Acheni kuifananisha Morogoro na vitu vya kijinga

Acheni kuifananisha Morogoro na vitu vya kijinga

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,204
Nyie mliofika Morogoro mjini na kusema kwamba vijana wa morogoro ni kama vijana wa Dar, eti ni wavivu mara wanywa supu ya pweza sijui goi goi sasa mkae mkijua kwamba Morogoro ni mji ambao una sehemu zake (vimji) vinavyojitegemea kama.

Morogoro mjini.
Kilosa.
Kilombero.
Mikumi.
Ifakara.
Gairo.
Mahenge .
Mvomero.
Malinyi

Na sehemu zingine Nyingi tu.

Zote ni sehemu zinazojitegemea na mtu akitoka kati ya sehemu mojawapo akitaka kwenda Morogoro mjini anasema na anapanga safari kwamba anaenda Morogoro kama nyie mnavyotoka mkoani na kuja moro yaani huwa hawajihesabii kama wako Morogoro.

Unaweza kumuuliza mtoto au kijana wa ifakara kwamba ulishawahi kufika Morogoro kama bado atakwambia bado sijafika Morogoro na wakati huo huo yuko ndani ya mkoa wa Morogoro.

Huko nilikotaja ukiachana na Morogoro mjini ndio utakutana na wana Morogoro halisi wachapa kazi.

Mfano ukienda Kilombero utakutana na mashamba ya miwa hekta kibao unafikiri wanalima wakinanani kama sio wanamoro wangekuwa wavivu ungeona ile miwa na kununua sukari yao KILOMBERO SUGAR.

Ukienda Ifakara, Lupiro mpaka Malinyi huko kuna bonde la mpunga hekta kibao unafikiri wanalima wakina nani kama siyo wanamoro wangekuwa wavivu ungeona mpunga unalimwa.

Acheni kuisema Morogoro nyie mmefika hapo tu mjini ambapo asilimia kubwa ya vijana wanafanya changes na vijana wa Dar.

Vijana wa Morogoro wanatoka jioni wanaenda kula bata Dar hivyo hivyo vijana wa Dar wanatoka wanakuja kula bata Morogoro mjini.

Siku inayofuata kila mtu anarudi kwenye mji wake. Nyie hamjafika Morogoro ila mmefika part ya Morogoro kwa hiyo msiipakazie Morogoro nzima.

Tafuteni watu wawatembeze Morogoro yote muone maajabu yake na niwaambie tu itakuwa tour itakayochukua mpaka mwezi mzima ili muweze kuimaliza Morogoro yote.
 
Hata mtu akiwa dumila anasema naenda morogoro. Morogoro sio mchezo ni kubwa hasa yenye kila aina ya hali ya hewa. Ukiwa gairo utadhani upo Dom. Ukiwa lumuma kama upo iringa ukija mikese kama upo pwani. Moro ndio kila kitu tz wengine wote mafisi. Mkoa unazalisha mazao yote unayoyajua wewe. Kuna minazi mpaka miparachichi. Mkuu wa mkoa wa kwanza Moro ni nyerere hata mara huko haijawahi tokea. Wajanja wote wapo Moro. Ukitoka mji mkubwa kwenda mji mkuu lazima upite Moro.
 
moro bado Local sana!! Full vigodoro kama Kilwa tuu !!
Labda usema panafaa kwa kilimo ila sio kula bata!
 
advance nimesoma moro......wilaya flani hivi.

nimewala sana wadada wa huko, hawajui kukataa, unamla bure bila hata senti, tena unaenda kwake unakuta kachinja na kuku kabisa unapiga supu kwanza....

shule yetu ilikuwa bording, kwa hiyo tukienda mtaan wadada walikuwa wanatuthamini sana, pia walituweka kwenye class flan hivi ni ngum kukukataa...

Mungu saidia, nimefanya uhuni sana moro....

sifa kuu ya moro, wakarimu , alafu kule kuna vitu vingi maisha sio magumu sana, changamoto ni maji yao tu full typhoid.
 
Moro ni upcoming city...
Haiwezi kutokea morogoro ukawa mji wa kuvutia hata siku moja, mvuto wa jiji ni tall towers-sasa nyie na mizinga hiyo mtawezaje kunyanyua mijengo ya maana na mirefu mkuu?
Moro itabaki kuwa na Nyumba fupi fupi tu kama waruguru walivyo,samahani lkn maana ukweli unauma.
😛 😛 😛 😛 😛
 
Hata mtu akiwa dumila anasema naenda morogoro. Morogoro sio mchezo ni kubwa hasa yenye kila aina ya hali ya hewa. Ukiwa gairo utadhani upo Dom. Ukiwa lumuma kama upo iringa ukija mikese kama upo pwani. Moro ndio kila kitu tz wengine wote mafisi. Mkoa unazalisha mazao yote unayoyajua wewe. Kuna minazi mpaka miparachichi. Mkuu wa mkoa wa kwanza Moro ni nyerere hata mara huko haijawahi tokea. Wajanja wote wapo Moro. Ukitoka mji mkubwa kwenda mji mkuu lazima upite Moro.
Wewe kweli kiboko,
Hadi lumuma unaoafahamu ?
Huko ni mwishi wa dunia
 
Back
Top Bottom