Abdulrahman Kinana: Who is he?

tibwilitibwili

Senior Member
Sep 12, 2006
184
10
Majuzi nimesikia kwamba Kinana alitinga kiwanjani kumpokea mwarabu mmoja mwekezaji wa Hotel za Kilinjaro zina jina jipya. Alikuwa kaongozana na wala rushwa waziri gani sijui yule.

Nimejiuliza Kinana ni nani kweney Serikali hadi aende upokea mwekezaji? Alienda kwa jina la CCM ama Serikali ? Kinana na issue yake ya Uraia iliishia wapi?

Nipeni mwelekeo kama kuna mwenye kulijua lolote hapa.

UPDATE: (August 2010)

The campaign director of President Benjamin Mkapa in the Tanzanian presidential contests of 1995 and 2000 was later elected speaker of the East Africa Legislative Assembly (EALA) before becoming the campaign director of President Jakaya Mrisho Kikwete in the Tanzanian presidential contests of year 2010.

A retired colonel who served as foreign minister and later defense minister under President Ali Hassan Mwinyi.

Abdulrahman Omari Kinana is a member of the national executive committee of the ruling Chama cha Mapinduzi (CCM) party.

Born in the Arusha region in October 1951, Kinana did his primary and secondary studies in that city, before attending the Old Moshi Secondary School.

He was one of those responsible for the TANU party youth organization in the Korogwe district between 1971 and 1972, before following the teachings of the Kivukoni Ideological College in 1973.

From 1974 to 1985, he undertook a long career as a political commissar in several military schools, and from 1984 to 1985, at the 20th division of the Tanzania Peoples Defence Force (TPDF).

In the meantime, in 1984, he had graduated from the university of Ljubljana in Yugoslavia.

For a decade, he also served as MP in the Tanzanian parliament for the district of Arusha.

Abdulrahman Omari Kinana can also boast a master's in management and public administration from Harvard, and heads the Tanzania Red Cross Society, which is under the patronage of President Benjamin Mkapa.
 
Tibwili nadhani Kinana yuko Dar ni kigogo anakula kwa mrija na CCM wanamwita thinker tank wao
 
Huyu Muungwana yupo Dar, baada ya kuondoka kwenye Uspika wa EA, hivi sasa amebaki na Wadhifa wake wa muda mrefu wa Chairman wa Red Cross - Tanzania, akiwa na Katibu wake mkuu na rafikiye mkubwa Adam Kimbisa,pia yupo busy na biashara yake ya kufua nguo pale Namanga - Dar (Falcon).

Ni mjumbe ktk bodi mbalimbali na bado serikali inamtumia kwenye mambo mengi kwa sababu ya Umtandao wake!

Inawezekana kweli yupo Harvard lakini habari hiyo itakuwa mpya zaidi.
 
Huyu Kinana ni Msomali ambaye tumefichwa kuambiwa aliingaje Tanzania na kupewe madaraka mbalimbali ingawa inajulikana kabisa kuwa si mtanzania. Jamaa aliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha!
 
Kichuguu,
Si ubunge tu. Mwinyi aliwahi kumteua naibu waziri wa ulinzi. Ndiyo, naibu waziri wa ulinzi.
 
Hivi hapa munajadili nini? Huyu Kinana ni Kada wa CCM na alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali ktk nchi yetu wala huko nyuma wakati wa utawala wa Mwalimu, Kinana hakuwahi kujadiliwa uraia wake ila ktk kipindi cha Mwinyi na huyu mwendawazimu aliyekuwa wakati huo Waziri wa mambo ya ndani Augustine Mrema!

Huyu Mrema alikuwa na rafiki yake aliyetaka kugombea ubunge wa arusha lakini tishio lilikuwa ni Abdurahmani kinana aliyekuwa mbunge wa muda mrefu huko Arusha na kwa kweli alikuwa akipendwa sana na wananchi wa Arusha Mjini, ndipo huyu Mwendawazimu Mrema kwa kutumia wadhifa wake huo akachomowa faili la uraia la Kinana ktk uhamiaji na kupayuka kuwa Kinana hawezi kugombea ubunge wa arusha mjini ati kwa sababu uraia wake unautata!

Sasa na nyinyi humu bado munaendeleza majungu yaleyale yaliyopitwa na wakati? yaani badala ya kujadili mambo muhimu yanayotukera leo kama vile ujinga, maradhi, njaa, shida ya umeme, barabara mbovu, rushwa,ukabila, udini, ujambazi, mauwaji, uongozi mbovu, umasikini, nk. tunamjadili Kinana kama ni raia au si raia? sasa mumevuka mpaka maana munataka kuingilia kazi za uhamiaji!

Kama hamumjui Kinana basi mimi namjuwa vizuri sana, mtaa na hospitali aliyozaliwa, Baba yake na mama ake wote ni wa TZ sasa kama nyinyi munaushahidi kuwa Kinana si raia basi thibitisheni hilo ili uhamiaji waweze kumshugulikia! lakini hilo haliwezekani kwani yeye ni kada damu wa CCM labda ajiunge na upinzani!

Kama munadai Kinana si raia ati kwa sababu asili yake ni usomali basi mbona wengi wetu hatutakuwa raia kwani asili zetu wengi ni kutoka nchi mbalimbali kama vile Malawi, Zaire, Kenya, Uganda, Ethiopia, Comoro, Arabuni nk.?
Tuache majungu na hasa hasa udini maana huyu Kinana kwa kuwa munamuona ni Muislamu na ana asili ya usomali! hata Salim Ahmed Salim alijadiliwa Uarabu wake wakati akigombea urais 2005!

Nchi yoyote yenye kufuata misingi au utawala wa sheria haiwezi kumbagua raia wake yoyote yule kwa misingi ya rangi, dini, jinsia au asili ya mtu! tuache fitina na chokochoko! sanasana wewe unaemjadili Kinana tukikuchunguza tunaweza kukugunduwa uharamu wa uraia wako!
 
kadogoo
hee hee taratibu, bila ya jazba, suali yuko wapi kinana na nani? sasa una habari zozote tupe bila ya jazba mkuu.

ama kama tukifuatilia roots zetu si watanzania hilo jengine itabidi uanzishe thread nyengine itayosema jee watanzania ni watanzania?(joke)

kadogoo fairplay usiingie watu nguoni watakukuta eeeh br.
 
Hivi hapa munajadili nini? Huyu Kinana ni Kada wa CCM na alishawahi kushika nyadhifa mbalimbali ktk nchi yetu wala huko nyuma wakati wa utawala wa Mwalimu, Kinana hakuwahi kujadiliwa uraia wake ila ktk kipindi cha Mwinyi na huyu mwendawazimu aliyekuwa wakati huo Waziri wa mambo ya ndani Augustine Mrema!

Huyu Mrema alikuwa na rafiki yake aliyetaka kugombea ubunge wa arusha lakini tishio lilikuwa ni Abdurahmani kinana aliyekuwa mbunge wa muda mrefu huko Arusha na kwa kweli alikuwa akipendwa sana na wananchi wa Arusha Mjini, ndipo huyu Mwendawazimu Mrema kwa kutumia wadhifa wake huo akachomowa faili la uraia la Kinana ktk uhamiaji na kupayuka kuwa Kinana hawezi kugombea ubunge wa arusha mjini ati kwa sababu uraia wake unautata!

Sasa na nyinyi humu bado munaendeleza majungu yaleyale yaliyopitwa na wakati? yaani badala ya kujadili mambo muhimu yanayotukera leo kama vile ujinga, maradhi, njaa, shida ya umeme, barabara mbovu, rushwa,ukabila, udini, ujambazi, mauwaji, uongozi mbovu, umasikini, nk. tunamjadili Kinana kama ni raia au si raia? sasa mumevuka mpaka maana munataka kuingilia kazi za uhamiaji!

Kama hamumjui Kinana basi mimi namjuwa vizuri sana, mtaa na hospitali aliyozaliwa, Baba yake na mama ake wote ni wa TZ sasa kama nyinyi munaushahidi kuwa Kinana si raia basi thibitisheni hilo ili uhamiaji waweze kumshugulikia! lakini hilo haliwezekani kwani yeye ni kada damu wa CCM labda ajiunge na upinzani!

Kama munadai Kinana si raia ati kwa sababu asili yake ni usomali basi mbona wengi wetu hatutakuwa raia kwani asili zetu wengi ni kutoka nchi mbalimbali kama vile Malawi, Zaire, Kenya, Uganda, Ethiopia, Comoro, Arabuni nk.?
Tuache majungu na hasa hasa udini maana huyu Kinana kwa kuwa munamuona ni Muislamu na ana asili ya usomali! hata Salim Ahmed Salim alijadiliwa Uarabu wake wakati akigombea urais 2005!

Nchi yoyote yenye kufuata misingi au utawala wa sheria haiwezi kumbagua raia wake yoyote yule kwa misingi ya rangi, dini, jinsia au asili ya mtu! tuache fitina na chokochoko! sanasana wewe unaemjadili Kinana tukikuchunguza tunaweza kukugunduwa uharamu wa uraia wako!

Hatuongelei rangi wala dini yake. Tanzania tumewahi kuwa na mawaziri wahindi na wazungu: Al Noor Kassum, Amil Jamal, Dereck Bryceson, Leader Sterling, n.k. Pamoja na kuwa baadhi yao walizaliwa nje ya Tanzania, uraia wao ulikuwa unajulikana bayana. Tatizo ni kuwa "uraia wa Kinana umeshasemekena una matatizo." Hata kama ni Mrema aliyetoa taarifa hiyo, hakuna mtu aliyebisha wakati inatolewa na wala hatujaambiwa kuwa swala hilo lilitatuliwa vipi ingawa mahakama haikumruhusu kugombea ubunge tena. Tunajua kuwa mtu kama Jenerali Ulimwengu naye uraia wake uliwahi kupatika na utata pamoja na kuwa aliwahi kushika madaraka mengi sana tena makubwa makubwa pale serikalini. Hata hivyo yeye aliamua kuuomba kiharali na kesi yake ikaisha. Swali ni je Kinana naye aliomba uraia wake ili kuuhalalisha? Kama wewe ulikuwapo wakati anazaliwa na unauhakika kuhusu uraia wake basi ungetuarifu hilo tu baada ya kuingia kwa jazba hivyo. Kama alikuwa ni raia wa kuzaliwa ni dhahili kuwa mahakama isengemkataza kugombea ubunge.
 
kadogoo kama jina lako kweli ni kadogoo na una uelewa mdogoo wa mambo . Umekurupuka na mengi sana na matusi lakini bado tunataka kuuliza Kinana ni nani Tanzania maana hata majuzi alienda kiwanjani akiwa na waziri fulani kumpokea mwekezaji wa Kempenisk .Je Ukada wake wa CCM una uhusiano na uwekezaji ? Kinana kakimbia EA kwa kuwa swala la uraia wake una utata mkubwa . Kwa kuwa ni kada ndiyo kila kitu kinazimwa kama Ditto ni kada katoka jela pamoja na kuua lakini bado tuna hoji ni nani ? Uraia wake pia ni upi ? Ushahidi upo kwamba alikuja Arudha kashikiliwa mkono na Baba yake leo unasema unajua alipozaliwa ? Machungu gani yamekushika na kuanza kuandika namna hii maana kwanza u mgeni hata aina ya uandishi wako na jazba . Endelea kutuelezea ni nani na yuko wapi ?
 
Huyu Kinana mwaka 1995 si alikuwa Meneja wa kampeni wa Mkapa..?aalfu nadhani alikuwa mwanajeshi akafikia cheo cha Ukanali.
 
Huyu Kadogoo kama kweli anamjua Kinana atuambie baba yake aliitwa nani kama sio Sheikh na ni mwarabu. Mama yake ni msomali. Na atusadie kutambia hili jina Kinana alipataje. Kama sio E Sokoinne alimuingiza kwenye siasa toka jeshini?? Tueleze ukweli.Toka Jeshini hakupelekwa Yugoslavia kama Political Commissar? Labda unaweza kutusaidia uhusiano wake na wale warabuu wa Loliondo (wawindaji) na hayo magari yao yalikuwa kwake Masaki.

Kama wa JF kweli wakitaka kuifuata history yake na utajiri wake ya wizi itawabidi waende kule UK kuhesabu nyumba zake na nani anakaa humo.

Na nikiendelea mtashangaa.
 
baba yake aliitwa nani kama sio Sheikh na ni mwarabu. Mama yake ni msomali

Yaleyale......halafu tunadai ubaguzi ni matatizo ya watutsi, wahindi, wazungu, wakenya......lakini sisi wala halituhusu....

Hili ni gonjwa linatula ndani kwa ndani na tusipofungua macho kukubali ukweli litatumaliza

Tanzanianjema
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom