Acheni wanawake watambe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Acheni wanawake watambe!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 13, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Inawezekana ni kweli wanaume wanaitawala dunia katika kile tunachokiita Mfumo Dume, lakini nao wanawake wanatawala kiota, siyo dunia. Ina maana gani? Kwa mujibu wa utafiti mpya wa hivi karibuni, inaonesha kwamba, wanawake wana nguvu kwenye maamuzi ya masuala ya nyumbani kuliko wanaume.

  Watafiti wamegundua kwamba, wanawake kwa wastani, wanakuwa na nguvu kubwa ya uamuzi, unapokuja mjadala nyumbani unaohusu familia. Bila kujali kama ni mwanamke au mwanamume aliyeanzisha majadala huo, wanawake siku zote ndiyo wenye nguvu kwenye kauli ya mwisho.
  Ndiyo maana ni rahisi hata kwa wanaume wakorofi kusikika wakisema, ‘nimeamua tufanye alivyotaka, ngoja mambo yaende vibaya, atanijua. Nimemwachia kusudi kama alivyotaka tufanye, lakini ataona mambo yakiharibika.’ Mara nyingi, mwanamke ndiye anayesikilizwa.
  Lakini, inaonesha kwamba, kwenye zile ndoa ambapo wanawake husikilizwa zaidi yanapokuja masuala ya ndani, ndoa hizo zinakuwa imara zaidi.
  Hii inaonesha kwamba, huenda mwanamke mahali pake siyo jikoni, bali ni nyumbani, yaani ni mtaalamu wa masuala ya familia na uhusiano kwa ujumla, ingawa mwenyewe hajui. Ndoa inapofikia miaka saba, kukawa na amani ya kuridhisha, kama wanawake kwenye ndoa hizo ndiyo wazungumzaji wakuu wa masuala ya ndani, mafanikio ya kindoa na kifamilia huwa mazuri, ukilinganisha na pale ambapo wanaume ndiyo wasemaji wakuu.

  Hii ina maana kwamba, ili kufikia mafanikio ya juu katika familia, mwanamume anapaswa kufunga mdomo, kwani majibu mengi anayo mwanamke. Kwa wanaume ambao hawako tayari kuwasikiliza wanawake au kuwaacha wanawake kuwa wazungumzaji wakuu kwenye masuala ya nyumbani na familia, wanapata hasara kubwa. Ni hasara inayotokana na ukweli kwamba, wanaume wengi hawajui kitu kuhusu masuala ya nyumbani na familia kama wanavyojua wanawake.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nikiwa kama mwanamke nakubaliana na wewe 90%
   
 3. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ahh kwavile nina jinsia mbili BAS NINA FAIDA SANA cz ntabalance kotekote job n home
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,656
  Trophy Points: 280
  sina uhakika ya kuwa hatujui kitu kuhusiana na masuala ya kifamilia.......................bali nionacho mimi ni mgawanyo wa majukumu............ingawaje ni ukweli usiopingika...................a stable family is a source of a blissful marriage and more cash in the pockets of the insiders............
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,656
  Trophy Points: 280
  yaani wewe ni hermaphrodite..............................basi kweli huhitaji mtu maana unajipea mwenyewe na huna zengwe la kuhofu kuibiwa na wezi wabaya..........ila kuweza jikoni, nyumbani na nje ya hapo ...............yategemea vipaji alivyokupa Muumba kuna akina dada wengineo ambao hata kukaanga yai hawawezi hadi waliunguze tu........................mie mwaya naweza hata kutokosa maharagwe.............na kukaanga vitumbua angawaje nina bakora pekee yake.............................................lol
   
 6. delabuta

  delabuta Senior Member

  #6
  Sep 13, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukweli mtupu
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  lol,umenikumbuhsa mbali na kutokosa... ila hermophrodite jinsia zote hazifanyi kazi kwa wakati mmoja. so pengine anahitaji hermphrodite mwenzie,lol!
  mada ni ya ukweli. mwanaume anayefanikiwa sana kwenye mambo yote ni yule anayemsikiliza mkewe na hata mama yake pia (tusiwatenge wanaume na mama zao jamani). na mwanamke anaweza kukupa ushauri wa maana sio tu nyumbani,lakini hata kuhusu kazi yako.
  <br />
  <br />
   
 8. Twande

  Twande JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tusichanganye mambo mama anaingiaje tena jamani! Ndoa inawahusu wa2 mume na mke! Kilichoandikwa hapo juu ni ukweli mtupu! Watu wengine wamekuwa obsessed na issues za mama kias kwamba sometime wanaharibu wenyewe mahusiano ya mke na mama! Hawa wanaitaji heshi tofauti na hawachanganyiki! Mama muheshimu na kumfanyia atakacho kwake! Msikilize mkeo nyumbani kwako!
   
 9. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa mkuu, ila mie napenda pamoja kwamba mie ni muongeaji, kuna kauli za mwanaume zinatakiwa hapo, kwamba anakujibu mawazo yako ni mazuri tuyafanyie kazi, au hili baya tusifanye uking'ang'ania anakukumbusha kwamba yeye ni mwamuzi wa mwisho, inapendeza zaidi, pamoja huwa tuna maamuzi ya busara tusing'ang'anie kila usemacho kipite bila kupingwa
   
 10. Twande

  Twande JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yes Gaga mi nazani shida inakuja pale mwanamke ambae si mwelewa anamisuse kuckilizwa kwake anakuwa mwanaume! Mwanaume ni mwanaume jamani! Kuna mahali mwanaume lazima afanye nafasi yake so kumckiliza mke hakubadili uanaume wake! Wanaume nao wengine wanazania watakuwa si wanaume wakisikiliza wake zao! I like the way my man ananickiliza na namckiliza na akisema no badae naona umuhimu wa pale aliponiambia hapana!
   
 11. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ni kwel lakin nakubaliana na wewe kuwa mambo mengi ya kifamilia mwanamke anayajua kuliko mwanaume
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Gaga, sipingani na wewe, lakini kama umesoma between line, naamini nimegusia jambo hilo, sema tu ni kwa mkabala tofauti... wakati wewe umesema "Half empty" mimi nimesema "Half full"......kitu ni kile kile.....LOL.......
  Nilichosema ni kwamba,....... ngoja ninukuu hapo mahali...............'

  "wanawake siku zote ndiyo wenye nguvu kwenye kauli ya mwisho.Ndiyo maana ni rahisi hata kwa wanaume wakorofi kusikika wakisema, &#8216;nimeamua tufanye alivyotaka, ngoja mambo yaende vibaya, atanijua. Nimemwachia kusudi kama alivyotaka tufanye, lakini ataona mambo yakiharibika.' Mara nyingi, mwanamke ndiye anayesikilizwa." Mwisho wa kunukuu.......

  Nilichomaanisha ni kwamba hizo kauli za kusifiwa au kupongezwa kwa ushauri makini huwa kunafanywa na wanaume wengi, hasa baada ya kugundua kuwa wake zao wana busara katika kutanzua maswala yahusuyo familia kwa ujumla, na kama atapingana na ushauri wa mkewe mara nyingi hutumia kauli zenye busara na ambazo hazitamkwaza mkewe........ lakini hata pale atokeapo mwanaume mkorofi, mbishi, na mbabaishaji, hukubali lakini akiwa ameupokea ushauri wa mkewe kwa mtazamo hasi...........kwamba, "ngoja nifanye anavyotaka, ili mambo yakiharibika nimshikishe adabu"........ kitu ambacho mara nyingi hakitokei, labda kama atakusudia kisilete majibu mazuri kwa nia ya kutimiza malengo yake, ya kumkomoa mkewe.......... upo hapo?
   
 13. C

  Capitani Member

  #13
  Sep 13, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata viumbe wengine wote jinsia ya kike ni ndogo kuliko kimamwili kuliko ya kiume lakini jinsia ya kike ndio yenye jukumu la nyumbani nina maaana sehemu ya familia ya wanyama hao chunguza nautaona ni kweli kabisa . madume kazi yao ni kutoa ulinzi tu. maamuzi yote mazuri hutokkea kwa jinsia ya kike.
   
 14. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280

  hahahaha.....tehe tehe. Mnachekesha kweli. Wakiwa mahermophrodite wote, halafu ikatokea jinsia moja ndo inahitaji mambo yetu yaleeee, ngoma itakuwaje? Nahisi kila siku watakuwa wanagongana kimahitaji na hivyo hawatapata kufanya mambo yetu yale, na ngoma itakuwa droo.

  Wanachojivunia ni kukwepa maambukizi ya vvu kwa sexual relations tu.
   
Loading...