Jamani naomba niwaulize swali linalonitatiza sana.Watu wanasema kwamba huyu mzee KINANA ni msomali na si mtanzania,sasa mimi kila nikimwangali na kumfananisha na wasomali naona hafanani nao,mana mi nimekaa sana na wasomali kule kenya,sasa nauliza huyu msomali ni msomali wa wapi? na mama yake na baba yake ni wa wapi? jina lake kweli linaonekana kabisa si la kitanzania hadi la ukoo hivyo kuwatia watu mashaka lakini mwenyewe ukimwona hata baadhi ya wamasai wanaweza kuwa wasomali kushinda mzee kinana,jambo jingine anachonishangaza ni kwamba anaonekana ni mjanja mno na ni mwerevu vibaya sana na bila shaka atakuwa na elimu sana pia nimegundua kwamba anapendwa sana na kuheshimiwa mno na CCM wenzake hadi viongozi wa upinzani hawakubali hilo hadharani ila kivitendo wanamweshimu sana nadhani anaweza kuwa anaongoza kwa kuheshimiwa na wote toka ccm,basi kwa wale wataalam munaomwelewa vizuri mtu huyu nifahamisheni nipate kuelewa na kuondoa tetesi hizi.
Huyu jamaa ni msomali pure,nenda pale Arusha kuna drycliner moja inaitwa facon,ipo karibu na metropole cinema, kuna mdogo wake pale ni msomali wala huna haja ya kuuliza.wazazi wake pia ni wasomali wapo pale mtaa wa bondeni,hatakama sio wazazi wa kumzaa pale ndio kwao na ndugu zake wapo pale.huyu jamaa kwa ukweli ni portures,tembo na faru wote kawamaliza yeye.
Huyu jamaa ni msomali pure,nenda pale Arusha kuna drycliner moja inaitwa facon,ipo karibu na metropole cinema, kuna mdogo wake pale ni msomali wala huna haja ya kuuliza.wazazi wake pia ni wasomali wapo pale mtaa wa bondeni,hatakama sio wazazi wa kumzaa pale ndio kwao na ndugu zake wapo pale.huyu jamaa kwa ukweli ni portures,tembo na faru wote kawamaliza yeye.
Si anajifanya amebobea kwenye intelijensia,CDM 2015 mwekeni ktk timu ya kampeni Mabere Marando ili ale nae sahani moja,mwizi wa kila aina huyu jasusi tena atakuwa ni Freemason huyu rafiki mkubwa wa Sir Chande!Pia ni mzuri kwenye wizi wa kura ,kacheza picha ya EPA na deal za pembe za ndovu si mbovu ni gamba na fisadi wa karne anaweza kufungua chuo! kwa hayo
Naona ni mTanzania kwa vile kazaliwa Nduruma na mama yake ni Mtanzania ijapokuwa ni Msomali.
KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Abdulrahaman Kinana atangaza kungatuka rasmi katika siasa .Written by haki | // 0 comments
Kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana
--
KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana ametangaza kungatuka rasmi katika siasa baada ya kukitumia chama chake kwa miaka 25 akiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Kamati Kuu (CC) na Kamati ya Maadili. Kinana ambaye amekuwa Meneja wa Kampeni za mgombea urais wa CCM tangu mwaka 1995 ulipoanza uchaguzi wa vyama vingi, alisema kwamba baada ya kutumikia chama katika nyadhifa za juu kwa robo karne sasa, ameamua kupumzika ili kuwaachia vijana waendelee kukijenga chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika.
Nimekuwa Mjumbe wa NEC kwa miaka 25, bila shaka muda huu unatosha, kwani wanaCCM wamenipa heshima ya kuwa katika vikao vya juu vya chama kwa robo karne. Sasa ni wakati wa kungatuka, nimetoa mchango kwa kadri nilivyoweza katika vikao mbalimbali na katika shughuli nyingi, alisema. Alisema anaamini kuachana kwake na siasa hakutakuwa na madhara kwa chama chake, kwani CCM ina hazina kubwa ya viongozi ambao wana sifa na wanaweza kuongoza chama hicho kuelekea Uchaguzi wa 2015.
Uongozi ni kupokezana vijiti. Wako wanaCCM wazuri, walio na uwezo mkubwa na sifa za kutosha kuongoza. Nawashukuru wanaCCM na viongozi kwa heshima waliyonipa wakati wote huu, alisema Kinana ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni wa Rais Benjamin Mkapa kwa vipindi viwili na Rais Jakaya Kikwete kwa vipindi viwili vya uchaguzi. Kinana alisema anajivunia kufanya kazi na marais wote wa Tanzania kuanzia Mwalimu Julius Nyerere hadi Rais Kikwete kwa uadilifu mkubwa na kuheshimiana.
Ushauri wangu katika vikao umekuwa ukiheshimika sana. Nimekuwa nikiheshimiwa na uongozi wote wa CCM na hata wapinzani nao tunaheshimiana. Nimesimamia kampeni za kistaarabu na ambazo zimeleta ushindi mkubwa kwa CCM tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, alisema. Kinana ambaye pia alikuwa Spika wa Kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), ameshauri vijana ndani ya CCM watangulize masilahi ya taifa mbele na wasikilize wananchi. Ni muhimu washikamane, wabuni mikakati ya kusaidia kukuza uchumi kwa haraka zaidi na kuendeleza umoja na undugu wetu, alisema.
Ushauri wa viongozi wapya CCM Kinana alishauri viongozi wapya ambao wanatarajiwa kuchaguliwa ndani ya chama chake, iwapo wataona upungufu wake wausahihishe. Ni matumaini yangu kuwa watakaopata uongozi wataona upungufu na watasahihisha makosa yangu, alisema. Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2015, Kinana aliwaasa viongozi wasiwaze nani anafaa kuwa mgombea urais bali washughulikie kero za wananchi.
Bado tuna kazi kubwa ya kutekeleza Ilani. Tusiwasumbue Watanzania kuwa ni nani anafaa kuwa Rais bali tushughulikie matatizo yao. Kwa sasa ajenda ya CCM ni kutekeleza ahadi zetu katika sekta zote siyo kutafuta nani atakuwa Rais 2015," alisema na kuongeza:
"Hata wapinzani wawaeleze Watanzania yale ambao wamedhamiria kutekeleza. Kueleza upungufu wa CCM ni mtaji mdogo kwa wapinzani, ajenda kubwa ni watafanya nini? Hapa bado wana kazi kubwa. Wanapoona upungufu wasisite kutusema, Kinana ambaye ana shahada ya uzamili katika utawala na masuala ya sera kutoka Chuo Kikuu cha Harvad nchini Marekani, alisema anatarajia kufundisha na kusoma Shahada ya Uzamivu (PhD) katika moja ya vyuo vikuu vya hapa nchini.
Baada ya kustaafu kuna mambo mawili ambayo natarajia kufanya. La kwanza ni kuona kama naweza kufundisha. Pili kusoma katika mojawapo ya vyuo vikuu vyetu, alisema. Mbali na nyadhifa zilizotajwa huko juu, Kinana ametumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa muda mrefu na kupanda cheo hadi kufikia Kanali. Amewahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mbunge wa Arusha Mjini
Hivi hapa munajadili nini? Huyu Kinana ni Kada wa CCM na alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali ktk nchi yetu wala huko nyuma wakati wa utawala wa Mwalimu, Kinana hakuwahi kujadiliwa uraia wake ila ktk kipindi cha Mwinyi na huyu mwendawazimu aliyekuwa wakati huo Waziri wa mambo ya ndani Augustine Mrema!
Huyu Mrema alikuwa na rafiki yake aliyetaka kugombea ubunge wa arusha lakini tishio lilikuwa ni Abdurahmani kinana aliyekuwa mbunge wa muda mrefu huko Arusha na kwa kweli alikuwa akipendwa sana na wananchi wa Arusha Mjini, ndipo huyu Mwendawazimu Mrema kwa kutumia wadhifa wake huo akachomowa faili la uraia la Kinana ktk uhamiaji na kupayuka kuwa Kinana hawezi kugombea ubunge wa arusha mjini ati kwa sababu uraia wake unautata!
Sasa na nyinyi humu bado munaendeleza majungu yaleyale yaliyopitwa na wakati? yaani badala ya kujadili mambo muhimu yanayotukera leo kama vile ujinga, maradhi, njaa, shida ya umeme, barabara mbovu, rushwa,ukabila, udini, ujambazi, mauwaji, uongozi mbovu, umasikini, nk. tunamjadili Kinana kama ni raia au si raia? sasa mumevuka mpaka maana munataka kuingilia kazi za uhamiaji!
Kama hamumjui Kinana basi mimi namjuwa vizuri sana, mtaa na hospitali aliyozaliwa, Baba yake na mama ake wote ni wa TZ sasa kama nyinyi munaushahidi kuwa Kinana si raia basi thibitisheni hilo ili uhamiaji waweze kumshugulikia! lakini hilo haliwezekani kwani yeye ni kada damu wa CCM labda ajiunge na upinzani!
Kama munadai Kinana si raia ati kwa sababu asili yake ni usomali basi mbona wengi wetu hatutakuwa raia kwani asili zetu wengi ni kutoka nchi mbalimbali kama vile Malawi, Zaire, Kenya, Uganda, Ethiopia, Comoro, Arabuni nk.?
Tuache majungu na hasa hasa udini maana huyu Kinana kwa kuwa munamuona ni Muislamu na ana asili ya usomali! hata Salim Ahmed Salim alijadiliwa Uarabu wake wakati akigombea urais 2005!
Nchi yoyote yenye kufuata misingi au utawala wa sheria haiwezi kumbagua raia wake yoyote yule kwa misingi ya rangi, dini, jinsia au asili ya mtu! tuache fitina na chokochoko! sanasana wewe unaemjadili Kinana tukikuchunguza tunaweza kukugunduwa uharamu wa uraia wako!
Ndugu, Wewe kwa akili yako umeona wikipedia is a reliable source of information?.Kadogooo usitake kuchefua watu hapa. Hivi huyu Kinena ni baba au babu yako???
Unatetea ujinga. Kinana Uraia wake ni questionable utake usitake. Hemu jaribu kusoma hii Biograph yake toka kwenye Wekipedia:
Kwamba alizaliwa mwaka 1951, akatumikia Jeshi la Wananchi Tanzania kwa miaka 20 na akastahafu Jeshi mwaka 1972!!!Je, wewe kwa akili yako unaweza kukubaliana na uongo huu ulio dhahiri hapa? Kwamba mtu amezaliwa mwaka 1951, kwa maana hiyo mwaka 1972 alikuwa na miaka 21 lakini mwaka huohuo akastahafu Jeshi baada ya kulitumikia kwa miaka 20 akiwa na Cheo cha Kanali.......!!!!
Hiki ni kichekesho. Lazima kuna siri inafichwa mahali fulani hapa. Watangnyika tunataka kujua Uraia halali wa Kinena. Kazaliwa wapi, na nani na mwaka gani!!! Kinana na vibaraka wake wa CCM kuna kitu wanaficha hapa. Kinana ana asili ya Kisomali, tunataka kujua wazazi wake wako Somalia au wako Tanzania? Na kama wako Tanzania walikuja mwaka gani na yeye alizaliwa Somalia au Tanzania? Je, alishawahi kuukana Uraia wake wa Somalia na kupewa Uraia wa Tanganyika?? Maana kama kweli alizaliwa mwaka 1951 iwe Somali au Tanzania lazima atakuwa aliandikishwa kama Raia wa Tanganyika!
Sasa wewe Bwana Kadogoo tunaomba utuwekee hapa Jamvini Birth Certificate ya Kinana ikionyesha alizaliwa tarehe ngapi huo mwaka wa 1951,hosptali gani,Kijiji gani,Tarafa,Wilaya na Mkoa na nani walikuwa wazazi wake. Kama aliapa Mahakamani weka Affidavidt yake kuonyesha ni Mahakama gani na nani walikuwa Mashaidi wake. Je, Passport yake ya kwanza aliipata mwaka gani na ilitolewa wapi na alikuwa anasafiri nje ya nchi kwenda wapi???
Tunaomba majibu ili tujiridhishe kama kweli Kinana ni Raia Halali wa Jamhuri ya Watu wa Tanganyika.
Abdulrahman Kinana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jump to: navigation, search
[TABLE="class: metadata plainlinks ambox ambox-content ambox-Refimprove"]
[TR]
[TD="class: mbox-image"][/TD]
[TD="class: mbox-text"]This article needs additional citations for verification. Please help improve this article by adding citations to reliable sources. Unsourced material may be challenged and removed. (May 2013)[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: infobox vcard, width: 22"]
[TR]
[TH="class: n, colspan: 2, align: center"]Abdulrahman Kinana[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2, align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="bgcolor: lavender, colspan: 2, align: center"]Chama Cha Mapinduzi Secretary General[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: lavender, colspan: 2, align: center"]Incumbent[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2, align: center"]Assumed office
November 2012[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"]Chairman[/TH]
[TD]Jakaya Kikwete[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"]Preceded by[/TH]
[TD]Wilson Mukama[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="bgcolor: lavender, colspan: 2, align: center"]1st Speaker of the EALA[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 2, align: center"]In office
November 2001 – 2006[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"]Succeeded by[/TH]
[TD]Abdirahim Abdi[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="bgcolor: lavender, colspan: 2, align: center"]Personal details[/TH]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"]Nationality[/TH]
[TD]Tanzanian[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"]Political party[/TH]
[TD]CCM[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Abdulrahman Omari Kinana is a Tanzanian politician who served as the first Speaker of the East African Legislative Assembly.[SUP][1][/SUP]
Kinana Background
Kinana served in the Tanzanian armed forces for 20 years before retiring as a Colonel in 1972.
He has also served as the Deputy Minister of Defence, Deputy Minister Foreign Affairs and Minister of Defence. He was also a member of the Tanzanian Parliament for Arusha constituency for 10 years.