Tetesi: Acacia keleta Askari Wazungu/Mamluki

Ndugu MOP, tafadhali rejea post namba #42 na urekebishe "quotation" manake hapo ndio unavyoweza kupotosha ulichosema na nilichokisema. Asante
 
Mitale, Sijawahi kusikia mgambo wanalinda "...people and assets..." kwa kutumia lugha kama hii "...in the best possible way..." Kufikia hapo tayari kuwa hao waliopo hawana uwezo huo. period Ya kuwalinda in the best posible way

Ina maana hatuhitaji askari wetu wapolisi au jeshi wawe na silaha za moto kulinda mali na watu wake? au unaweza kunisahihisha

Sijasema hakutakuwa na usalama mtaani, ila nafikiria kama, na hii ni kama tu, kama wataajiri mamluki itakuwa ina maana hawana confidence na vyombo vyetu vya Usalama. Na kama sivyo hivyo, na hao wamefundishwa kwa sheria za kimataifa za kiusalama, kwa nini uwaajiri G4s? oooh "outsourcing" just another legal business practise!

Nahili linanisumbua kwani baada ya kuniibia, unanitukana kwa namna moja au nyingine kuwa sina uwezo wa kujua hili au kuendesha uchunguzi by kutaka an "independent inquiry" na kuongeza chumvi kuwa hata majeshi ya nchi yangu hayana uwezo wa kukulinda na mali "zetu"?
Sisi tunaweza kulinda popote pale tunapotaka. Muda wowote Bila kuzuiwa na mtu yoyote mkuu...
Hapa tunazungumzia nadhani askari waajiriwa wa acacia sio hawa wetu military au police forces.
 
Katika kile ambacho kinazungumziwa na "Wanasheria" sasa wazungu kuletwa Kulinda mali na wafanyakazi(wazungu) wa Accacia

Kwa udadisi mfupi niliyofanya baada ya Accacia kutoa matamshi haya, "We have decided to outsource our security staff, because we believe that by doing so our people and assets will be protected in the best possible way" hayo yalisemwa na Meneja wa mawasiliano ya umma Nectar Foya wa Accacia.

Maoni yangu ni kuwa Vita hii bado itaendelea. Walakini, Kuna umuhimu wa bunge au vyombo vikuu vya serikali kuingilia haya tusije tukawa kama Ivory coast, au Angola.

Vivyohivyo, "Haingii akilini" kuwa hata ndani ya mikataba hiyo kunaruhusu kuleta Askari kutoka nje ili kuwalinda "wazungu" na mali "zetu" What a shame!

"Haiingii akilini" kuona jinsi hawa watu wachache( Uongozi wa Accaia Tanzania) wanavyoweza kuvunja heshima ya majeshi ya ulinzi wa Tanzania.

Kuna ulazima wa kuungana katika vita hii #TZ-Nomercenariesforourgold
Sasa tatizo lipo wapi!!!....migodi hii hawajaweka hela kidogo wana haki ya kuwa na ulinzi madhubuti maana kwa sasa wao wanajiona kama wanaonewa na labda serikali wnaweza shirikiana na wananchi/wafanyakazi katika kuwahujumu zaidi
 
Hamna tatizo mkuu...Jukwaa la JF ni huru kwa mtu yeyote aliyesajiliwa kucomment kwa hiyo ni kawaida tu...Hamna tatizo, sio lazima kuwahi kila mahali
Ila wewe jamaa muungwana Sana ila Upo faster sana Mkuu nipe siri yako
 
Vita hivi havitaacha mtu salama.
Hata walete drones....Kuibiwa ni mwisho...kodi halali lazima ilipwe...na kilichoibwa kirejeshwe
Kodi halali ni ipi, si tunapewa tulichokubaliana, au ndo ganzi inawaisha. Labda muwashtaki kwa udanganyifu kama itathibitika pasi na shaka yoyote. Ndo malipo ya tamaa, ubinafsi, uchoyo na kutaka kujilimbikizia mali kati ya maskini mamilioni waliowachagua (kama ni kweli). Unalimbikiza mali ambazomutazitumia mpaka unakufa.
 
Hapo ndipo najilaumu huyu mtu alichelewa wap? Na najua amezoa confidence ya kutosha na tecniques za kukwepa mishale dhidi ya hawa wezi wa ulaya toka kwa mzee poo wa kagame.
Nchi ina adab sasa hivi walau
Samaki wa Magufuli walitufanyaje? Au umesahau mkuu. Mtu mzima awezi badili tabia yake kirahisi. Tusubiri tuone na Mungu amtangulie.
 
Magu akifukua makabur imekula kwake.
Waliomtangulia walisha haribu toka mwanzo.
Yeye ahakikishe ananyoosha mambo asijefanya madudu kama walomtangulia.

Mkataba ni makubaliano baina ya pande mbili kisheria.
Atakae kiuka hizi sheria atashitakiwa. Plz Magu angalie usijetengeneza zimbabwe ya pili! Mwenzio Mugabe alijaribu kufuta mikataba ya kikolon ... unajua kilichomkuta
 
Mie nipo upande wa accacia ? Why mliwapa wenyewe sasa mnalia lia vita hii lazima fisi watoke madarakani
Mijitu mingine bwana eti mi niko upande wa accacia alafu linaweka alama ya kuuliza.sasa unamuuliza nani?nenda na accacia wako.
 
Mie nipo upande wa accacia ? Why mliwapa wenyewe sasa mnalia lia vita hii lazima fisi watoke madarakani
Mkuu ni kweli una uhuru wa kukaa upande wowote.... Inauma sana awajamaa walio uza mali zetu ovyo ovyo kwa tamaa zao....

Lakini je waendelee kutuibia tu?
Makosa yameshatokea aina haja ya kulaumiana, Ni bora tuchukue tu hatua ili rasilimali zetu zitufaidishe sisi na Vizazi vyetu....!

Ni kweli vita hii inaweza kumtoa fisi madarakani lakini unazan ata akija simba ataweza kubadil mikataba? Nae akileta fyoko fyoko watamtoa tu! Nafikiri ata Fisi Mkuu analijua ilo ila kajitolea roho na mwili kupigana tofauti nafis wenzie.....

Tusiweke usimba na Uyanga katika hili tujumuike pamoja tupambanie Taifa letu
 
ila acacia waombe "mungu wao" tukose ushahidi beyond reasonable doubt walikua wanachezea "numbers" intentionally juu ya viwango halisi vya madini kwenye mchanga vinginevyo itawala pakubwa mnooo. navoelewa hakuna kitu wazungu wanachukia kama makampuni yao kujihusisha au kuonekana wamejihusisha na "udanganyifu" na ukwepaji kodi na possibly hisa za hawa raia zaweza kuhit record low baada ya hii report ya pili sasa tu cha msingi "the man himself" atembee nao mdogo mdogo tu awashitaki kwa nchi zao wawashinikize kulipa hasara tulopata miaka yote then hii isaidie kuweka grounds za kui review hii mikataba yote (kuivunja haraka inaweza kututia kwenye matatizo).. wala hata asiwaendee kwa jazba asije kujikuta ameenda kinyume na mikataba kidogo wakapata upenyo wa kuipona hii "roba ya mbao" ambayo so far ameipanga vizuri kwenye shingo ya hawa jamaa. na +255 itamkumbuka kwa mengi, hilo likiwa mojawapo kubwa sana..
 
Kwenye mikabataba statement ikitofautiana unaweza kuvunja mkataba na kama wameleta askari tupeleke wa kwetu pia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom