Acha kushangaa huu ndo ukweli

Lutala

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
848
103
Unashangaa nini matokeo kupinduliwa?

Mosi, Chama chenyewe ni cha MAPINDUZI, kwa hiyo kupindua matokeo si jambo la ajabu.
Pili, Viongozi wake wote wa juu ni Wanajeshi

Mwenyekiti: Luteni Kanali Jakaya Kikwete
Katibu Mkuu: Luteni Yusuf Makamba
Naibu Katibu Mkuu: Kapteni George Mkuchika
Katibu wa Itikadi/Uenezi: Kapteni john Chiligati
Meneja Kampeni: Kanali Abdulrahaman Kinana

Tatu, Gazeti la Serikali, Daily News ambalo editor in Chief ni Rais, limeshasema: Dk. Slaa hatakuwa rais wa tano wa Tanzania

Nne: Tamko la Luteni Jenerali Shimbo linajieleza: "Wagombea wakubali matokeo, la sivyo..."

Tano: Katiba ya nchi/ sheria ya uchaguzi iko wazi: Matokeo ya urais yakishatangazwa, hakuna chombo chochote kinachoweza kuyapinga.

Sasa mnashangaa nini eti mnajidanganya bila kujua kuwa nchi hii ni ya utawala wa kijeshi.

Haya nendeni mkapige kura kutimiza haki yenu ya kikatiba, narudia tena kutimiza haki yenu ya kikatiba.
 
Kweli kabisa!hiki ni chama cha wanajeshi,mimi nilikuwa sijashitukia kabisa!Ndiyo maana waliamua kiingilia kati walipoona kinaweza kupoteza serikali!
 
Una hoja broda!
Lakini pia kumbuka wajeshi wote wa ngazi za juu za majeshi yetu ni wanaCCM hai!
Kwahiyo upinduaji kura ni jambo lisiloepukika!
 
Una hoja broda!
Lakini pia kumbuka wajeshi wote wa ngazi za juu za majeshi yetu ni wanaCCM hai!
Kwahiyo upinduaji kura ni jambo lisiloepukika!

Ndo kazi yao miaka nenda rudi ya kupindua kura
 
Historia haisemi kuwa kuna jeshi duniani lilowahi kushinda nguvu ya UMMA.Msidanganyike na nyakati za 1995,2000 na 2005, hii ni 2010 asilimia 50% ya wapiga kula wamebalehe na kuvunja ungo katika kipindi cha mfumo wa vyama vingi wamekua wakishuhudia machufuko zanzibar wakati wa uchaguzi na kwingineko duniani, wameshuhudia kila mara mabomu yakipigwa kutawanya watu na pia wamekulia dunia ya dot.com wanaona yanayotokea duniani.Hao wanajeshi wasijidanganye, wapiga kura wa mwaka 2010 wana uelewa naujasiri tofauti na wa nyuma.Na pia kumbukeni hawa ni vijana waliokaa tangu wamalize std seven, form iv na formVI na wachache wenye degrees wengi kati ya hao;
  • hawana kazi, wanashinda wakilanda landa mitaani
  • Hawajaoa
  • Hawana majukumu ya kifamilia
  • Hawana watoto
  • wako tayari kulinda kura usiku kucha na kuwa tayari kupambana inapobidi
  • Wanasubilia ajira kwa matarajio iko siku watatoka
Hawa wote hawaoni kigeni ukiongelea kupambana na jeshi la hao maofisa uliowataja


Kazi kwenu mnaojipa moyo wa kuiba kura
 
pia wakuu wote wa mikoa na wilaya kama sio wanajeshi wastaafu basi ni usalama wa taifa.hebu fikiria
 
Alikuwepo Sauli aliyeamua kuupinga uamuzi sahihi wa Mungu kuchaguliwa Daud awe Mfalme akamfukuza kila sehem wakati ni yeye aliyesaidia kumuuwa Goliat jitu lenye ft 9 urefu, akaokoa taifa lake, lkn hakuona hilo, ni Slaa aliyewezesha kuwataja mafisadi hata wengine kurudisha kiasi fulani cha pesa lkn wanamuona kama fisadi, nawaambia kuwa mwaka wa kufa nyani miti yote inateleza, hata kama watatumia Mgabeism, lkn haki ni maji mengi na CHANGES IS MUST. Watahadaa wachache lkn wengi watafanya watakalo siku inakuja nayo inafanya haraka sn.
Mungu iponye TZ Mungu waponye wote wenyekupigania haki ya watu wako.
Mungu mlinde Rais Slaa, mpe maisha mema kwafaida ya vizazi vijavyo.
Amen.
 
Dr Slaa alitaja list of shame, hao wanajeshi walikuwa wapi wasimshughulie.

Mimi nimejiandaa kuwalipua wote watakaoshiriki katika kuchakachua matokeo.
 
Hakina sifa ya kuitwa chama cha siasa, ni chama cha kijeshi ndiyo maana wameanzisha jeshi lao la Mungiki (green Guard)

Kweli kabisa!hiki ni chama cha wanajeshi,mimi nilikuwa sijashitukia kabisa!Ndiyo maana waliamua kiingilia kati walipoona kinaweza kupoteza serikali!
 
nasikitikia sana tanzania yangu,naomba mungu mwaka huu uwe wa mwisho kutawaliwa na hawa wajeda
 
Back
Top Bottom