Blank page
JF-Expert Member
- May 28, 2015
- 6,179
- 6,348
dah mmeniacha wakuu.
Miaka ya 1970s kununua Gari lazima muwe Watu wasiopungua Sita kupata Kibali
Dkt Hassy Kitine Mkuu wa Usalama wa Taifa kabla ya Balozi Augustine Mahiga alitumbuliwa kwa kosa la kununua Gari binafsi bila ya kumjulisha Mwl Myerere
Hata kununua Fridge ya kupoza Maji ilikuwa ni uhujumu Uchumi!
Watu tulikuwa tunavaa Kama Sare za Shule kwa kuwa hapakuwa na Mitumba wala Nguo za kutoka Nje ya Nchi
Ile Minguo ya Urafiki ikizalishwa kwa wingi Kama Uniform zikiingizwa Sokoni huna option zaid ya kununua
Sitamani zile enzi kwa kweli!, kilikuwa kipindi cha Ujima au Zama za Mawe za Kale!
Bwana Magu kaamua kugeuza Gari kuturudisha zile enzi
Acha hizo wala rushwa na wahujumu Nyerere hakuwabeba. Wapenda haki waliishi
Zamani magorofani Ilala pale kila baba alikuwa na gari. Kulikuwa na datsun, volswagen kobe na kombi, ford cortina na escort. Kulikuwa na land cruiser, landrover na range rover. Mikebe ya benzi za zamani. Pijo ndio usiseme. Teksi zote ni 404. Washua walikuwa na 204, 304, 404 na 504 kwa mabishoo wa mji. Halafu 404 na datsun zilikuwa na pick up zake. Weweee
Kwa wasio na magari. UDA ilinguruma kila dakika tano. Hii nchi ilikuwa sambamba na ulaya kwenye miaka ya sabini. Mitaa ilikuwa misafi na nyumba za mpangilio. Tizama nyumba za kota Ilala au za CDA Dodoma.
Sijui tulipotea stepu wapi!
Ni kweli huu mkate wa siha ulikuwa ni mkate bora kuwahi kutokea. Tangu kufa kwa National Milling na mkate nao ukafa. Dhana yangu ni kuwa wapo baadhi ya wafanyakazi wanakumbuka fomula ya kutengeneza huu mkate, tunaomba wajitokeze waturudishi huu mkate.
Halafu kulikuwa na mkate wa boflo...![]()
Mkate laini kama sufi. Sio siri Bongo ya zamani ilikuwa raha sana hata jua lilikuwa halina usongo na ukali kama hivi sasa.
Halafu hizi kelele za vyama vingi pia hazikuwepo. Wazee wetu walifanya kazi au biashara waliyamudu maisha. Walikuwa na magari na nyumba.
Maisha swafi. Sio kila mtu mwizi wenye wanaita kupiga dili.