Abdul Kambaya awasha moto Tanga. Ataka watu wajiunge CHADEMA ili kuondoa mifumo mibovu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa habari na uenezi wa chama wa Chama cha Wananchi CUF, Abdul Kambaya, na wanachama 384 kutangaza kujiunga na Chadema. Sasa wawasha moto.

Tarehe 23 Februari 2023, Kambaya na wenzake walitangaza kujivua uanachama CUF kwa madai kuwa chama hicho kimepoteza mwelekeo na kumtuhumu Mwenyekiti Profesa Ibrahimu Lipumba kukiuka katiba ya chama hicho.

Sasa wameongeza nguvu chadema na wameshaanza kazi rasmi ya kubadilisha fikra hasi. Tatuzo ni mifumo ya Nchi. Na mfumo wenyewe ni katiba iliyopo. Anataka uwepo wa katiba mpya.

Hapa Kambaya akiwa anakiwasha Mabanda ya Papa Kata ya Msambweni na Ngamiani Kati na Kata ya Mwazange Jijini Tanga chini ya Mwavuli wa CHADEMA.


 
Propaganda za udini na ukabila zilizopandikizwa na magamba miaka na miaka ziliumiza sana upinzani na kwa uelewa wa watanzania walifanikiwa to some extent. Mkabila halisi alikuja kujulikana baadaye.
 
Huyu kambaya kesho haribu haribu huko CUF naona kuingia chadema sidhani kama atadumu, maana hakuna loop hole za kuiba fedha kama alivyofanya CUF, chadema imeshikwa na wajanja kwelikweli wenyewe ruksa mtu baki hapana, ndio maana nasema hapa kambaya hapo CDM ni stranger tu.
 
Huko chadema si kuna mfumo wa mwenyekiti kukalia kiti maisha, mbona hawajauondoa huo? Au kwao ni mfumo mzuri? Kwa mwenyekiti wa chama ni mfumo mzuri, kwa rais ni mfumo mbaya!
Uzezeta upo wa aina nyingi.
 
Back
Top Bottom