Acheni uvivu katika kutafuta elimu

KiuyaJibu

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
841
175
Ninasema hivyo ni kiwa na maana kuwa uelewa wa mambo mengi ni kitu muhimu sana kwa binadamu tena katika zama hizi za utandawazi.Watanzania wenzako,naomba tuwe na jitihada za kujifunza mambo tofauti ili tuweze kupambana na maisha ya kila siku.
Ukizingatia elimu ndiyo ufunguo wa maisha;basi ni vizuri tukawa na huo ufunguo ilituweze kutatua changamoto za kimaisha kama zinavyoibuka siku hadi siku hapa nchini na dunia kwa ujumla.
Kitu kingi ambacho kinapelekea mimi kuandika hii habari;nimegundua kuwa watanzania wengi ni wavivu wa kujisomea/hawa utamaduni wa kujisomea.Mara nyingi utaonana mtu anajisomea kwaajili ya usahili/mtihani.
Chukulia mfano mdogo tu ndani ya mbunge letu,ile sheria ya mafao ilipitishwa na wabunge katika bunge la mwezi March/April,2012.Taarifa zilipoanza kutolewa na SSRA(Social Security Regulatory Authority);baadhi ya watu wakagundua kuna kipengele cha umri wa miaka 55/60 ndiyo mtu anaruhusiwa kudai mafao yake.Wafanyakazi/wananchi wakaja juu kuona kuwa haiwatendei haki na wabunge wakaja juu pia na kuanza kuomba mwongozo baada ya kukiri kuwepo madhara hasi kwa wenye fedha zao.Jana Mr.Mbowe katika maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu akasema "mh.waziri mkuu sheria iliyotumika kulifungia gazeti la Mwana halisi kuwa ni sheria kandamiza na ulikwisha pigiwa kelele na vyombo vya habari kwasababu inavinyima uhuru vyombo vya habari pale vinapoandika habari zisizoifurahisha serikali na serikali inakuwa na nguvu za kukifungia chombo cha habari bila hata kukipa nafasi ya kujitetea;je,mh.waziri mkuu huoni kwamba ni sheria kandamiza katika nchi inayofuata demokrasia?Mh.akajibu kwa kusema,"sioni kama ina ubaya wowote katika utendaji wake,na kama mtu ameonewa anaruhusiwa kukata rufaa katika mahakama;na hata hivyo mh.spika sheria yenyewe imepitishwa na bunge lako tukufu na iataendelea kutumika mpaka pale mtakapo ileta hapa bungeni kwaajili ya marekebisho zaidi."
Hii inaonyesha jinsi gani hata wabunge wetu wanapopewa makablasha kwenda kuyasoma inaonyesha hawasomi/hawayaelewi ndiyo maana utaona wanapitisha vitu halafu baadaye vinakuja ku-back fire ndiyo utasikia naomba mwongozo wakati wangeweza kuzuia hali kama hizi zisijitokeze mapema.
Hebu angalia kiambatanisho hapa chini;kinaonyesha jinsi gani wenzetu walivyo serious katika kujifunza/kujua mambo.
 

Attachments

  • Sweep.jpg
    Sweep.jpg
    18.5 KB · Views: 57
Unachosema nakiunga mkono ingawa na mimi ni mmoja ya watu wasopenda kusoma but umetushauri jambo jema
 
Back
Top Bottom