ACT-Tanzania, Mapato na matumzi ya chama

ACT-Tanzania, Mapato na matumzi ya chama

Mnachokosea nyie katika mjadala huu ni dhana au kufikiri kwamba pengine mimi ni mwanachama wa ACT ama naunga mkono kila wanalolifanya kina Zitto. Dada Alinda Unakosea sana, kwa sababu mimi nachoandika ni REALITY kama ninavyoiona mimi. Ndio maana nikasema ACT ni zao la CDM wenyewe, ACT yaweza kuwa mpini wa CCM lakini alouchonga mpini ni CDM, ndio maana nikamtetea Mwigamba, Kitila na Zitto walipofukuzwa CDM. Toka najiunga Jamii forums katika mijadala yetu miye hutazama Uhalisia zaidi ya Matumaini kwa sababu siwezi kuweka matumaini mahala ambapo Wadanganyika wenyewe ni wanafiki na vigeugeu..Nawatazama kwanza Wadanganyika wenyewe kisha naunganisha na wazo ama idea ilojitokeza..

Kitu pekee kinachoniweka mimi sawa na ACT ni Mrengo wao kaitka siasa za UJAMAA na kurudisha misingi tuliyoanza nayo katika ujenzi wa Taifa letu. Hawa matajiri iwe ni watu aa mataifa matajiri siku zote ni WANAFIKI na walaghai wakubwa wapo tayari kutumia fedha zao kutununua na kama fedha ikishindikana kuwanunua basi watatumia nguvu. Ndipo ujue hawakuwa na nia njema toka mwanzo.

Kwa hiyo nawatetea kina Zitto katika yale nayoyaona nia njema zile siasa za majitaka kwa sababu Zitto alifukuzwa CDM inakuwaje watu wanamfuata hadi alikokimbilia? Mkisha mfukuza mtu atoke nje ya nchi na akapanda pipa halafu bado unamfuata hadi huko aliko, inatupa shaka zaidi sisi tunaofuatilia siasa za Bongo..

Hoja iliyopo ni mapato na matumizi ya ACT (chama unachotetea katika mrengo wao) Wao walituahidi kuleta kila baada ya robo mwaka report ya mapato na matumizi ya chama chao.. Hivyo mimi mimi Alinda ambaye ni mtanzania ninayohaki ya kuhoji walichotuahidi. Na ndicho nilichofanya.

Nimekumention Wewe kwa ungwana tu kaka yangu kwani ulishawahi uliza lini na wapi ACT wazalendo walisema kuleta report ya mapato na matumizi..

Pia ni muhimu pale vyama vya siasa wanaposema jambo basi walitekeleza sasa kama wasipotekeleza jambo dogo kama ili tuawaaminije katika mambo makubwa?
 
Hoja iliyopata ni mapato na matumizi ya ACT (chama unachotetea katika mrengo wao) Wao walituahidi kuleta kila baada ya robo mwaka report ya mapato na matumizi ya chama chao.. Hivyo mimi mimi Alinda ambaye ni mtanzania ninayohaki ya kuhoji walichotuahidi. Na ndicho nilichofanya.

Nimekumention Wewe kwa ungwana tu kaka yangu kwani ulishawahi uliza lini na wapi ACT wazalendo walisema kuleta report ya mapato na matumizi..

Pia ni muhimu pale vyama vya siasa wanaposema jambo basi walitekeleza sasa kama wasipotekeleza jambo dogo kama ili tuawaaminije katika mambo makubwa?
Nakumbuka walisema report ipo katika Ofisi zao mwenye kuzitaka utazipata huko. Halafu kama nilivyosema jamani tufuate Uhalisia zaidi kwa sababu ACT hakuna chama kinachoanika hesabu zake kwa kila mwezi au siku. Huwa kuna utaratibu maalum wa aidha miezi kila miezi mitatu, sita au mwaka. Mahesabu hayatolewi kila mtu anapoyataka hata Tukisema ya CDM au CCM hata nbila wao kudai hivyo unaweza kuzipata ukifiata tu utaratibu wao..
 
Mkandara wasome wenyewe.. Walisema hivi Chama kinawaomba watanzania wahesabu miezi minne toka chama kilipopata usajili wa kudumu na hapo wasipopata taarifa ya fedha, basi watakuwa na haki ya kuhoji.Ni jambo lisolokuwa na wasi wasi kwamba taarifa itakapotoka kila mtu atajua ACT-Tanzania inapata wapi mapato yake, imepata kiasi gani, imetumia kiasi gani, imetumia kwenye nini, na imebaki na nini.

Pia wakasema:
Kama ambavyo watanzania wengi wamekishauri chama kuwa kila kinapotoa taarifa muhimu, kisitegemee mitandao ya kijamii pekee bali kutumia mbinu zote za mawasiliano ili kuwafikia watanzania wote, ni dhahiri kwamba zoezi hilo linahitaji gharama kidogo.

Hapo hakuna wanaposema taarifa tuzifuate ofisini.

Well leo katika hotuba yao wamesema chama kina siku 97 kwa hiyo subiri...
 
Ndugu watanzania wote kwa ujumla, kokote mlipo tunawasalimu kwa salamu inayo ashiria mabadiliko na uwazi.

Ndugu watanzania, miongoni mwa maswali ambayo watanzania walikuwa wameuliza kuhusiana na chama cha ACT-Tanzania, ni pamoja na kutaka kujua kwamba chama kilitumia kiasi gani cha fedha katika zoezi la usajili na uhakiki wa wanachama waanzilishi zaidi ya 2000, na mpaka sasa chama kimetumia kiasi gani cha fedha, kimebaki na kiasi gani cha fedha na kimepata wapi fedha hizo.

Swali hili kimsingi ni muhimu sana kwa kuwa linagusa moja kwa moja moja ya msingi mmojawapo mkubwa wa chama, yaani "msingi wa uwazi"; ambapo chama kinaamini kwamba ni lazima kifanye shughuli zake kwa uwazi wa hali ya juu.Vile vile chama kinatambua kuwa miongoni mwa maeneo yanayofaa kupimia uadilifu wa watu ni katika eneo hili la mapato na matumizi.

Kwa kuwa ACT-Tanzania inajipambanua katika misingi ya uwazi √

Kwa kuwa ACT-Tanzania ni chama cha siasa cha mfano nchini √

Kwa kuwa taasisi yoyote ya umma ina wajibu wa kuweka wazi mapato na matumizi yake kwa kuwa yanatokana na umma wenyewe √

Kwa kuwa wanachama wanajitahidi kuchangia chama kwa moyo safi pamoja na kuwa na kipato duni √

Na kwa kuwa ACT- Tanzania imekuja kumaliza mazingaombwe ya kisiasa nchini √

ACT- Tanzania inapenda kuwafahamisha watanzania wote kwamba, kwa kuanzia itakuwa ikitoa taarifa zake za mapato na matumizi kwa umma, kila baada ya kipindi cha robo mwaka (miezi mnne) kwa kuanzia.Chama kinatamani ikiwezekana kiwe kinatoa taarifa zake kila mwezi lakini kwa kipindi hiki cha kuanzia, hakitaweza kufanya hivyo kwa kuwa zoezi hilo linahitaji gharama kubwa na chama bado hakijawa na chanzo cha mapato cha kuaminika.Kama ambavyo watanzania wengi wamekishauri chama kuwa kila kinapotoa taarifa muhimu, kisitegemee mitandao ya kijamii pekee bali kutumia mbinu zote za mawasiliano ili kuwafikia watanzania wote, ni dhahiri kwamba zoezi hilo linahitaji gharama kidogo.

Chama kinawaomba watanzania wahesabu miezi minne toka chama kilipopata usajili wa kudumu na hapo wasipopata taarifa ya fedha, basi watakuwa na haki ya kuhoji.Ni jambo lisolokuwa na wasi wasi kwamba taarifa itakapotoka kila mtu atajua ACT-Tanzania inapata wapi mapato yake, imepata kiasi gani, imetumia kiasi gani, imetumia kwenye nini, na imebaki na nini.

Ni matumaini yetu kwamba kila mtanzania mzalendo atakuwa ametuelewa vyema.

Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa ajili ya taifa letu leo na kesho!

Tuwasiliane kwa acttanzania@yahoo.com au acttanzania@gmail.com
Ikumbukwe kuwa ACT-Tanzania ni kwa ajili ya taifa letu leo na kesho! Hapana hapana!!!!!!!!!!!!! huuu ni uongo ACT ipo kwa ajili nya ZZK NDO MAANA ILIANZA MUDA MFUPI KABLA YA KUJIONDO CDM. ZZK UNAMDANGANYA NANI ,KWANZUNATUMIWA NA CCM. PILI WEWE NI MSALITI MKUBWA WA MAPAMBANO DHIDI YA MAFISADI WA NCHI HII. WEWE NI SHOCK ABSORBER WA CCM DHIDI YA KASI KUBWA YA UKAWA. KWAHIYO USIANDIKE AYA NDEFU KUWAPUMBAZA WATU. UMEANZA VIBAYA NA UTAMALIZA VIBAYA
 
Well leo katika hotuba yao wamesema chama kina siku 97 kwa hiyo subiri...

Kama wamesema hivyo basi au wao ni waongo au hakuelewa vizuri walichosema maana ACT wazalendo ilipata usajili wa kudumu tarehe 5.5.2014 na mwaka huu wamesherekea mwaka mmoja wa ACT. soma hapa.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/846150-act-wazalendo-taarifa-kwa-vyombo-vya-habari.html

Hivyo basi si kweli kuwa ACT wazalendo kina siku 97 bali kina siku zaidi ya 365.

Wasimamie wanalohubiri walete mapato na matumizi ya chama chao.
 
Alinda nimekupenda bure (no offense). Umembana Mkandara vilivyo kwa data. Na hii ndio njia pekee ya kuonesha utapeli na uongo wa hawa jamaa. Walituambia tuhesabu miezi minne sasa leo tunaambiwa eti wana siku 97 how come? Unajua ACT wanatka umaarufu na mafanikio ya haraka kwa kuahidi vitu ambavyo haviwezekani km CCM. Mfano naona jana Zitto katika hotuba yake hakutaja kabisa neon ujamaa wakti ndio sera kuu ya chama. sasa wameanza kufanya U-turn au nini?

ACT tupeni taarifa ya mapato na matumzi km mlivyoahidi! Acheni porojo.
 
Du, nimekuja fasta kuangalia ma balance sheet na ma trading acc but nimekutana na ahadi! Kuanzia leo sitakua nafungua uzi ulioanzishwa ma act wazalendo na mtela mwampamba, sababu ni ndogo tu, hawa watu ni waongo sana.
 
Well leo katika hotuba yao wamesema chama kina siku 97 kwa hiyo subiri...

Kweli sasa sielewi ukweli ni upi na kwanini kulikuwa na ugomvi na akina Limbu. Haiwezekani chama hiki kilianzishwa siku 97 zilizotangulia kwa sababu kilitokana na chama alichokuwa anaongoza Limbu.

Sitaki kusikia kuwa ACT -Wazelendo no chama kipya cha siasa. Labda niambiwe sasa kuwa taratibu za uanzishwaji wa chama zilikiukwa. Na kwann ilikuwa hivo.
 
Kama wamesema hivyo basi au wao ni waongo au hakuelewa vizuri walichosema maana ACT wazalendo ilipata usajili wa kudumu tarehe 5.5.2014 na mwaka huu wamesherekea mwaka mmoja wa ACT. soma hapa.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/846150-act-wazalendo-taarifa-kwa-vyombo-vya-habari.html

Hivyo basi si kweli kuwa ACT wazalendo kina siku 97 bali kina siku zaidi ya 365.

Wasimamie wanalohubiri walete mapato na matumizi ya chama chao.
OK, pengine mimi ndio nimeisoma vibaya hotuba ya Mwigamba ktk ukurasa wa Zitto...Kifupi mimi nachotaka kusikia ni ukombozi wa Taifa hili haya ya
ACT sijui mahesabu ya CDM wakati Taifa linahitaji Siasa safi na Uongozi bora hazinisumbui kichwa kabisa. Hivi vitu hivi viwili ndivyo vimetufikisha hapa tulipo leo.
 
ok, pengine mimi ndio nimeisoma vibaya hotuba ya mwigamba ktk ukurasa wa zitto...kifupi mimi nachotaka kusikia ni ukombozi wa taifa hili haya ya
act sijui mahesabu ya cdm wakati taifa linahitaji siasa safi na uongozi bora hazinisumbui kichwa kabisa. Hivi vitu hivi viwili ndivyo vimetufikisha hapa tulipo leo.
.
Njia ya mwongo ni fupi. Ujamaa si kazi rahisi kama anavyofikiri zzk. Very soon watakuwa flat hawa ndipo unafiki wao utakapodhihika wazi mbele ya watz. Zzk atajuta kuiacha cdm maana ndiko alikopandia na kuwa maarufu
 
Mkuu UJAMAA ndio njia pekee ya kulikomboa taifa letu hapo tutabishana hadi kesho kwa sababu nyie mnafikiria kwamba UJAMAA ni wa aina moja na mkachukulia mifano ya miaka ya 1970s wakati hata huo Ubepari miaka ya 80s uli fail kwa baadhi ya Nchi na leo zipo zinazo fail vibaya kabisa. Hiyo Ugiriki iko wapi leo, Purto Rico, Zimbabwe sii mabepari wale. hao Kenya ni mabepari toka enzi ya Nuhu wako wapi haswa mbona wanakuja tafuta kazi Tz?

Watu wengi mnashindwa kuelewa kwamba UJamaa haipingi Soko Huria wala Utandawazi isipokuwa nchi za Kijamaa ndizo hutengwa na nchi za Kibepari wanapokataa kutawaliwa kiuchumi wakati hao Mabepari wanajua wewe maskini huwezi kutawala uchumi wa nchi zao hata kama watakupa nafasi hiyo. Na bado, wanachokifanya watakufungia wewe Mjamaa kama wanavyoifanya Cuba na North Korea kwa visingizio vya haki za binadamu lakini ukifungua milango tu hawatajali kama haki hizo umewapa wananchi wao.

Wao wanatazama interest zao tu nanyi mnafikiri wanajali sana haki za binadamu. tazama Misri na Libya wamezifanya nini kama sio kutawaliwa kiuchumi. Kama wangetaka kweli tujue Ujamaa haufai wangiruhusu Cuba ifanye nao biashara maana sio Cuba iliiwekea vikwazo Marekani bali ni Marekani waloiwekea vikwazo Cuba. Na unapowekewa Vikwazo haijalishi wewe ni Mjamaa au Bepari utakwama tu, tazama Libya, Iran, Zimbabwe..wambie waache kweli soko liwe Huru na Utandawazi bila vikwazo halafu tuone kama kweli nchi za Kijamaa zita fail..
 
unajua ndg zangu, mjanja kuwahi. ukisubiri saccos za kawaida ili zikuinue kiuchumi utalala mlango wazi. jamaa ana-struggle apate tu wabunge angalau wawili ili ruzuku na michango mingine imuzoee. zzk alishasema yeye si mwanasiasa, kwake ualimu na kilimo ndo kila kitu. kesho yake akageuza kibao huku akiamini wtz ni mazuzu hawawezi kumbuka alichosema jana. palitica saccos are paying, nyie pigeni kelele tu. akina mlamba alichota mabilion lkn wameambiwa walete mil. 5, na miaka mitatu ambayo ni kama ck 2 tu kwa wizi wake
 
OK, pengine mimi ndio nimeisoma vibaya hotuba ya Mwigamba ktk ukurasa wa Zitto...Kifupi mimi nachotaka kusikia ni ukombozi wa Taifa hili haya ya
ACT sijui mahesabu ya CDM wakati Taifa linahitaji Siasa safi na Uongozi bora hazinisumbui kichwa kabisa. Hivi vitu hivi viwili ndivyo vimetufikisha hapa tulipo leo.

Sawa kabisa Taifa linahitaji Siasa safi na Uongozi bora, Lakini utawezaje kuwa na kiongozi bora kama kiongozi huyu ni Muongo au mlaghai? Siasa safi zinapatikana pale chama chochote cha siasa kinaposimamia mambo/jambo kilichoahidi.

Hawezikani Chama chochote kilichoanza kwa misingi ya uongo na ulaghai kuja kuwa chama chenye siasa safi, Na haiwezekani kiongozi yeyote yule ambaye anashindwa hata kutekeleza jambo lolote aliloahidi mwenye kuja kuwa Kiongozi safi. Na hatutegemei ACT ifanye wafanyavyo Chadema au CCM maana kama ni hivyo hakuna haja ya kuwa na ACT wazalendo. Maana wanafanya mambo yale yale wafanyao vyama vingine.

ACT tunataka kujua mapato na matumizi ya mapato yetu,
 
Du, nimekuja fasta kuangalia ma balance sheet na ma trading acc but nimekutana na ahadi! Kuanzia leo sitakua nafungua uzi ulioanzishwa ma act wazalendo na mtela mwampamba, sababu ni ndogo tu, hawa watu ni waongo sana.
Nakuunga mkono kabsa haina haja kufungua post zao jamaa ni weu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom