Amewataka waandishi wa gazeti wanaobakia waendelee kufanya kazi kwa bidii, kwa ajili ya kulikomboa taifa kwa kuuanika ukweli pasipo kuogopa,
Kazi ipo,Kibanda anaenda kuajiriwa kwa Bashe, sasa ataanza kuwasafisha mafisadi. Ngoja tuone atakuwa na mpya gani.
"Tukiwakamata Mafisadi, Uchumi wa nchi yetu utayumba".....Mizengo Kayanza Peter Pinda, Bungeni 2011
Hawawezi mkuu labda iwe ni mkakati wa kambi yao.Pengine mkakati wa kumshughulikia Mbunge wa mtama na kiongozi ajaye wa upinzani (baada ya uchaguzi mkuu 2015)Sasa huko alikoenda kuna changamoto gani?Nchi yetu hii tamu kweli kweli! Nataka nione zile makala motomoto za kuichachafya serikali na CCM zikitoka kwenye magazeti ya New Habari! Ndugu Mwita Maranya yametia yaliyonenwa na manabii
Kweli kazi ya uandishi wa habari Tanzania haina tofauti na uuza baa. Jamani Kibanda kama aliyokuwa akiandika yalikuwa yanatoka moyoni, huko ataandika nini au ni wale wale akina Salva Rweyemamu. Kweli namna hii hatuwezi kuendeleza nchi yetu. Yaani kila mtu anapigwa bei kienyeji hivi hivi.
Aliyekuwa mhariri mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda, leo ameaga rasmi na kuachia nafasi yake mhariri mtendaji, kwa maelezo kuwa anaenda kujiunga na kampuni ya New Habari Corporation 2006, inayochapisha zaidi ya magazeti manne hapa nchini.
Akiongea na wafanyakazi wa gazeti la Tanzania Daima leo asubuhi, kibanda alisema sababu kubwa ya kuondoka hapo ni kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya katika majukumu yake ya uandishi.
Amewataka waandishi wa gazeti wanaobakia waendelee kufanya kazi kwa bidii, kwa ajili ya kulikomboa taifa kwa kuuanika ukweli pasipo kuogopa,