Mwizukulu wa Buganda
JF-Expert Member
- Nov 19, 2024
- 638
- 1,771
Chama cha ACT Wazalendo kimesema kimejipanga kuchukua hatua za Kisheria kwa kile wanachodai kuwa ni kudai haki ya ushindi walioupata katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Kauli hiyo imetolewa na Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Profesa Omar Fakih, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chama hicho eneo la Vuga, mjini Zanzibar.
Amesema katika uchaguzi huo, Chama chao kilipata ushindi kwenye jumla ya Majimbo 32 ya Ubunge, Uwakilishi na Udiwani, lakini wanadai Matokeo hayo yaliporwa, hivyo watafuata taratibu za Kisheria kudai haki yao.