ACT - Wazalendo badala ya kupambana kupanda, wanatamani CHADEMA ishuke ili wao waonekane juu

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Chadema haikufika hapo ilipo kwa kutamani NCCR, CUF zishuke zife ili wao wawe juu bali walipambana na CCM hadi wakafika walipo. ACT wakitegemea CCM iwapandishe juu kwa kuihujumu Chadema hawatafika popote.

Lengo la CCM siyo kuipandisha ACT bali kuitumia ACT chini ya Zitto kuihujumu Chadema, chama kinachoonekana kuwa na msimamo kama iliyokuwa CUF ya Maalimu Seif ILI kukifanya kuwa kama CUF ya Lipumba. Baada ya CCM kufanikiwa lengo lake ACT itatupwa na kubaki kama ilivyo CUF na Zitto atadharaulika kama walivyo Lipumba na Mrema.

Zitto asijenge ACT kwa kutegemea mgongo wa Chadema na CUF akijenge chama chake kwa misingi waliyojiwekea kama chama. Chadema ina misingi yake akifata misingi ya Chadema kujenga chama chake atapotea.

“Huwezi kuwa tajiri kwa kuombea tajiri afirisike”.
 
Kinachowaponza chadema ni kishindwa kujua wanapigania nini?

Awali wananchi waliwaelewa walipokuja na ajenda ya ufisadi akaingi JPM na hyo ajenda, kawabana wote mafisadi,badala ya kumuunga mkono,wakabaki wanawakingia mafisadi kifua, na kuanza kumponda JPM

Haya Sasa, wataingia Kwa wanananchi na ajenda gani wawaelewe km hapo mwanzo?

Infact hawana Tena mvuto,kwani nao wameshaonekana wana ajenda mbaya nyuma ya pazia.

Hata kipindi Cha Corona,wakawa wanalazimisha Watu wafungiwe ndani!!

Hapo ndipo uzalendo wao ulizidi kuonekana ni zero.

Maelezo ni mengi, heri CCM waendelee tu,Hadi chama kingine chenye Nia njema na nchi hii kitakapo anzishwa
 
Awali wananchi waliwaelewa walipokuja na ajenda ya ufisadi...akaingi JPM na hyo ajenda, kawabana wote mafisadi,badala ya kumuunga mkono,wakabaki wanawakingia mafisadi kifua,...
Okay, unasema mwanzo Chadema walikuwa na ajenda ya ufisadi, Magufuli akaja na ajenda hiyo na akawabana mafisadi, kwa akili yako kwenye ajenda hiyo unadhani nani alifanikiwa.
 
Chadema mbona ilishajishukia zamani tu, sasa hivi tunapigwa nao vumbi na jua kali huku vijiweni
 
Chadema haikufika hapo ilipo kwa kutamani NCCR, CUF zishuke zife ili wao wawe juu bali walipambana na CCM hadi wakafika walipo. ACT wakitegemea CCM iwapandishe juu kwa kuihujumu Chadema hawatafika popote
 
Question from Mnyika to TCD Zitto:

“Why do you proclaim that the conference "will be attended by all parties" while even the invitation letters have not been received by respective parties and consequently confirmations have not been made hitherto?”

Respond from Zitto:

“I am a leader. Properly groomed. I desist from responding to you. However parties which won’t attend are free to do so as it is within their constitutional rights. The invitation is open to all registered political parties, CSOs and religious leaders”.
 
Vijana wa chaggadema mavi kabisa.

Kila siku ninyi ndio mnaanzisha mada na kutengeneza vikatuni vya kuwashambulia vyama vingine halafu mnataka kulaumu watu wengine.

Nawashauri tu kwa Nia njema, vijana wa chaggadema punguzeni Pombe Kali, bange na KITIMOTO.

Kama Ni kufa au kushika chadomo itashuka tu, viposti vya mitandaoni havitasaidia chochote.
 
Kinachowaponza chadema ni kishindwa kujua wanapigania nini?

Awali wananchi waliwaelewa walipokuja na ajenda ya ufisadi...
Ulichoandika hapa hakina msingi wowote.

Magufuli angewanyang'anya ajenda ya "ufisadi" Chadema, asingehangaika vile kutaka kuiua Chadema na viongozi wake. Juhudi za kuiua Chadema zinaendelea hadi sasa kwa kuwazushia kesi za ugaidi.

Chadema umekuwa mfupa mgumu sana kwa CCM, kwa maana mbvinu zote za kukiua chama hicho zinabuma. Sasa wakikosea tu na kumwachia Mbowe, hapo ndipo mwisho wa CCM utakapoanzia.

Sasa usije ukanichanganya, kwa kudhani kwamba nawapigia chepuo Chadema. Ukweli ulivyo kwa sasa Chadema ni bora kuliko chama kingine chochote bila kujali sera wanazosimamia.
 
Kinachowaponza chadema ni kishindwa kujua wanapigania nini?

Awali wananchi waliwaelewa walipokuja na ajenda ya ufisadi.
Hakuna mwanaCCM asiyependa CCM iendelee.

Hakuna mwanaCCM anayejua CHADEMA inasimamia nini.

Kwa hiyo ni haki yako kulitetea hilo takataka lako,mtaanzisha vyama kibao lakini CHADEMA Ipo hapa milele na soon itakuoneaha inachosimamia.
 
Kinachowaponza chadema ni kishindwa kujua wanapigania nini?

Awali wananchi waliwaelewa walipokuja na ajenda ya ufisadi akaingi JPM na hyo ajenda, kawabana wote mafisadi,badala ya kumuunga mkono,wakabaki wanawakingia mafisadi kifua, na kuanza kumponda JPM

Haya Sasa, wataingia Kwa wanananchi na ajenda gani wawaelewe km hapo mwanzo?

Infact hawana Tena mvuto,kwani nao wameshaonekana wana ajenda mbaya nyuma ya pazia.

Hata kipindi Cha Corona,wakawa wanalazimisha Watu wafungiwe ndani!!

Hapo ndipo uzalendo wao ulizidi kuonekana ni zero.

Maelezo ni mengi, heri CCM waendelee tu,Hadi chama kingine chenye Nia njema na nchi hii kitakapo anzishwa

Magufuli hakuwahi kupambana na mafisadi, bali alikuwa analipa visasi kwa matajiri aliokuwa na chuki nao. Sana sana alikuwa anapambana na matumizi ya neno fisadi. Hakuna mtu anapambana na mafisadi akawa adui wa vyombo vya habari. Kutokana na propaganda zilizokuwepo zililenga kuonyesha Magufuli anakubalika na wananchi, lakini alichokifanya kunajisi uchaguzi kulidhihirisha hakuwa anakubalika kama propaganda zilivyokuwa.

Hiyo kuwa cdm imepoteza mvuto ni matamanio ya kila mwanaccm, ndio maana cdm hashindani na ccm tena, bali vyombo vya dola ndio vimebeba jukumu hilo. Ili tuamini Simba au Yanga zimepoteza mvuto, tunataka ziingie uwanjani bila vyombo vya dola kuwaingilia, kisha tuone wakipoteza ushindi. Sio hiyo ya cdm imepoteza mvuto, lakini wakifanya mkutano tu na watu kujaa mnaanza kuwabambikia kesi, na hawaruhusiwi kufanya mkutano. kwenye uchaguzi tunaona mabox ya kura yakiletwa kuibeba ccm, tena kwa uratibu wa vyombo vya dola. Cdm haiwezi kufa kwa kuifanyia hila maana kwa sasa cdm ni imani.
 
Chadema haikufika hapo ilipo kwa kutamani NCCR, CUF zishuke zife ili wao wawe juu bali walipambana na CCM hadi wakafika walipo. ACT wakitegemea CCM iwapandishe juu kwa kuihujumu Chadema hawatafika popote.

Lengo la CCM siyo kuipandisha ACT bali kuitumia ACT chini ya Zitto kuihujumu Chadema, chama kinachoonekana kuwa na msimamo kama iliyokuwa CUF ya Maalimu Seif ILI kukifanya kuwa kama CUF ya Lipumba. Baada ya CCM kufanikiwa lengo lake ACT itatupwa na kubaki kama ilivyo CUF na Zitto atadharaulika kama walivyo Lipumba na Mrema.

Zitto asijenge ACT kwa kutegemea mgongo wa Chadema na CUF akijenge chama chake kwa misingi waliyojiwekea kama chama. Chadema ina misingi yake akifata misingi ya Chadema kujenga chama chake atapotea.

“Huwezi kuwa tajiri kwa kuombea tajiri afirisike”.

ACT ndio wazuri, CCM waliwatandika viboko na risasi hadi mbunge wao mmoja akafariki. Lakini bado wakaenda kufunga ndoa na CCM kwa kupewa Wizara mbili tu na nafasi ya Makamu wa Rais ambaye majina aliteua Rais mwenyewe wa CCM baada ya kupelekwa majina matatu. Hao ndio CCM anawataka anakufanya atakavyo lakini huondoki.
 
Tangu
Vijana wa chaggadema mavi kabisa.

Kila siku ninyi ndio mnaanzisha mada na kutengeneza vikatuni vya kuwashambulia vyama vingine halafu mnataka kulaumu watu wengine.

Nawashauri tu kwa Nia njema, vijana wa chaggadema punguzeni Pombe Kali, bange na KITIMOTO.

Kama Ni kufa au kushika chadomo itashuka tu, viposti vya mitandaoni havitasaidia chochote.

Tangu enzi za wasira naskia CHADEMA itakufa mpaka leo. Wao wanakufa wanaiacha.
 
Chadema haikufika hapo ilipo kwa kutamani NCCR, CUF zishuke zife ili wao wawe juu bali walipambana na CCM hadi wakafika walipo. ACT wakitegemea CCM iwapandishe juu kwa kuihujumu Chadema hawatafika popote.

Lengo la CCM siyo kuipandisha ACT bali kuitumia ACT chini ya Zitto kuihujumu Chadema, chama kinachoonekana kuwa na msimamo kama iliyokuwa CUF ya Maalimu Seif ILI kukifanya kuwa kama CUF ya Lipumba. Baada ya CCM kufanikiwa lengo lake ACT itatupwa na kubaki kama ilivyo CUF na Zitto atadharaulika kama walivyo Lipumba na Mrema.

Zitto asijenge ACT kwa kutegemea mgongo wa Chadema na CUF akijenge chama chake kwa misingi waliyojiwekea kama chama. Chadema ina misingi yake akifata misingi ya Chadema kujenga chama chake atapotea.

“Huwezi kuwa tajiri kwa kuombea tajiri afirisike”.
ACT ilipandishwa na Maalim 2025 inafutika kabisa
 
Hivi kati ya Chadema na ACT ni nani anaefatilia sana mambo ya mwenzake?

CHADEMA ni chama kinachobomolewa na BAVICHA maana hayajielewi
 
Back
Top Bottom