Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Ndugu wananchi na wanachama wa Jimbo la Kigoma Mjini leo tarehe 15/Julai /2025 ambayo ni siku ya mwisho ya kuchukua na kurejesha fomu ndani ya chama chetu nimechukua fomu ya kuomba ridhaa kugombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini kwa mujibu wa katiba ya JMT ya 1977 ibara ya 21 na Katiba ya chama chetu ibara 11(c) toleo la 2024. Nimekabidhiwa fomu na Katibu wa Jimbo la Kigoma Mjini ndugu.Iddi Adam Sumvya.
Ndugu, wananchi na Wanachama wa ACT Wazalendo Jimbo la Kigoma Mjini,kama mnavyofahamu sio mara ya kwanza kuchukua fomu kuomba ridhaa ndani ya chama kugombea Ubunge Jimbo la Kigoma.Tarehe 5,Julai 2020 nilichukua fomu katika hatua ya kura ya maoni kuomba ridhaa ya chama chetu kugombea Ubunge Jimbo la Kigoma Mjini ila kwa uwezo wa Mungu kura zangu hazikutosha ,na hivyo kiongozi wa chama mstaafu Mh.Zitto Zuberi Kabwe akapitishwa kuwa mgombea wetu kabla ya dola na CCM kuvuruga uchaguzi wa 2020
Soma pia: GE2025 - Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge katika Uchaguzi Mkuu 2025
Ndugu, wananchi na Wanachama wa ACT Wazalendo Jimbo la Kigoma Mjini,dhamira yangu ya kugombea tena mwaka huu 2025 haikutikisika wala kuyumba na ndiyo maana leo kwa mara nyingine nimechukua fomu ili kuomba ridhaa ya chama changu kuwa mgombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini,nina amini nitapewa ridhaa sababu nina uwezo,dhamira,nia na nina tambua changamoto na shida za wananchi wa Jimbo la Kigoma Mjini
Na kama ikitokea kura zangu hazitatosha na kukosa ridhaa, nitatumia muda wangu wote kama nilivyofanya uchaguzi wa 2020 kushirikiana na wananchi, wanachama na viongozi wa chama changu Jimbo la Kigoma Mjini kuhakikisha tunapambana mgombea atakayepitishwa na kupewa ridhaa na chama anashinda kwa kura nyingi na za heshima.Ili kurejesha hadhi na heshima ya mji wetu,ili kukamilisha miradi yote ya maendeleo tuliyoipigania 2015-2020,ili kuboresha hali ya uchumi wa watu wetu na kurejesha sauti ya utetezi Bungeni kwa wananchi wa Jimbo la Kigoma Mjini.
Jimbo la Kigoma Mjini sio Jimbo la majaribio,sio Jimbo la kuleta mizaha na kutafutia umaarufu. Ni Jimbo lenye wananchi waelevu wanaojua wanataka nini ,na wanataka Mbunge wa namna gani.
Na ndiyo maana tumejidhatiti kurejesha hadhi na heshima ya Mji wetu wa Kigoma Mjini kwa Kupiga kura ,kulinda kura na kupambana dhidi ya hujuma zotezote za dola na CCM ili kuhakikisha chama chetu kinashinda kwa kura nyingi nafasi ya Ubunge, pia kurejesha Manispaa chini ya ACT-Wazalendo katika uchaguzi huu wa 2025.
Ahsanteni, Mungu awabariki sana.
Abdul Omary Nondo.
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa ACT Wazalendo.
Mtia nia Jimbo la Kigoma Mjini, 2025.