Abdulrahman Kinana: Who is he?

Abdulrahman Kinana: Who is he?

KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Abdulrahaman Kinana atangaza kung’atuka rasmi katika siasa .Written by haki | // 0 comments
Kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana
--
KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana ametangaza kung’atuka rasmi katika siasa baada ya kukitumia chama chake kwa miaka 25 akiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Kamati Kuu (CC) na Kamati ya Maadili. Kinana ambaye amekuwa Meneja wa Kampeni za mgombea urais wa CCM tangu mwaka 1995 ulipoanza uchaguzi wa vyama vingi, alisema kwamba baada ya kutumikia chama katika nyadhifa za juu kwa robo karne sasa, ameamua kupumzika ili kuwaachia vijana waendelee kukijenga chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika.

“Nimekuwa Mjumbe wa NEC kwa miaka 25, bila shaka muda huu unatosha, kwani wanaCCM wamenipa heshima ya kuwa katika vikao vya juu vya chama kwa robo karne. Sasa ni wakati wa kung’atuka, nimetoa mchango kwa kadri nilivyoweza katika vikao mbalimbali na katika shughuli nyingi,” alisema. Alisema anaamini kuachana kwake na siasa hakutakuwa na madhara kwa chama chake, kwani CCM ina hazina kubwa ya viongozi ambao wana sifa na wanaweza kuongoza chama hicho kuelekea Uchaguzi wa 2015.

“Uongozi ni kupokezana vijiti. Wako wanaCCM wazuri, walio na uwezo mkubwa na sifa za kutosha kuongoza. Nawashukuru wanaCCM na viongozi kwa heshima waliyonipa wakati wote huu,” alisema Kinana ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni wa Rais Benjamin Mkapa kwa vipindi viwili na Rais Jakaya Kikwete kwa vipindi viwili vya uchaguzi. Kinana alisema anajivunia kufanya kazi na marais wote wa Tanzania kuanzia Mwalimu Julius Nyerere hadi Rais Kikwete kwa uadilifu mkubwa na kuheshimiana.

”Ushauri wangu katika vikao umekuwa ukiheshimika sana. Nimekuwa nikiheshimiwa na uongozi wote wa CCM na hata wapinzani nao tunaheshimiana. Nimesimamia kampeni za kistaarabu na ambazo zimeleta ushindi mkubwa kwa CCM tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi,” alisema. Kinana ambaye pia alikuwa Spika wa Kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), ameshauri vijana ndani ya CCM watangulize masilahi ya taifa mbele na wasikilize wananchi. Ni muhimu washikamane, wabuni mikakati ya kusaidia kukuza uchumi kwa haraka zaidi na kuendeleza umoja na undugu wetu,” alisema.

Ushauri wa viongozi wapya CCM Kinana alishauri viongozi wapya ambao wanatarajiwa kuchaguliwa ndani ya chama chake, iwapo wataona upungufu wake wausahihishe. “Ni matumaini yangu kuwa watakaopata uongozi wataona upungufu na watasahihisha makosa yangu,” alisema. Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2015, Kinana aliwaasa viongozi wasiwaze nani anafaa kuwa mgombea urais bali washughulikie kero za wananchi.

“Bado tuna kazi kubwa ya kutekeleza Ilani. Tusiwasumbue Watanzania kuwa ni nani anafaa kuwa Rais bali tushughulikie matatizo yao. Kwa sasa ajenda ya CCM ni kutekeleza ahadi zetu katika sekta zote siyo kutafuta nani atakuwa Rais 2015," alisema na kuongeza:

"Hata wapinzani wawaeleze Watanzania yale ambao wamedhamiria kutekeleza. Kueleza upungufu wa CCM ni mtaji mdogo kwa wapinzani, ajenda kubwa ni watafanya nini? Hapa bado wana kazi kubwa. Wanapoona upungufu wasisite kutusema,” Kinana ambaye ana shahada ya uzamili katika utawala na masuala ya sera kutoka Chuo Kikuu cha Harvad nchini Marekani, alisema anatarajia kufundisha na kusoma Shahada ya Uzamivu (PhD) katika moja ya vyuo vikuu vya hapa nchini.

“Baada ya kustaafu kuna mambo mawili ambayo natarajia kufanya. La kwanza ni kuona kama naweza kufundisha. Pili kusoma katika mojawapo ya vyuo vikuu vyetu,” alisema. Mbali na nyadhifa zilizotajwa huko juu, Kinana ametumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa muda mrefu na kupanda cheo hadi kufikia Kanali. Amewahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mbunge wa Arusha Mjini
 
Pia ni mzuri kwenye wizi wa kura ,kacheza picha ya EPA na deal za pembe za ndovu si mbovu ni gamba na fisadi wa karne anaweza kufungua chuo! kwa hayo
 
Kweli huyu jamaa alitoka jeshini akiwa amebobea haswa kwenye mambo ya ujeshi...sishangai akiwa anafanya madudu yote haya. Watu kama hao wakikaa bure mtaani unafikiri wanafanya nini? Ni excellent or worst of all!
 
A quote from Julius Nyerere " Kila nilipokuwa nikitaka kung'atuka, walikuwa wakiniambia Mwalimu andelea tu, hii nchi bado ni changa na umeitoa mbali, nchi haitaendelea bila wewe. Nami niliendelea, hadi pale nilipokuja kugundua kumbe nchi changa wanayoiongelea ni FAMILIA ZAO, na hazitaendelea bila mimi kuwepo madarakani, maana walikuwa hawana uhakika kama RAIS ajae atawaacha katika nafasi walizokuwa nazo" mwisho wa nukuu. Haya ndio maneno wasemayo viongozi wetu wa sasa, wanasema BILA CCM nchi haitaendelea, lakini ukweli ni kuwa BILA CCM ufisadi wao hautaendelea, maana hawan uhakika kama CHAMA kingine kikichukua nchi watabaki salama!

LIKE yangu imechelewa kwa miaka miwili!
 
Mzee Kinana hana ubavu mkubwa wa kujitetea au kulumbana na Augustine Lyatonga Mrema kama alivyofanya Kadogoo.Tatizo dogo tu, Kadogoo anamjua mwendawazimu mmoja aitwaye Mrema wakati watu wa Vunjo wanamjua Mheshimiwa Augustine Lyatonga Mrema kama Mbunge wao na yamkini hata mama yake Kadogoo na wakina mama wengine wanajua alivyowabana wanaume ambao hawana hoja zaidi ya matusi kurusha ngumi na mateke na vichwa!
 
Majuzi nimesikia kwamba Kinana alitinga kiwanjani kumpokea mwarabu mmoja mwekezaji wa Hotel za Kilinjaro zina jina jipya. Alikuwa kaongozana na wala rushwa waziri gani sijui yule.

Nimejiuliza Kinana ni nani kweney Serikali hadi aende upokea mwekezaji? Alienda kwa jina la CCM ama Serikali ? Kinana na issue yake ya Uraia iliishia wapi?

Nipeni mwelekeo kama kuna mwenye kulijua lolote hapa.

.....Labda ni mdau mwenzake katika kuwekeza katika hoteli zake za uarabuni.... .
 
Kinana namfahamu sana ni mzee clean hana mambo ya ufisadi hata kidogo ni mtu wa kutegemewa ndani ya CCM kwa ushauri na mambo mengi tu hata ya usalama wa nchi sula la uraia halina mashiiko ni mtanzania halisi mwenye asili ya Kisomali.Kuwa Mtanzania si lazima uwe Mbantu ila ni kuipenda nchi na kutanguliza maslahi yake mbele

.....ukikutana naye muulize kuhusu zile hoteli uarabuni alizipataje??....
 
Kuna ile kampuni ya uchimbaji mafuta iliyokuwa huko Mtwara alihusishwa nayo,nadhani ikiitwa "Artumas Group Inc" kama sikosei.So hata hizi vurugu zake maybe anajipanga tu,na yeye ni fisadi.
Hapo chini ni mjadala ule kipindi kilee!
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/15393-abdlahaman-kinana-na-artumas-4.html#post4689740

jmushi@ acha majungu yasio na tija, Mzee Kinana nimiongoni mwa watu waadilifu sana na hana chembe yoyote ya ufisadi. Mtu wa watu na mahiri sana ndio maana heshima yake iko juu sana. Yupo nchini na ameamua kung'atuka na shughuli za uongozi wa CCM ili awapishe vijana nao wakue kiuongozi. Yeye ni BBC (Born before computer) huu ni wakati wa dot com (Kizazi cha facebook na mtandao)
 
Huyu ni mwizi anayeweka pesa za vigogo wa CCM na kuwafundisha namna ya kusema uongo ili waendelee kula nchi. Akichukua nchi hii magufuri aah ni Sita aaaaah nimekosea Lembeli aaaaaaah ni Filikunjombe aaaaaaaaah wamekwisha

Fitina mbaya!!
 
jmushi@ acha majungu yasio na tija, Mzee Kinana nimiongoni mwa watu waadilifu sana na hana chembe yoyote ya ufisadi. Mtu wa watu na mahiri sana ndio maana heshima yake iko juu sana. Yupo nchini na ameamua kung'atuka na shughuli za uongozi wa CCM ili awapishe vijana nao wakue kiuongozi. Yeye ni BBC (Born before computer) huu ni wakati wa dot com (Kizazi cha facebook na mtandao)
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/15393-abdlahaman-kinana-na-artumas-4.html#post4689740 Umeufuatilia huu mjadala uone majungu yangu yako wapi?
 
mku nafkir ungetumia lugha ya taifa ili tuelewane vizuri mana wengne mstar mzima tunasoma dictionary!,au iv ndo hua inaeleweka vzur!
 
huyu jamaa ni tajiri sana na ni deal breaker wa viongozi wengi serikalini, inasemekana ni mtu mwenye kichwa kizuri sana na ana mahusiano mazuri sana na viongozi wengi afrika mashariki siyo tu tanzania. uraia wake uliwahi kutiliwa shaka kwa sababu za kisiasa lakini hakuwahi kuzuiliwa kugombea ubunge na mahakama bali aliacha mwenyewe.

anamiliki hisa nyingi kwenye mashirika mengi makubwa kule bandarini kama vile emirates shipping, diamond shipping na mengine. pia ni maarufu kwa kuandika jina lake kwenye hisa za baadhi ya viongozi na ni mtu msiri sana. si jambo la ajabu kuingia Ikulu na kumkuta kinana akizunguuka kama vile yuko nyumbani kwake maana marais wote waliopita Tanzania wamekuwa wakimpenda na kumwamini sana. mbali na kuwa na master digrii ya Harvard pia kinana ana uwezo mkubwa sana wa kutengeneza mikakati ya kisiasa na kiutawala
 
Jamani naomba niwaulize swali linalonitatiza sana.Watu wanasema kwamba huyu mzee KINANA ni msomali na si mtanzania,sasa mimi kila nikimwangali na kumfananisha na wasomali naona hafanani nao,mana mi nimekaa sana na wasomali kule kenya,sasa nauliza huyu msomali ni msomali wa wapi? na mama yake na baba yake ni wa wapi? jina lake kweli linaonekana kabisa si la kitanzania hadi la ukoo hivyo kuwatia watu mashaka lakini mwenyewe ukimwona hata baadhi ya wamasai wanaweza kuwa wasomali kushinda mzee kinana,jambo jingine anachonishangaza ni kwamba anaonekana ni mjanja mno na ni mwerevu vibaya sana na bila shaka atakuwa na elimu sana pia nimegundua kwamba anapendwa sana na kuheshimiwa mno na CCM wenzake hadi viongozi wa upinzani hawakubali hilo hadharani ila kivitendo wanamweshimu sana nadhani anaweza kuwa anaongoza kwa kuheshimiwa na wote toka ccm,basi kwa wale wataalam munaomwelewa vizuri mtu huyu nifahamisheni nipate kuelewa na kuondoa tetesi hizi.
 
Jamani naomba niwaulize swali linalonitatiza sana.Watu wanasema kwamba huyu mzee KINANA ni msomali na si mtanzania,sasa mimi kila nikimwangali na kumfananisha na wasomali naona hafanani nao,mana mi nimekaa sana na wasomali kule kenya,sasa nauliza huyu msomali ni msomali wa wapi? na mama yake na baba yake ni wa wapi? jina lake kweli linaonekana kabisa si la kitanzania hadi la ukoo hivyo kuwatia watu mashaka lakini mwenyewe ukimwona hata baadhi ya wamasai wanaweza kuwa wasomali kushinda mzee kinana,jambo jingine anachonishangaza ni kwamba anaonekana ni mjanja mno na ni mwerevu vibaya sana na bila shaka atakuwa na elimu sana pia nimegundua kwamba anapendwa sana na kuheshimiwa mno na CCM wenzake hadi viongozi wa upinzani hawakubali hilo hadharani ila kivitendo wanamweshimu sana nadhani anaweza kuwa anaongoza kwa kuheshimiwa na wote toka ccm,basi kwa wale wataalam munaomwelewa vizuri mtu huyu nifahamisheni nipate kuelewa na kuondoa tetesi hizi.


Kinana ni kati wanasiasa wachache kama wapo ndani ya CCM ambao wana upeo mpana sana katika masuala muhimu ,anaheshimijka na makundi yote ndani ya chama, anaheshimika na viongozi wa upinzani,ni mkweli mvumilivu sana, hana tabia ya kujikweza kama walivyo wanasiasa wengi wa chama tawala,ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja ni mtu wa watu.

kama binadamu ana mapungufu yake lakini kwa kifupi jamaa ni MWUUNGWANA sana
 
Back
Top Bottom