Abood Bus Service this is too much!

Kwenye mabasi ya Abood kuna utaratibu wa kwamba zile siti za pale mbele (wenyewe wanziita 61 na 62) na pale jirani na dereva kuna watu wanakaaga ambao hesabu yao anaichukua dreva na utingo (labda kuna officials wengine pia wamo kwenye mgao). Wakati mwingine mpaka watu wanasimama bila shida yoyote.

Kwenye hayo makundi ndio utawakuta hao wezi, na inarahisishwa na utaratibu wa kushuka shuka njiani.
 
Dar to Moro tumieni BM hayo magari ya Abood situmii hata Kwa ngumi
 
Ndio maana wezi huku kitaa tunawatia kibiriti! Sasa mtu aibe vyeti usawa huu harafu akatupe duh,nakuotesha mkia.
 
Mandieta-utakuwa mpambe wa Abood wewe siyo bure.!!

ulijuajeeee mkuu! mijitu kama hiyo wapo wapambe tu huyo atakuwa katokea msamvu moro....maana huwezi tetea ujinga kama huo
 

Wewe wacha kutumika nia yako ni kulichafua basi pendwa la ABOOD kwani hilo basi la A BOOD linakwenda route gani na hayo ni kampuni mbili tofauti ABOOD BUS na uchafu wako wa A BOOD
 
pole sana. Hili ndio basi nilikuwa nikiliamini kwa usafiri wa moro dar.

wajirekebishe watapoteza wateja.
 
Kwa nini hujaripoti tukio hilo la uhalifu Polisi?

Au umekata tamaa, kutokana na mfumo wa utawala wa nchi hii, kwa kuwa mmiliki wake ni mheshimiwa Mbunge, tena kupitia chama tawala, kwa hiyo unajua wazi kuwa, lazima Polisi watakua wanamgwaya?

Hebu jaribu kuimagine, watu wa design hiyo ya akina Abood na Shabiby, pamoja na kuwa ni wafanyibiashara wakubwa sana wa usafirishaji wa mabasi, lakini bado waliusaka Ubunge kwa njia zote, hadi wakaupata.

Sasa unategemea huyo mmiliki,atarejesha vipi hayo mapesa mengi,aliyoinvest kwenye ubunge, inawezekana ni pamoja na 'kuwaagiza' wafanyi kazi wake, wa mabasi hayo, 'kuzilamba' laptop zote zinazokaa, kihasarahasara, ili zipigwe bei, angalau, zirejeshe nusu ya hasara, iliyopatikana, wakati wa kuusaka, uheshimiwa ubunge!!
 
Aisee hayo mabasi bwana hata kuna dokta wangu mmoja aliibiwa kila kitu....
 
Watanzania tuache kulialia kama watoto wadogo, yaani unaibiwa mzigo ndani ya Basi halafu unamlaumu mwenye Basi.!?

Hivi wakati unaingia ndani hukuona tangazo "ABIRIA CHUNGA MZIGO WAKO WA NDANI",aulimkabidhi Konda.?
Ndani ya Basi kwenye keria kunakua na mzigo midomidogo mingapi hadi konda aweze kuilinda yote.?

Tuache kudeka vitu vingine tuwe tunajiongoza wenyewe sio kila kitu kusimamiwa tu.
 

mkuu tiari nilishaenda police kitambo.
 
Kwann unasafiri na vyeti orijino?
Kwenye usafir wa public???
Tembea na photokopi mkuu
 
Huwa nikisafiri kama sio rasket basi mizigo yote inawekwa chini kama ni rasket basi naipakata hadi mwisho
 
hahahahaa,,,mdau kama zipu mbovu,,,ikifungukia ndan ya bas je?

sasa inabidi ufanye designing ambayo zipu haitafunguka kirahisi, unaweza hata ukaweka vikofuli vidogo lengo ni mwizi aliibe aondoke nalo, atakapo fungua tu, mpaka mdaula watakoma
 
Huwa nikisafiri kama sio rasket basi mizigo yote inawekwa chini kama ni rasket basi naipakata hadi mwisho
Same to me,nilikua na safar ya Lindi,nimekumbatia rasket yangu na laptop bag mpaka nafika
 
Wakuu wote mliokumbwa na janga la janga la kuibiwa katika mabasi ya abood nadhani ufumbuzi umepatikana ... muda huu hapa mlandizi limesimama basi la abood ambapo wakashushwa watu wawili wakipewa kichapo kitakatifu..kuuliza nikaambiwa wamekamatwa wakijaribu kuiba mabegi..wakati tunataka kuwafundisha adabu polisi wakawa wameshafika na kuondoka nao hadi kituoni.hivyo kama ni muhanga kuna wezi wawili wamekamatwa wapo kituo cha polisi mlandizi
 
Fanya taratibu ya kuwa na hand luggage/rucksack ndogo ya kuhifadhi vitu muhimu unaposafiri.
 
Kampuni inabidi kuanzisha taratibu ya kutoa luggage tag kama kampuni za ndege(AZam marine inayo utaratibu huu usafiri wa meli)

Bag tags, also known as baggage
tags, baggage checks or luggage
tickets, have traditionally been used
by bus, train and airline companies to
route passenger luggage that is
checked on to the final destination. The
passenger stub is typically handed to
the passenger or attached to the ticket
envelope: a) to aid the passenger in
identifying their bag among similar
bags at the destination baggage
carousel; b) as proof—still requested at
a few airports—that the passenger is
not removing someone else's bag from
the baggage reclaim hall; c) as a
means for the passenger and carrier to
identify and trace a specific bag that
has gone astray and was not delivered
at the destination.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…