ACT-Wazalendo: Maridhiano ya funika kombe tunayakataa, hatutatumika

tunaweza kubishana sku nzima kuhusu ccm na chadema, ila ukitaka kujua wananchi wanahisia gan kuhusu chadema nenda kaangalie kwa kiongozi yoyote akipost kule X comments za wananchi zikoje
Namie nakutuma

Nendeni X na Instagram then angalia kwanini account za viongozi wa serikali wakipost wanafunga comments🤣🤣
 
Mbona ni kama CHADEMA tu, kwa nini hawakuungana tangu mwanzo kuukataa ule uchaguzi, si wangefanikiwa pakubwa kuleta mageuzi? ACT hawana msimamo
Unadhani ACT Wazalendo nao wangejitoa uchaguzi usingefanyika? Hata wangeshiriki NRA, DP na CCM tu, uchaguzi ungefanyika.

Amandla...
 
Namie nakutuma

Nendeni X na Instagram then angalia kwanini account za viongozi wa serikali wakipost wanafunga comments🤣🤣
kwa sababu ya matusi, ushawahi kuona sisi tunatukana viongozi wenu?
 
Mzee wangu LMG aliwahi sema kuwa chama cha siasa ni watu.
CCM wanadai wana mtaji wa wanachama milioni 10.
CHADEMA wanadai wana wanachama milioni 10.
CHADEMA walikuja na NRNE.
Turn out ya voters GE29 ni chini ya milioni 4.

Hapo tunaona kuwa hata hao wanachama wa CCM kwa wingi, wanawasikiliza na kufuata maamuzi ya viongozi wa CHADEMA.
watu hua ni wavivu kuvote kwa sababu wanajua kiongozi bora atashinda ndo maaana kampeni zinakua kubwa sana, however tutumie presence mtandaoni kama mfano:
tuchukue page za chadema na ccm tulinganishe nani ana wafuasi wengi lakini pia twende na global latest records, kwa mfano ccm iko registered na wanachama mil 13 na katika ranking iko #9 duniani

with all these there is no denial ccm has the most
 
Maridhiano ya kweli hayawezekani ccm ikiwa madarakani - same old same.
 
Hiki chama sio cha kukiamini hata kidogo

Wakisogezewa kibunda tu wanabadili mwelekeo

Ni chama cha mapimbi flani matemate
Mnaanza wote ila mwishoni wanakutosa!
 
Mbona ni kama CHADEMA tu, kwa nini hawakuungana tangu mwanzo kuukataa ule uchaguzi, si wangefanikiwa pakubwa kuleta mageuzi? ACT hawana msimamo
kabisa , wangeeleweka kama wangeungana na chadema toka kipindi kile
 
watu hua ni wavivu kuvote kwa sababu wanajua kiongozi bora atashinda ndo maaana kampeni zinakua kubwa sana, however tutumie presence mtandaoni kama mfano:
tuchukue page za chadema na ccm tulinganishe nani ana wafuasi wengi lakini pia twende na global latest records, kwa mfano ccm iko registered na wanachama mil 13 na katika ranking iko #9 duniani

with all these there is no denial ccm has the most
I don't doubt about CCM having the most members, but they are not loyal to the party/leaders.
These members are forced to be CCM due to some advantages they hope to get,not for their wishes.
 
I amnot responsible for your assumptions
 
Hoa wanaccm mmewaingiza na id kumi kumi mnadhani hatujui hali hiyo? Uhalisia ulikuwa juzi kwenye uchaguzi, ile voters turn out iliongea kila kitu. Huko X hao uvccm hadi wamekuwa kama wajinga, wanaleta habari za kutunga kuwa viongozi wa RC na cdm wana watoto wa nje. Wote wanaigana kuhusu uzushi mnaowapa! Kama wana content kwanini kila mmija asiwe na mawazo yake, badala ya kurudia kitu hicho hicho cha mwenzake?
Nmh
 
Kamuulize JMK majibu aliyopewa na Mukandala baada ya utafiti wa kukubalika kwa CCM.
1768079651601.png

1768079686338.png

what else do you need

1768079723946.png
 
Huu ndio ujuha.
Kwa nini aende X wakati nchi hii ipo wazi.
Nendeni X na Instagram then angalia kwanini account za viongozi wa serikali wakipost wanafunga comments🤣🤣
Mbinu wanayotumia X na Instagram ni kuwa na ID nyingi halafu wanajifanya ni Umma.
Ukitaka kusoma hisia za Wananchi kasikilize mikutano ya mtandaoni.

Mbinu multiple IDs wameitumia JF pia, wamejaza watu wakiandika habari moja mara 10 ili kujaza nafasi.
Mbinu hiyo wanaifanya kwa kuifungia JF technically, ili wao waendelee nayo Umma ukiwa hauna access

Wasichokitambua ni hisia za Wananchi. Walitumia mbinu za kuwaweka mahabusu viongozi wa CHADEMAikawa ni baraka kwao maana wangekuwa nje OCT29 sijui ingekuwaje. Je, walizuia kilichotokea?

ACT hawana msimamo tangu Zitto alipoambatana na Kamati ya Mkandala kutengeneza marejeo feki ya Katiba.

Z'bar huwasikii wanagaiwa keki! si Mansour, si OMO wala Jusa. Wametulia maana waliambiwa ''ni wakati wetu''. Maalimu huko aliko sijui anajisikia.

Maalim aliasisi 'HAKI SAWA'' lakini ACT ya leo si ile ya Maalimu. Mchinjita yupo Bungeni , Dorothy anasema hataki maridhiano ni vurugu tupu. Hawa ACT si wa kuwasikiliza hata nukta

Wasubiri nusu mkate na OMO keshapeleka majina!

JokaKuu
 
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ameweka msimamo mzito kuhusu mchakato wa maridhiano nchini, akisisitiza kuwa chama hicho hakitashiriki katika mazungumzo yoyote ya "ulaghai" yanayolenga kufunika makosa yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Akizungumza kwenye kikao cha viongozi wa chama cha ACT Wazalendo kilichofanyika Januari 8, 2026 Jimbo la Lindi Mjini katika ukumbi wa Gafu, Kata ya Makonde mkoani Lindi, Semu amesema maridhiano ya kweli lazima yasimame kwenye misingi ya haki, uadilifu, na kukiri kwa makosa yaliyofanywa dhidi ya raia.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa maridhiano ya dhati yanapaswa kuambatana na mageuzi ya kimuundo katika mifumo ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi ambayo imekuwa chanzo cha migogoro nchini. Amesema kuwa ACT Wazalendo itakuwa mstari wa mbele kudai maridhiano jumuishi yanayoheshimu utu wa kila Mtanzania badala ya kutumika kama chombo cha kuhalalisha dhuluma.

Semu alitumia fursa hiyo kutoa pole kwa wanachama na wakazi wa Lindi waliokumbwa na madhila wakati wa uchaguzi, akihimiza umoja na mshikamano katika kuendelea kupigania haki za raia

Ila kwenye uchafuzi wa mwaka jana mlikubali kutumika mkitarajia mngeambulia majimbo.

Baada ya kutoswa ndio mnaonyesha jeuri.
 
Mbinu wanayotumia X na Instagram ni kuwa na ID nyingi halafu wanajifanya ni Umma.
Ukitaka kusoma hisia za Wananchi kasikilize mikutano ya mtandaoni.

Mbinu multiple IDs wameitumia JF pia, wamejaza watu wakiandika habari moja mara 10 ili kujaza nafasi.
Mbinu hiyo wanaifanya kwa kuifungia JF technically, ili wao waendelee nayo Umma ukiwa hauna access

Wasichokitambua ni hisia za Wananchi. Walitumia mbinu za kuwaweka mahabusu viongozi wa CHADEMAikawa ni baraka kwao maana wangekuwa nje OCT29 sijui ingekuwaje. Je, walizuia kilichotokea?

ACT hawana msimamo tangu Zitto alipoambatana na Kamati ya Mkandala kutengeneza marejeo feki ya Katiba.

Z'bar huwasikii wanagaiwa keki! si Mansour, si OMO wala Jusa. Wametulia maana waliambiwa ''ni wakati wetu''. Maalimu huko aliko sijui anajisikia.

Maalim aliasisi 'HAKI SAWA'' lakini ACT ya leo si ile ya Maalimu. Mchinjita yupo Bungeni , Dorothy anasema hataki maridhiano ni vurugu tupu. Hawa ACT si wa kuwasikiliza hata nukta

Wasubiri nusu mkate na OMO keshapeleka majina!

JokaKuu
Tatizo, umeadimika sana siku hizi, pengine ni kwa sababu maalum!

Kujadili ACT katika maswala ya Tanzania nyakati hizi ni kama kupoteza muda tu, kwa sababu, kama ulivyo gusia CUF/ACT ya Maalim, ni mbali kabisa na hii ya akina Kabwe/OMO na wengine wote..

Natamani sana mijadala makini kuhusu ubakwaji wa Tanzania kunakofanywa kirahisirahisi sana na huyu mwanamke ambaye kwa kawaida uwezo wake ni mdogo sana. Lakini nashindwa kujuwa amewezawezaje kuwahonga na kuwarubuni viongozi woote wakuu wa vyombo vya usalama na kukubali kumlinda yeye na Genge lake kiasi hiki tulichoweza kushuhudia hadi sasa.

Hawa watu wanaokubali kutumiwa kuunga maovu kwa teuzi mbalimbali; inakuwaje watu wote hawa wanakubali kunajisi taifa waziwazi kwa ushiriki wao katika kuendeleza uovu?

Samia kutumia uzanzibar wake kuwa kama mtawala anayetawala Tanganyika, kwa nguvu; na kuingizwa maswala ya udini kuwa kinga ya utawala.

Kuwa na mtawala mwongo, aliyejaa ulaghai wa kila aina!

Tutajikwamuaje toka kwenye hali hii? Kwa nini waTanzania wanaonekana kutegemea watu wengine kuja kuwakomboa toka kwenye mkwamo huu!

Haya ndiyo baadhi ya maswala ambayo ningependa sana mijadala makini juu yake.
 
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ameweka msimamo mzito kuhusu mchakato wa maridhiano nchini, akisisitiza kuwa chama hicho hakitashiriki katika mazungumzo yoyote ya "ulaghai" yanayolenga kufunika makosa yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Akizungumza kwenye kikao cha viongozi wa chama cha ACT Wazalendo kilichofanyika Januari 8, 2026 Jimbo la Lindi Mjini katika ukumbi wa Gafu, Kata ya Makonde mkoani Lindi, Semu amesema maridhiano ya kweli lazima yasimame kwenye misingi ya haki, uadilifu, na kukiri kwa makosa yaliyofanywa dhidi ya raia.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa maridhiano ya dhati yanapaswa kuambatana na mageuzi ya kimuundo katika mifumo ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi ambayo imekuwa chanzo cha migogoro nchini. Amesema kuwa ACT Wazalendo itakuwa mstari wa mbele kudai maridhiano jumuishi yanayoheshimu utu wa kila Mtanzania badala ya kutumika kama chombo cha kuhalalisha dhuluma.

Semu alitumia fursa hiyo kutoa pole kwa wanachama na wakazi wa Lindi waliokumbwa na madhila wakati wa uchaguzi, akihimiza umoja na mshikamano katika kuendelea kupigania haki za raia

ACT walifanya kosa kukubali kushiriki uchaguzi. Wasirudie tena kosa kwa kukubali kushiriki GNU. Huu ulaghai wa CCM laxima ufikie mwisho sasa.
 
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu, ameweka msimamo mzito kuhusu mchakato wa maridhiano nchini, akisisitiza kuwa chama hicho hakitashiriki katika mazungumzo yoyote ya "ulaghai" yanayolenga kufunika makosa yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Akizungumza kwenye kikao cha viongozi wa chama cha ACT Wazalendo kilichofanyika Januari 8, 2026 Jimbo la Lindi Mjini katika ukumbi wa Gafu, Kata ya Makonde mkoani Lindi, Semu amesema maridhiano ya kweli lazima yasimame kwenye misingi ya haki, uadilifu, na kukiri kwa makosa yaliyofanywa dhidi ya raia.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa maridhiano ya dhati yanapaswa kuambatana na mageuzi ya kimuundo katika mifumo ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi ambayo imekuwa chanzo cha migogoro nchini. Amesema kuwa ACT Wazalendo itakuwa mstari wa mbele kudai maridhiano jumuishi yanayoheshimu utu wa kila Mtanzania badala ya kutumika kama chombo cha kuhalalisha dhuluma.

Semu alitumia fursa hiyo kutoa pole kwa wanachama na wakazi wa Lindi waliokumbwa na madhila wakati wa uchaguzi, akihimiza umoja na mshikamano katika kuendelea kupigania haki za raia

Hawa mazafakas wanakumbuka shuka wakati kumeshakucha!
 
Kujadili ACT katika maswala ya Tanzania nyakati hizi ni kama kupoteza muda tu, kwa sababu, kama ulivyo gusia CUF/ACT ya Maalim, ni mbali kabisa na hii ya akina Kabwe/OMO na wengine wote..
Hoja ya ACT kwamba watalinda kura ni ya kijinga na kipuuzi sana. Maalim Seif na ushawishi aliokuwa nao hakuweza kulinda kura chaguzi 5 seuse wa leo akina OMO

Si kwamba hawakujua walifanya hivyo kama alivyosema Mansour Himid '' ... yale mambo ya JPM ya kutekana hakuna tena kwasababu sisi ni Waungwana''. kwa maana hiyo wasingeweza kwenda kinyume na muungwana.
Juzi OMO ameanza kupeleka majina kwa kujificha ili wapewe ''haki yao ya nusu mkate'' . Maalim alidai Haki-sawa
Hawa watu wanaokubali kutumiwa kuunga maovu kwa teuzi mbalimbali; inakuwaje watu wote hawa wanakubali kunajisi taifa waziwazi kwa ushiriki wao katika kuendeleza uovu?
Tatizo ni utamaduni wa business as usual. Wengi alijua CCM na Serikali zake zitadumu milele.
Kwa yaliyotokea , Wasanii wameanza kujitafakari . WanaCCM makini wanaiona hatma yao usoni.
Viongozi watabadilika, 2025 umefunua macho wengi ''the writings are on the wall''
Tutajikwamuaje toka kwenye hali hii? Kwa nini waTanzania wanaonekana kutegemea watu wengine kuja kuwakomboa toka kwenye mkwamo huu!
Kwa waliobahatika kuiona Tanzania nyakati tofauti ''Tanzania is not the same. ''Duniani, michezo huunganisha Taifa linalopitia changamoto. Tumegawanyika hadi kwa timu ya Taifa. Si kwa kuitakia mabaya na mema bali mapokezi yaliashiria jambo. Habari za Timu hazina mvumo wala mvuto! Kuna tatizo!

Kilevi kinachoitwa ''madaraka'' ni kibaya kuliko vingi hasa unapokishushia na nyama choma inayoitwa ''kiburi''. Kilevi madaraka kinaua ''sense' alizotoa Mungu! kuona ,kusikia, kugusa au kunusa. 'sense' inayobaki ni kuji mwambafai! Walevi wa kilevi hicho hawajitambui hadi watakapojikuta mitaroni. Ni kote duniani inatokea hivyo
 
Hawakutegemea wananchi wangeweza kuandamana, na wakadhani kwakuwa cdm wamegoma kushiriki wao wangeonewa huruma na ccm. Sasa wamejua kuwa msimamo wa cdm ndio ulikuwa wa wananchi, hivyo na wao sasa hivi inabidi wafuate msimamo wa cdm, kwani ndio yenye imani ya umma.

Ile voters turn out imewatisha, hawakujua kuwa wao pamoja na ccm hawana ushawishi wa umma kiasi kile. Hivyo ili wasipoteze kabisa kwenye umma, inabid kucheza bit za cdm.
Tlaatlaah ERTUGRUL BEY HAYA LAND HOV stakehigh
nonsense :HAhaa:
 
Back
Top Bottom