Hivi hapa munajadili nini? Huyu Kinana ni Kada wa CCM na alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali ktk nchi yetu wala huko nyuma wakati wa utawala wa Mwalimu, Kinana hakuwahi kujadiliwa uraia wake ila ktk kipindi cha Mwinyi na huyu mwendawazimu aliyekuwa wakati huo Waziri wa mambo ya ndani Augustine Mrema!
Huyu Mrema alikuwa na rafiki yake aliyetaka kugombea ubunge wa arusha lakini tishio lilikuwa ni Abdurahmani kinana aliyekuwa mbunge wa muda mrefu huko Arusha na kwa kweli alikuwa akipendwa sana na wananchi wa Arusha Mjini, ndipo huyu Mwendawazimu Mrema kwa kutumia wadhifa wake huo akachomowa faili la uraia la Kinana ktk uhamiaji na kupayuka kuwa Kinana hawezi kugombea ubunge wa arusha mjini ati kwa sababu uraia wake unautata!
Sasa na nyinyi humu bado munaendeleza majungu yaleyale yaliyopitwa na wakati? yaani badala ya kujadili mambo muhimu yanayotukera leo kama vile ujinga, maradhi, njaa, shida ya umeme, barabara mbovu, rushwa,ukabila, udini, ujambazi, mauwaji, uongozi mbovu, umasikini, nk. tunamjadili Kinana kama ni raia au si raia? sasa mumevuka mpaka maana munataka kuingilia kazi za uhamiaji!
Kama hamumjui Kinana basi mimi namjuwa vizuri sana, mtaa na hospitali aliyozaliwa, Baba yake na mama ake wote ni wa TZ sasa kama nyinyi munaushahidi kuwa Kinana si raia basi thibitisheni hilo ili uhamiaji waweze kumshugulikia! lakini hilo haliwezekani kwani yeye ni kada damu wa CCM labda ajiunge na upinzani!
Kama munadai Kinana si raia ati kwa sababu asili yake ni usomali basi mbona wengi wetu hatutakuwa raia kwani asili zetu wengi ni kutoka nchi mbalimbali kama vile Malawi, Zaire, Kenya, Uganda, Ethiopia, Comoro, Arabuni nk.?
Tuache majungu na hasa hasa udini maana huyu Kinana kwa kuwa munamuona ni Muislamu na ana asili ya usomali! hata Salim Ahmed Salim alijadiliwa Uarabu wake wakati akigombea urais 2005!
Nchi yoyote yenye kufuata misingi au utawala wa sheria haiwezi kumbagua raia wake yoyote yule kwa misingi ya rangi, dini, jinsia au asili ya mtu! tuache fitina na chokochoko! sanasana wewe unaemjadili Kinana tukikuchunguza tunaweza kukugunduwa uharamu wa uraia wako!