Abiria wa mikoani waomba kusafiri usiku

Abiria wa mikoani waomba kusafiri usiku

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Abiria wa mabasi yanayotoka mikoa ya bara yanayopita mkoani Morogoro kuelekea jijini Dar es Salaam wameiomba serikali iruhusu mabasi ya abiria kusafiri baada ya saa sita usiku hasa katika maeneo ambayo sio hatarishi kwa usafiri wa wakati huo.

Abiria hao walitoa ombi hilo jana Ijumaa wakati wakizungumza na Mwananchi katika kituo cha mabasi Msamvu.
Wamelalamikia kitendo cha kuzuiwa kuendelea na safari hata kabla ya saa sita usiku na kubainisha kuwa kinasababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wengi.
Kwa muda mrefu sasa serikali imepiga marufuku mabasi ya abiria kuendelea na safari baada ya saa sita usiku hivyo baadhi ya mabasi yanayotoka mkoani Mwanza na Mbeya kuelekea Dar es Salaam yanalazimika kulala mkoani Morogoro.

Abiria Shiraji Nyanda alisema kulala njiani kunawaongezea wasafiri gharama na wale wenye watoto wanapata usumbufu zaidi.
"Nia ya serikali ni njema ya kuhakikisha usalama wa watu wake lakini kwa barabara ya Dar-Moro ni salama sana… wangeruhusu tu mabasi yaendelee na safari. Lakini kibaya zaidi tunazuiliwa hapa kabla hata ya hiyo saa sita," alisema Nyanda.

Hata hivyo, kwa mujibu wa kanuni zilizopo, mabasi ya abiria hayaruhusiwi kusafiri baada ya saa nne usiku.
Abiria mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jane Arnold, ambaye alikua anasafiri na watoto, alisema kulala kwenye basi na watoto kumemsababishia usumbufu na kumuongezea gharama za safari.

Akizungumzia malalamiko hayo, Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Morogoro, Victor Ayo, alisema mabasi hayo yanazuiliwa Morogoro sit u kwa kuogopa kutenkwa, bali pia kwa usalama wa abiria na vyombo hivyo vya usafiri.
Akifafanua, alibainisha kuwa mabasi yanazuiliwa kusafiri usiku ili pia kupunguza ajali zinazoweza kutokea kutokana na uchovu wa dereva.

Alisema kwa wakati huo dereva anakuwa amechoka baada ya kuendesha gari kwa muda mrefu na barabara hiyo inakuwa na msongamano wa malori.
"Niwashauri tu abiria wawe wavumilivu katika hili kwani linafanyika kulinda usalama wao," alisema.

Ofisa huyo pia aliwataka madereva kutii sheria za usalama barabarani ili kulinda usalama wao na usalama wa watumiaji wengine wa barabara.
 
Bora safari ya usiku,tochi zimekua kero sana.Yaani wanajificha maporini kisha unaonyeshwa picha eti umezidi speed 63 km/hr.Kenya wanasafiri usiku.Uchumi wetu utakua maana MTU atachagua asafiri muda gani baada ya kumaliza shughuli zake.Tutakua na uchumi wa SAA 24
 
Nchi zote zinazijitambua wanasafiri usiku. Ukiwa pale Nakonde unataka kwenda Lusaka unaondoka saa 10 jioni unafika alfajiri. Pale Isbania magari ya Nairobi yanaondoka saa 11 jioni watu wanafika Nairobi alfajiri. Advantage zake ni kuwa unafika kwa wakati unafanya shopping halafu unaondoka same day kama ni mfanyabiashara, badala ya watu kulala stendi huku wamesafiri kutwa nzima. Kwa wakati huu ambao speed inajulikana ni 80 polisi wanatakiwa kufunga GPS kwenye magari na kudhibiti mwendo huku usalama barabarani unaimarishwa kwa Patrol au escot badala ya kuwalaza watu kwenye gari ambayo ni kero na hatari kwa afya. Imebaki Tanzania tu ndio tuko gizani
 
Kufuatilia mwenendo wa mabasi kws GPS ni point ya msingi sana mkuu. Nimeshaona kampuni flani ya malori wao wana kama control center ambapo kuna watu wanafanya kazi ya kufuatilia mienendo ya malori yao yote. Polisi wana resources za kutosha hili haliwezi kuwashinda, waachane na teknologia za kizamani za tochi
 
polisi wanatakiwa kufunga GPS kwenye magari na kudhibiti mwendo
Polisi watakuwa na kazi sana wakisema wafunge GPS wataweza kumonitor kila gari? Pia kumbuka wamiliki ndio wako responsible na matengenezo magari yao wanaweza haribu makusudi isisome. Bora hii ya tochi inaheshima.
 
Isibania 2 Nairobi mabasi yanaondoka saa 11 jioni? Wakati flan nilitaka kupita isibania nikafika saa 6 mchana nikaambiwa mabasi ya Nairobi mpaka kesho yaKe
 
Akizungumzia malalamiko hayo, Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Morogoro, Victor Ayo, alisema mabasi hayo yanazuiliwa Morogoro sit u kwa kuogopa kutenkwa, bali pia kwa usalama wa abiria na vyombo hivyo vya usafiri.
Akifafanua, alibainisha kuwa mabasi yanazuiliwa kusafiri usiku ili pia kupunguza ajali zinazoweza kutokea kutokana na uchovu wa dereva.

Basi matuta yaondolewe njia kuu zote maana ile punguza na ongeza mwendo kwenye matuta nayo ni chanzo kikubwa cha uchovu kwa wasafiri na madereva hata kuchelewesha mabasi kufika sehemu husika kwa wakati
 
Hakuna mantiki ma basi yanayoka mbali kama Bukoa, Musoma,Kampala Rwanda na Sudani nk yaweke Madereva Dodoma kupokea mabasi hayo. Na Iringa au Morogoro.
Wawe shanter na wasajiliwe basi
 
Nchi zote zinazijitambua wanasafiri usiku. Ukiwa pale Nakonde unataka kwenda Lusaka unaondoka saa 10 jioni unafika alfajiri. Pale Isbania magari ya Nairobi yanaondoka saa 11 jioni watu wanafika Nairobi alfajiri. Advantage zake ni kuwa unafika kwa wakati unafanya shopping halafu unaondoka same day kama ni mfanyabiashara, badala ya watu kulala stendi huku wamesafiri kutwa nzima. Kwa wakati huu ambao speed inajulikana ni 80 polisi wanatakiwa kufunga GPS kwenye magari na kudhibiti mwendo huku usalama barabarani unaimarishwa kwa Patrol au escot badala ya kuwalaza watu kwenye gari ambayo ni kero na hatari kwa afya. Imebaki Tanzania tu ndio tuko gizani
Kwa sasa hakuna safari za usiku kwa mabasi pale nakonde
 
Polisi watakuwa na kazi sana wakisema wafunge GPS wataweza kumonitor kila gari? Pia kumbuka wamiliki ndio wako responsible na matengenezo magari yao wanaweza haribu makusudi isisome. Bora hii ya tochi inaheshima.
Basi za dar mwanza zimeshafungwa GPS kwa majaribio...
 
Wenzetu nchi za Kusini mabasi ya safari ndefu husafiri usiku lakini hakuna ajali zinazosemwa. Wao hudai wakati wa usiku husaidia sana kwani lami hua imepoa hivyo ni salama Kwa tairi pia.
Muulize Mzee John Samweli Malekela atakwambia habari ya kusafiri usiku na madhara yake huko tuliko toka.
 
Kuna kipindi jamaa walikua wanatoboa..wanaingia ubungo usiku mwingi..
 
Abiria wa mabasi yanayotoka mikoa ya bara yanayopita mkoani Morogoro kuelekea jijini Dar es Salaam wameiomba serikali iruhusu mabasi ya abiria kusafiri baada ya saa sita usiku hasa katika maeneo ambayo sio hatarishi kwa usafiri wa wakati huo.

Abiria hao walitoa ombi hilo jana Ijumaa wakati wakizungumza na Mwananchi katika kituo cha mabasi Msamvu.
Wamelalamikia kitendo cha kuzuiwa kuendelea na safari hata kabla ya saa sita usiku na kubainisha kuwa kinasababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wengi.
Kwa muda mrefu sasa serikali imepiga marufuku mabasi ya abiria kuendelea na safari baada ya saa sita usiku hivyo baadhi ya mabasi yanayotoka mkoani Mwanza na Mbeya kuelekea Dar es Salaam yanalazimika kulala mkoani Morogoro.

Abiria Shiraji Nyanda alisema kulala njiani kunawaongezea wasafiri gharama na wale wenye watoto wanapata usumbufu zaidi.
"Nia ya serikali ni njema ya kuhakikisha usalama wa watu wake lakini kwa barabara ya Dar-Moro ni salama sana… wangeruhusu tu mabasi yaendelee na safari. Lakini kibaya zaidi tunazuiliwa hapa kabla hata ya hiyo saa sita," alisema Nyanda.

Hata hivyo, kwa mujibu wa kanuni zilizopo, mabasi ya abiria hayaruhusiwi kusafiri baada ya saa nne usiku.
Abiria mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Jane Arnold, ambaye alikua anasafiri na watoto, alisema kulala kwenye basi na watoto kumemsababishia usumbufu na kumuongezea gharama za safari.

Akizungumzia malalamiko hayo, Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Morogoro, Victor Ayo, alisema mabasi hayo yanazuiliwa Morogoro sit u kwa kuogopa kutenkwa, bali pia kwa usalama wa abiria na vyombo hivyo vya usafiri.
Akifafanua, alibainisha kuwa mabasi yanazuiliwa kusafiri usiku ili pia kupunguza ajali zinazoweza kutokea kutokana na uchovu wa dereva.

Alisema kwa wakati huo dereva anakuwa amechoka baada ya kuendesha gari kwa muda mrefu na barabara hiyo inakuwa na msongamano wa malori.
"Niwashauri tu abiria wawe wavumilivu katika hili kwani linafanyika kulinda usalama wao," alisema.

Ofisa huyo pia aliwataka madereva kutii sheria za usalama barabarani ili kulinda usalama wao na usalama wa watumiaji wengine wa barabara.
Watulize mzuka kwa faida yao. Highway zetu zote zimejaa mahandaki. Si rahisi dereva kuyaona yote usiku huku akiwa naye amechoka. Hayo ya majambazi na malori yasiyo na reflectors ni nyongeza tu.
 
Back
Top Bottom