Abdallah: Naamka kwenye kifusi, naenda shuleni

Abdallah: Naamka kwenye kifusi, naenda shuleni

OUT OF TOPIC
Barnabas Samata

Mbwana Samata

Stamily Samata.

Kuna undugu wowote hapa?
mkuu ndio maana ukajipa hilo jina ulilojipa? maana kila post yako niliyoiona unakua nje ya point kuu
 
Wanalazimisha kuwafunza ukatili watoto wetu, watoto kama hawa wanatakiwa wapate watu wa kuwarekebisha kisaikolojia la sivyo wanaweza kufanya mambo ya ajabu waakiwa wakubwa, kushudia nyumba yao ikibomolewa ni sawa kuona mauaji ya ndugu zake, wanalazimisha masikini wawe wengi ili wawatawale kwa nguvu
kweli mkuu, mimi kama mtu wa mabo ya saikolojia, hii itawaathiri sana watoto hadi ukubwani mwao
mwenyewe nilisikia kuwa magufuli akiwa mdogo sana alishuhudia nyumba yao ikibomolewa na wazazi wake kuteseka kwa muda naye ikamuathiri saikolojia ndio maana anafanya anachofanya
 
Matatizo ya kutojua priorities. Hili la kubomoa halingeweza kufanywa kwa ubinadamu zaidi? Mbona wenye fedha hawafanyiwi hivi!
 
God will never bless such a government & country; They don't have even a piece of compassion & sympathy to these innocent children!? Halafu kiongozi anakuja na kusema, hawana mpango wa kuwatafutia sehemu! What about this kids?!

And the most astonishing thing, "God always listens to the cries of those oppressed." So, whatever they are cursing this country with their painful situation, "He will do it." Kumbukeni nini kilitokea Tanzania pale albino na vikongwe walipompazia sauti Mungu, kwa sababu Yeye huwa hapendi kabisa the shedding of innocent blood.
kilitokea nini hivi??? nimesahau
 
Wabongoooooooooooooooooooo.Let me get reluief from my signature
 
Mvua za masika zinapoanza kila mtu anayekatiza akiwa ndani ya gari huku akizichungulia nyumba ambazo zimezingirwa na maji katika maeneo ya mabondeni huwaonea huruma watu wanaoishi katika hizo nyumba, lakini wakati wa jua kali ndipo tunajenga hoja nyepesi za kuyatetea makazi ya watu wa mabondeni, siasa zimeharibu kila kitu cha nchi hii. Miaka ya 70, 80 na 90 maeneo hayo hayakuwa na watu na maji ya mvua yalikuwa yakienda baharini bila ya vipingamizi vya nyumba. Hakuna ujanja mwingine zaidi ya nchi kuendeshwa kwa kufuata sheria na kanuni.
 
“Inawezekana wazazi
wetu wameikosea
Serikali kiasi cha
kupewa adhabu hii
kali inayotugusa hata
sisi watoto, lakini
najua inaweza
kutusaidia. Najua ina
fedha za kutunza
watu wake, najua
hatuna thamani wala
hadhi ya
kuhudumiwa lakini,
ituhurumie.
Itusaidie, tunaumia
na maisha haya
yameshatuchosha,”
anasema Jacob.
Jamani! Naomba wa jf tumsaidie huyu dogo. Tutabarikiwa sana tuungane watupe namba ya akaunt/simu halafu ianzishwe special thread yake tutupie humo chochote. Waliopo tayari tafadhari, mm nipo tayari.
 
Awamu ya Tano ni kufuata Utawala wa Sheria na Kanuni hamna jinsi. Tulizoea kuishi kwa mazoea na kuidharau serikali.
Huyo Abdallah yakija mafuriko hapo na kuisomba familia yake yote nani atakuwa responsible hapo!!???
Tuwe tunafikiria kwa kina kabla ya kuandika upuuzi. Kuna watoto wa ngapi wanaishi maisha ya dhiki kuliko huyo Abdallah Tanzania hii!!!????? Mnaleta siasa za Maji taka kwenye mambo ya kimsingi. Mbona kuna watu/ familia zimebomolewa hapo na wahehamia sehemu nyingine salama na kuanza maisha mapya. Kwa nini hamuendi kuwatafuta hao muwahoji!!!?????
Zoezi la BOMOA BOMOA litaendelea kwa mujibu wa SHERIA NA KANUNI ZA MIPANGO MIJI NA MATUMIZI BORA YA ARDHI.
Ni kweli kabisa miaka takribani 35 ya kuishi kwa mazoea imetufikisha hapa, maswali yanayobaki ni sisi kuchagua sasa:
"sheria kwanza busara baadae" au
"busara kwanza sheria baadae"!
 
Ni kweli kabisa miaka takribani 35 ya kuishi kwa mazoea imetufikisha hapa, maswali yanayobaki ni sisi kuchagua sasa:
"sheria kwanza busara baadae" au
"busara kwanza sheria baadae"!
Mkuu Lukindo,
Kwa hali ilivyo sasa mimi binafsi nafikiri kwa tulipofikia hapa inabidi iwe "Sheria kwanza Busara baadae" mkuu. Maana hamna jinsi.
 
Mkuu Lukindo,
Kwa hali ilivyo sasa mimi binafsi nafikiri kwa tulipofikia hapa inabidi iwe "Sheria kwanza Busara baadae" mkuu. Maana hamna jinsi.
Sheri inafanya kazi kwe masikini sio kwa matajiri, busara inafanya kazi kote. kama serekali kwa nini wasijenge nyumba za room 2 na choo na bafu wapangishe kwa bei nafuu ambayo asilimia 85 ya watu wanaoishi mitaa mibovu wangepangisha, NHC ina vyumba vya Sh 48,000 kama wangekua na nyumba nyingi Watz wangepangisha.sio kuwabomolea makazi yao. sio suluhisho kwani watahamia maeneo mengine na kujenga hivyo hivyo, kama wanataka suluhisho la haraka, afanye kama Idamini, alivyoangamiza viwete. nao wafanye hivyo kuondoa masikini!!!!!!!!
 
Tunatumia picha kutafuta huruma. Vipi zikiwekwa picha huyo mtoto yuko juu ya paa la nyumba kutokana na mafuriko? Kweli watz ni wepesi kusahau kuliko kiumbe yeyote ulimwenguni

..serikali iwajengee nyumba.

..mbona kule Bagamoyo waliopisha ujenzi wa bandari wanajengewa nyumba na serikali?
 
Sheri inafanya kazi kwe masikini sio kwa matajiri, busara inafanya kazi kote. kama serekali kwa nini wasijenge nyumba za room 2 na choo na bafu wapangishe kwa bei nafuu ambayo asilimia 85 ya watu wanaoishi mitaa mibovu wangepangisha, NHC ina vyumba vya Sh 48,000 kama wangekua na nyumba nyingi Watz wangepangisha.sio kuwabomolea makazi yao. sio suluhisho kwani watahamia maeneo mengine na kujenga hivyo hivyo, kama wanataka suluhisho la haraka, afanye kama Idamini, alivyoangamiza viwete. nao wafanye hivyo kuondoa masikini!!!!!!!!
Aiseee!!!!!! Basi nenda mahakamani. Pole kwa kukumbwa na BOMOA BOMOA ...
 
Tunatumia picha kutafuta huruma. Vipi zikiwekwa picha huyo mtoto yuko juu ya paa la nyumba kutokana na mafuriko? Kweli watz ni wepesi kusahau kuliko kiumbe yeyote ulimwenguni
Kwani mafuriko yanaletwa na matinga tinga...
 
Tunatumia picha kutafuta huruma. Vipi zikiwekwa picha huyo mtoto yuko juu ya paa la nyumba kutokana na mafuriko? Kweli watz ni wepesi kusahau kuliko kiumbe yeyote ulimwenguni
Huyu mtoto anatafuta huruma ndio

... Kama unaweza msaidie
 
watz ni kivutio cha utalii kwa vituko vyao
 
Back
Top Bottom