ACACIA wapunguza wafanyakazi 1,200

ACACIA wapunguza wafanyakazi 1,200

Nashangaa serikali hii kusababisha maelfu ya watu kupoteza ajira ACACIA bulyahkulu ? Only for a political mission!?
Ndio tayari tena mkuu , tutachimba wenyewe kwa machepeo , tutatengenezea shanga ili tuuziane , maana iko wazi sokoni tutapigwa ban.
 
One of the strategy to make government softens it's hard decisions...Uwongo wao upo wazi Kabisaa... Kama walidai makinikia haina Zahabu kiasi tunachodai Kwanini wadai wanapata hasara Kwa percent hiyo kubwa kiasi cha kuathiri uzalishaji?
Yes... Let's prepare for even worse kama tu itamanisha tutachomoka kwenye huu unyonyaji wa mali zetu za urithi...
 
Una uhakika..nenda buzwagi ukaone barrick wamekuachia nini na faida iliyopatikana kwa wenyeji wa hapo na nchi..kisha uje kasi huku kama nyumbu aliyekoswa koswa na mamba
Na kusema ukweli hii ndiyo definition ya wao kutopata faida... Wali vuna dhahabu Kwa muda mfupi Kwa gharama kubwa ili wahamishe utajiri haraka kukwepa uncertain future... Wamecheza Na non-renewable exploitation model wakachagua shorter path na ili wasipate hasara wakaingiza garama zote kwenye mikataba
 
"Wasitutishe..wao ndo watishike"- JPM


Sasa sijui wanaotishika ni kina nani hapa...

Kesho maelufu wanabaki home kutizamana na wake zao nyumbani..
 
Nimesikia mitambo mengine wanaondoa Isiwe ikawa kama watatakiwa kulipa basi tusiwe na chakubaki nacho kama tulivyo taifisha almasi.... Mungu wewe upo pamoja nasi nami naamini hutatuacha kamwe!
 
Mzungu anaenda kusalimia familia yake anaacha kafunga mgodi na kufurumusha maelfu ya vijana na serikali inatizama tu, hapa kuna tatizo.
 
Hiyo heading duuh! Ungeandika kiswahili. Halafu hata haiweleki. Maana hata kama ulimaanisha "can a government layoff thousands of people." Haihusiani na Acacia
 
Hakuna MUWEKEZWAJI ambae haibiwi, lakini wanajaribu kuangalia faida nyingine nje ya kodi, kumbuka faida ya mradi sio kodi tu, ndio maana baadhi ya serikali zinawasaidia wawekezaji wakubwa hata kwa kuwapa ruzuku!!! Ili viwanda visifilisike, tuache kuwaza kodi tuuuuu
 
Hakuna MUWEKEZWAJI ambae haibiwi, lakini wanajaribu kuangalia faida nyingine nje ya kodi, kumbuka faida ya mradi sio kodi tu, ndio maana baadhi ya serikali zinawasaidia wawekezaji wakubwa hata kwa kuwapa ruzuku!!! Ili viwanda visifilisike, tuache kuwaza kodi tuuuuu
HATUNA UWEZO WA KUWA NA UWEKEZAJI ASIYEWEZA AU KUTUIBIA KTK KULIPA KODI MPAKA BAADAE. HIVI HUE!EWI WAKULIMA WOTE ULAYA WANA PESA WANAPEWA NA SERIKALI ILI WAENDE?EZE KILIMO MAANA NI HASARA? HII HUSAIDIA KTK AJIRA PIA KUWA NA USALAMA WA CHAKULA.
 
KAMPUNI ya uchimbaji madini ya Acacia, imekamilisha hatua za kusitisha shughuli za uchimbaji katika mgodi wa Bulyanhulu uliopo Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kwa kupunguza wafanyakazi wake 1,200, wakandarasi 800 na kubakia na 200 pekee.

Jana jioni uongozi wa mgodi huo uliandaa sherehe kuwaaga wafanyakazi wake waliopunguzwa kazi ikiwa ni hatua ya mwisho ya ufungaji mgodi huo.

Taarifa ya kampuni hiyo iliyotumwa juzi kwa gazeti hili, inaeleza kuwa wamefikia uamuzi wa kufunga mgodi huo kutokana na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji mara baada ya zuio la usafirishaji wa mchanga wa madini (Makinikia).

Acacia ilieleza kuwa tangu kuwekwa zuio la usafirishaji wa makinikia nje ya nchi, uzalishaji wa mgodi huo uliathirika kwa asilimia 35 kwa sababu ya kukumbwa na tatizo la ongezeko la hifadhi ya makinikia yenye thamani ya takribani Dola za Marekani milioni 265 sawa na Sh bilioni 590.

Taarifa hiyo ilifafanua kwamba mgodi huo utafungwa na kubaki na wafanyakazi wachache ambao watakuwa na jukumu la utunzaji wa mali zote zisizohamishika na mitambo, ili kuwezesha mgodi huo kurejea katika utendaji wa kawaida hapo baadaye pindi zuio la usafirishaji makinikia litakapoondolewa na mazingira ya biashara kutulia.

“Kwa sasa shughuli za uchimbaji wa chini ya ardhi na uchenjuaji wa miamba utasitishwa pamoja na usafishaji wa mashapo ambao umesitishwa kwa muda ili kupisha zoezi la kuhifadhi maji kutokana na hali ya ukame,” ilieleza taarifa ya Acacia.

Ilibainisha kwamba kwa sasa usafishaji wa mashapo uliositishwa unatarajiwa kuendelea Oktoba baada ya mvua za kutosha kunyesha. Watazalisha kwa kiwango cha kati ya wakia 30 hadi 35,000 kwa mwaka huku shughuli za uchimbaji chini ya ardhi zikiendelea kusitishwa.

Ilielezwa kuwa Acacia inaamini kuwa majadiliano kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yanayoendelea yatakuwa yenye ufumbuzi na kusisitiza kuwa majadiliano hayo ndiyo njia bora zaidi kwa pande zote zinazohusika kumaliza tofauti iliyojitokeza.


Wafanyakazi wanena
Akizungumzia hatua hiyo, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Migodini (NUMET), Nicomedes Kajungu, alisema tayari wamekutana na uongozi wa Acacia katika vikao viwili na kukubaliana kupunguzwa kwa wafanyakazi hao kutokana na uongozi wa mgodi huo kuamua kusitisha uzalishaji.

Kajungu alisema kwa sasa wanasubiri kikao kingine kujadiliana namna ya kuwalipa wafanyakazi wake 1,200 ambao watapunguzwa kazi na kuiomba Serikali kumaliza mgogoro wake na Acacia kwa kuwa idadi ya wafanyakazi wanaoathirika ni kubwa na ina athari kwa uchumi na ustawi wa maisha ya kila mmoja.

“Kusitishwa kwa shughuli za mgodi huu, kuna athari kubwa kwani utaathiri mauzo ya saruji ambapo mgodi huo ulikuwa ukilipa Dola za Marekani milioni 40, walikuwa wakilipa dola 25 za gharama za umeme, lakini walikuwa wachangiaji wa mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hale kwa asilimia 60 na Halmashauri ya Msalala asilimia 70,”

CHANZO: Mtanzania
Tuko radhi kula majani, kuliko kuibiwa.Waondoke tu,tutachimba hata baada ya miaka 200 kama tutakuwepo bado.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ni mwendawazimu pekee anayeweza kufurahia kupotea kwa uwekezaji. Awamu hii kazi yake kubwa ni kuua hata uwekezaji mdogo ulikokuwa umefanywa na awamu zilizotangulia.

Hakuna muujiza wa nchi kupiga hatua katika maendeleo bila ya uwekezaji, na hasa uwekezaji mkubwa. Mpaka sasa tangu awamu hii iingie uwekezaji umeshuka toka 26.8% mpaka 3.4%. Hivi kama hakuna uwekezaji, hata hawa vijana wetu waliopo mashuleni na vyuoni, baada ya kumaliza wataenda wapi?
 
Tuko radhi kula majani, kuliko kuibiwa.Waondoke tu,tutachimba hata baada ya miaka 200 kama tutakuwepo bado.

Tunaibiwa nini? Anayewadanganya amejua kuwa nyote ni wajinga, anawalisha kila atakalo, na ninyi kwa ujinga mnameza kama mnavyolishwa. Mbona kodi zote kwenye madini zinalingana na mataifa mengine? Mbona baadhi ya nchi kodi zao ni za chini kuliko za kwetu kwenye madini, na hakuna hizo kelele za kuibiwa?
 
Tunaibiwa nini? Anayewadanganya amejua kuwa nyote ni wajinga, anawalisha kila atakalo, na ninyi kwa ujinga mnameza kama mnavyolishwa. Mbona kodi zote kwenye madini zinalingana na mataifa mengine? Mbona baadhi ya nchi kodi zao ni za chini kuliko za kwetu kwenye madini, na hakuna hizo kelele za kuibiwa?
Mkuu hatuibiwi kwenye madini tu,ni kila sehemu.Tafuta kitabu alichoandika Walter Rodney kinachoitwa "How Europe Underdeveloped Africa," kama una roho ndogo utalia.Ina uma mkuu.Sijui kwa nini mnaendelea kukataa ukweli huu,ni kama mtu anayekataa Holocaust hivi.Utajiri wao unatoka kwetu mkuu,they are thieves,sio siri.
 
Acha mawazo mgando, nchi yenye ardhi kubwa, si wakakamate jembe na chaki za kufundishia wanafunzi? Usije niambia wewe utakuwa na familia kwa lia lia huku!
 
Mkuu hatuibiwi kwenye madini tu,ni kila sehemu.Tafuta kitabu alichoandika Walter Rodney kinachoitwa "How Europe Underdeveloped Africa," kama una roho ndogo utalia.Ina uma mkuu.Sijui kwa nini mnaendelea kukataa ukweli huu,ni kama mtu anayekataa Holocaust hivi.Utajiri wao unatoka kwetu mkuu,they are thieves,sio siri.
Toa pumba pumbavu weee. Kwani mliokuwa mkipiga kelele sio ndo nyie. Akili za makalioni zimejaa mavi
 
Back
Top Bottom