Unajihakikishia VIP kwamba marekani wametoa 800mil kwa ajili ya bajeti wakati kwenye vitabu vya revenue volume 1 vya wabunge kina ZERO MONEY? porojo time
saf kk kwa ufafanuz wakoIsaya mp,
Unaelewa maana ya 'Bilateral' assistance? Labda nikuelimishe kidogo.
Serikali ya Tanzania hupokea misaada kupitia njia kuu tatu:
1. General Budget Support (GBS), fedha hutolewa moja kwa moja kuchangia bajeti ya serikali
2. Basket Fund, wafadhili kadhaa (i.e. zaidi ya nchi moja) huchangia mradi kwa pamoja
3. Project Fund, Mfadhili analipia miradi moja kwa moja.
Njia 1 & 2 fedha huwa hazipitii hazina hivyo mara nyingi huwezi kuziona kwenye bajeti ya serikali kama ilivyo kwa option ya kwanza (GBS). Serikali hupendelea hela zote zipitia hazina lakini kuna wafadhili ambao wanapendelea kwenda kivyao na kulipia miradi moja kwa moja.
Kwa historia, Marekani hutumia options 1 & 2 na sio kutoa hela moja kwa moja Hazina, ndio sababu unasikia miradi imefadhiliwa na USAID. Sasa ufadhili huu wa nchi moja kama ilivyo kwa Marekani na Tanzania ndio unaitwa 'Bilateral assistance' maana ni makubaliano yake yeye Mmarekani peke yake na Tanzania na sio kutoa hela akaweka kwenye kapu na wengine (Multilateral).
Baaada ya maelezo hayo unaweza sasa kuendelea na ngonjera zako.