika kipindi kisichozidi wiki moja ambapo aliyekuwa mtia nia mwingine wa Jimbo hilo la Ruangwa, Said Ally Nangendekwa alitekwa, kujeruhiwa na kuumizwa vibaya maeneo mbalimbali ya mwili wake ambapo anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Faraja huko Ruangwa.

Aidha sisi kama chama tunanasibisha matukio hayo na kuwapo kwa umoja wa wazee wa Ruangwa ambao walitangaza hadharani na kuapa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aachwe awe mgombea pekee Jimbo la Ruangwa na mtu yeyote atakayejaribu kuchukua fomu basi ajulikane kwamba ni msaliti.

Baadhi ya wazee hao ambao majina yao tunayo ni pamoja na Mohammed Chande, Mohammed Kweka pamoja na Taufiq Namulya.
Kutokana na kushamiri kwa vitendo hivi, sisi ACT-Wazalendo tunatishwa na kushangazwa zaidi na ukimya wa vyombo vya dola katika kushughulikia vitendo hivi vya kinyama ambavyo vinazidi kutia doa ustawi wa jamii ya wana Ruangwa na Taifa kwa ujumla.

Kutokana na kujirudia kwa matukio haya tunamtaka Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi awajibishwe au ajiuzulu kwa kushindwa kulinda raia kwa mujibu wa kiapo chake,na kuachia vikundi vya wahalifu kufanya watakavyo.

Pia tunamtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro aingilie kati vitendo hivyo na kufanyia uchunguzi wa haraka ili kuruhusu kampeni na hatimaye Uchaguzi Mkuu vifanyike kwa amani.

Aidha tunamtaka na kumuonya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa asijiingize katika michezo michafu ya kisiasa ya kupita bila kupingwa kwa gharama ya wanachama wetu.

Majaliwa atambue kuwa nchi yetu niya mfumo wa vyama vingi vya siasa, hivyo ajipange kufanya kampeni majukwaani ili avune alichopanda na asitafute njia za mkato.

WILAYA YA NGORONGORO

Katika tukio lingine, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Hamza Mohammed Taka ameamrisha polisi kupiga wananchi, kupora na kuharibu mali, kubaka wanawake.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Ngorongoro ameagiza Jeshi la Polisi kuvamia na kufanya vitendo vya uvunjifu wa Haki za Binaadamu kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, 2020.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo tarehe 13/8/2020 katika Kata ya Sale, Kijiji cha Sale ambapo vijana wa kiume wamekimbilia porini na wazee, wanawake na watoto wamejihifadhi nyumbani kwa Diwani wa ACT Wazalendo aliyemaliza muda wake na pia ni mgombea wetu wa Kata ya Sale mwaka huu, Ndugu Mary Zakaria (0620474418).

Chanzo cha tatizo hilo ni mgogoro wa ardhi uliochochewa kisiasa na mgombea udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Hamza James Masebo anayehofia kushindwa Uchaguzi kutokana na kutokubalika kwake na wananchi. Wamasai wa Kijiji cha Malambo na Wasonjo wa Kijiji cha Sale wamechonganishwa ili kuleta vurugu kijijini hapo na kusababisha uharibufu mkubwa wa mali, mashamba, makazi, nakadhalika.

Wananchi walifanya juhudi za kuwatafuta Viongozi wao Mkuu wa Wilaya, RPC, OCD na wengineo lakini majibu ya Mkuu wa Wilaya yalikuwa “…mtaendelea Kupigwa, Kubakwa, kuharibiwa mali..mpaka msalimu amri…”

Tukio hili la uvamizi wa ardhi limetokea Juzi na jana Jeshi la Polisi usiku kuchwa limevamia kijiji cha Sale na silaha za kivita na kupiga risasi ovyo jambo lililowaogopesha sana wananchi.

ACT Wazalendo;

JOACHIM NG'OMBO APATIKANA AKIWA AMETUPWA PORINI WILAYA YA MKURANGA

ACT.jpg
 
Wahuni katika ubora wao wa kusambaza ubuyu wa kihuni. Sasa umekuja kutafuta Huruma huku ndo Kuna polisi au mahakama?

Unachukua taarifa Tena kutoka kwenye account ya mhuni ambayo haipo hata verified unaileta huku Tena ukashindwa kuambatanisha hata picha achilia mbali na vedeo ya wakipigwa.

NOTE; Hakuna Kura za Huruma mwaka huu Watanzania tushaamuka kichwani hatupo tayari kuvumilia uhuni wa Namna hii.

Mwisho; kama kweli Hilo tukio limetokea nalaani vikali na naomba polisi wachukue hatua juu ya wafanya fujo hao. Ikumbukwe; Kuna maisha baada ya uchaguzi
 
CCM ndiyo zao hizo haijalishi kama ni PM. Hiyo ni trela ya yale yatakayo wakabili wapinzani sehemu tofauti nchini. Wapinzani wanatakiwa waje na dawa ya hili. Mola wetu awape nguvu. Hapiti mtu bila kupingwa hapa.
 
Mwanasiasa yoyoye yule yeye ni maslahi kwanza,akiona maslahi yake yako kwny hatihati ndipo utamjua vzr.

Kwa hio hii unayoiona sasa hivi ndio true colour ya mkuu.
Hakika mkuu
Na hapo ndio nimeona true color yenyewe.

Pia mkuu sio wanasiasa tuu,hadi binadamu tunaoishi nao.
 
Back
Top Bottom