ACT-Tanzania, Mapato na matumzi ya chama

ACT-Tanzania, Mapato na matumzi ya chama

Jamani mi Mgeni hapa ,hivi hicho ki ACT ni kikundi cha Sanaa au ni kikundi cha uharamia ?
 
Soon ACT itafunika vibaya,vyama vingine ukihoji matumizi utaitwa msaliti na majina yote mabaya mwisho ni kuvuliwa uanachama,kumbe act jambo hili ni moja ya sera zake!!!??? Inapendeza sana.
 
"Chama kinatamani ikiwezekana kiwe kinatoa taarifa zake kila mwezi lakini kwa kipindi hiki cha kuanzia, hakitaweza kufanya hivyo kwa kuwa zoezi hilo linahitaji gharama kubwa na chama bado hakijawa na chanzo cha mapato cha kuaminika"

Hapo kwenye RED, kwani hazina ya serikali kuu chini ya Mwigulu imekwenda wapi? Vipi zile za mgawo wa Escrow account hazijafika huko?

Tiba
hawa vijana nilifikiri kushinda kwao mitandaoni wana jipya kumbe wanakula hela ya zzk bure tu
 
hawa vijana nilifikiri kushinda kwao mitandaoni wana jipya kumbe wanakula hela ya zzk bure tu

Ngoja wazile, wasipokula wao nani mwingine tena atakula? Bahati mbaya ni kodi zetu hizo zinatumika ovyo badala ya kutumika kwenye shughuli za kuleta maendeleo.

Tiba
 
hawa vijana nilifikiri kushinda kwao mitandaoni wana jipya kumbe wanakula hela ya zzk bure tu
Vinana gani? na wewe umejua je kuwa wanakula hela za zzk? au wewe cashier wa zzk? rudi kwenye mada maana utakuwa kuko smart zaidi kidogo ya hivyo.
 
Ngoja wazile, wasipokula wao nani mwingine tena atakula? Bahati mbaya ni kodi zetu hizo zinatumika ovyo badala ya kutumika kwenye shughuli za kuleta maendeleo.

Tiba

Dah! aisee! ACT-Tanzania wanakula kodi yako, wanaitumia ovyo badala ya kufanyia shughuli za maendeleo, halafu ni bora tu kuwaacha wale maana hakuna mtu mwingine wa kuzila! aisee!

Ni Tiba !!!!!!!!1!? au macho yangu?
 
Last edited by a moderator:

Hicho chama chako ni tawi la CCM mko funded na ccm hiyo hiyo and pesa inayotumiwa na ccm ni ya walipa kodi kama mimi. Bado unabisha?
 
Last edited by a moderator:
Hicho chama chako ni tawi la CCM mko funded na ccm hiyo hiyo and pesa inayotumiwa na ccm ni ya walipa kodi kama mimi. Bado unabisha?
Inaonekana wewe ni mjuvi mzuri.Sasa wewe ni mhasibu upande wa CCM (Wanaotoa fund) au muhasibu upande wa ACT-Tanzania (wapokea fund) au wewe ni transaction facilitator, au wewe observer tu unayetizama jinsi ACT-Tanzania wanavyotumia vibaya kodi yako lakini huna la kufanya kwa kuwa wasipoila wao hamna wa kuila kama ulivyosema hapo awali?

Yap kula tu wakati wenu ndo huu.
 
Ndugu watanzania wote kwa ujumla, kokote mlipo tunawasalimu kwa salamu inayo ashiria mabadiliko na uwazi.

Ndugu watanzania, miongoni mwa maswali ambayo watanzania walikuwa wameuliza kuhusiana na chama cha ACT-Tanzania, ni pamoja na kutaka kujua kwamba chama kilitumia kiasi gani cha fedha katika zoezi la usajili na uhakiki wa wanachama waanzilishi zaidi ya 2000, na mpaka sasa chama kimetumia kiasi gani cha fedha, kimebaki na kiasi gani cha fedha na kimepata wapi fedha hizo.

Swali hili kimsingi ni muhimu sana kwa kuwa linagusa moja kwa moja moja ya msingi mmojawapo mkubwa wa chama, yaani "msingi wa uwazi"; ambapo chama kinaamini kwamba ni lazima kifanye shughuli zake kwa uwazi wa hali ya juu.Vile vile chama kinatambua kuwa miongoni mwa maeneo yanayofaa kupimia uadilifu wa watu ni katika eneo hili la mapato na matumizi.

Kwa kuwa ACT-Tanzania inajipambanua katika misingi ya uwazi √

Kwa kuwa ACT-Tanzania ni chama cha siasa cha mfano nchini √

Kwa kuwa taasisi yoyote ya umma ina wajibu wa kuweka wazi mapato na matumizi yake kwa kuwa yanatokana na umma wenyewe √

Kwa kuwa wanachama wanajitahidi kuchangia chama kwa moyo safi pamoja na kuwa na kipato duni √

Na kwa kuwa ACT- Tanzania imekuja kumaliza mazingaombwe ya kisiasa nchini √

ACT- Tanzania inapenda kuwafahamisha watanzania wote kwamba, kwa kuanzia itakuwa ikitoa taarifa zake za mapato na matumizi kwa umma, kila baada ya kipindi cha robo mwaka (miezi mnne) kwa kuanzia.Chama kinatamani ikiwezekana kiwe kinatoa taarifa zake kila mwezi lakini kwa kipindi hiki cha kuanzia, hakitaweza kufanya hivyo kwa kuwa zoezi hilo linahitaji gharama kubwa na chama bado hakijawa na chanzo cha mapato cha kuaminika.Kama ambavyo watanzania wengi wamekishauri chama kuwa kila kinapotoa taarifa muhimu, kisitegemee mitandao ya kijamii pekee bali kutumia mbinu zote za mawasiliano ili kuwafikia watanzania wote, ni dhahiri kwamba zoezi hilo linahitaji gharama kidogo.

Chama kinawaomba watanzania wahesabu miezi minne toka chama kilipopata usajili wa kudumu na hapo wasipopata taarifa ya fedha, basi watakuwa na haki ya kuhoji.Ni jambo lisolokuwa na wasi wasi kwamba taarifa itakapotoka kila mtu atajua ACT-Tanzania inapata wapi mapato yake, imepata kiasi gani, imetumia kiasi gani, imetumia kwenye nini, na imebaki na nini.

Ni matumaini yetu kwamba kila mtanzania mzalendo atakuwa ametuelewa vyema.

Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa ajili ya taifa letu leo na kesho!

Tuwasiliane kwa acttanzania@yahoo.com au acttanzania@gmail.com

Act wazalendo ahadi ni deni .. Tunaomba mapato na matuzimi ya chama..

Aione Kapwela , Mkandara, JokaKuu, Zitto na wengineo..

Si maneno yangu bali ya ACT Wazalendo...
 
Last edited by a moderator:
Act wazalendo ahadi ni deni .. Tunaomba mapato na matuzimi ya chama..

Aione Kapwela , Mkandara, JokaKuu, Zitto na wengineo..

Si maneno yangu bali ya ACT Wazalendo...
Dada unahangaika sana na huyu Zito kulikoni?? Angalia hizi chuki sio nzuri kwa afya yako na Familia yako.
 
Last edited by a moderator:
Dada unahangaika sana na huyu Zito kulikoni?? Angalia hizi chuki sio nzuri kwa afya yako na Familia yako.

Chuki tena? Yaani kukumbushia jambo ambalo wao walituahidi ni chuki? hebu wasome hapo juu.. Watanzania tubadilike tuwe na ujasiri wa kuhoji, kuuliza maswali pale penye utata, na nk.

Tusiwaache wanasiasa wakatufanya sisi ni vichwa vya wanawazimu. Na nipouuliza kitu ambacho chama kiliahidi tena kwa maandishi hizo si chuki bali ni kutaka kujua ukweli kuwa je ni kweli wanazingatia yale wasemayo? au ni kama wale wale tuliowazoea..

Ni wajibu wetu kuona hizi siasa za kilaghai zinakoma iwe kwa Chadema, CCM, ACT na chama chochote kile.

Hivyo basi ni wajibu wa ACT- Wazalendo kuleta mapato na matumizi kama walivyoahidi mwenyewe la sivyo watakuwa hawana tofauti na vyama vingine.. Kitila Mkumbo
 
Act wazalendo ahadi ni deni .. Tunaomba mapato na matuzimi ya chama..

Aione Kapwela , Mkandara, JokaKuu, Zitto na wengineo..

Si maneno yangu bali ya ACT Wazalendo...
Mnachokosea nyie katika mjadala huu ni dhana au kufikiri kwamba pengine mimi ni mwanachama wa ACT ama naunga mkono kila wanalolifanya kina Zitto. Dada Alinda Unakosea sana, kwa sababu mimi nachoandika ni REALITY kama ninavyoiona mimi. Ndio maana nikasema ACT ni zao la CDM wenyewe, ACT yaweza kuwa mpini wa CCM lakini alouchonga mpini ni CDM, ndio maana nikamtetea Mwigamba, Kitila na Zitto walipofukuzwa CDM. Toka najiunga Jamii forums katika mijadala yetu miye hutazama Uhalisia zaidi ya Matumaini kwa sababu siwezi kuweka matumaini mahala ambapo Wadanganyika wenyewe ni wanafiki na vigeugeu..Nawatazama kwanza Wadanganyika wenyewe kisha naunganisha na wazo ama idea ilojitokeza..

Kitu pekee kinachoniweka mimi sawa na ACT ni Mrengo wao kaitka siasa za UJAMAA na kurudisha misingi tuliyoanza nayo katika ujenzi wa Taifa letu. Hawa matajiri iwe ni watu aa mataifa matajiri siku zote ni WANAFIKI na walaghai wakubwa wapo tayari kutumia fedha zao kutununua na kama fedha ikishindikana kuwanunua basi watatumia nguvu. Ndipo ujue hawakuwa na nia njema toka mwanzo.

Kwa hiyo nawatetea kina Zitto katika yale nayoyaona nia njema zile siasa za majitaka kwa sababu Zitto alifukuzwa CDM inakuwaje watu wanamfuata hadi alikokimbilia? Mkisha mfukuza mtu atoke nje ya nchi na akapanda pipa halafu bado unamfuata hadi huko aliko, inatupa shaka zaidi sisi tunaofuatilia siasa za Bongo..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom