A Program Note: Tutaweka Hoja Zetu Wazi

Mwaka 2009 Zitto hakuzuiwa kugombea. Alitaka kugombea ila aliombwa ajitoe na akakubali angeweza kukataa na kuendelea kama angetaka.....

Mikakati yake ya 2014, ilikuwa kinyuma na taratibu za Chama na taratibu za Chama zilikuwa zinaendelea kumshughulikia kabla ya yeye kukimbilia mahakamani kuzuia mchakato wa chama kumshughulikia....



 

ndugu kinachoudhi sana hapa, sio kuwa na tabaka za wagombea au mipango ya kubaguana. Ila mtu yoyote anaweza ingia kwenye chama na baada ya hata mwezi akagombea nafasi yoyote ya kiungozi ndani ya chama.
Lakini sio mtu ambaye amekatwa kwenye kinyanganyiro kwenye chama chake akakimbilia chama kingine tena kwa masharti ya lazima yeye ashike sukani tena bila hata ushindani na wanachama wengine waliojijenga miaka kadha ndani ya chama. That’s not ethical at all its corrution and dictatorial behaviour period.
Si unaona sasa kuna mshururu wa vigogo wa ccm walioangushwa kwenye kura za maoni, wamefunga foleni chadema zaidi ikifuatiwa na act, wakijue au wakiwa wamehadiwa na lowassa kuwa atawasaidia.
Lowassa amewaahidi kuwaletea makapi wana chadema. Ndugu usemayo sio kweli, am not a chadema supporter, but am a true tanzanian it will disasterous is a strong opposition party like chadema is destroyed by greed. Leo serekali ya ccm haiwezi kufanya jambo bila ya kujiuliza mara mbili , jee cdm wataleta upinzani gani, a strong cdm is necessary for ccm to perform.
 
Kwa chama kinachoongozwa na mtu wa level ya Form Four mtategemea sana mabadiliko lakini mtajifunga mabao ya wazi, kama hili la Slaa na Lowassa.
 

Mbona mnalialia kwani nyie mmejipangaje? Nyie tulieni atoe hoja.
Kati ya zitto na team mbowe nani wameisaliti cdm kimisingi
 
Mkuu
with serious note!

"Hatukukaa kimya kwa watawala walioshindwa wa sasa, na hatuwezi kukaa kimya kwa wanaotaka kuwa wa kesho" MM
 

Nakubaliana nawe.Kwani ifike mahali tuone vyama ni vya wananchi na si vya waanzilishi wa vyama hivyo.Hata kama itabidi kuchanga pesa toka kwa wanachama kuwarudishia waanzilishi hao ili waviache vyama viongozwe na wanachama.

Ni kweli mtu mgeni unakaribishwa badala ya kuandaliwa chakula unaingia jikoni mwenyewe eti unatengeneza unachotaka wewe kula.

Hii ipo hapa kwetu.Viongozi wetu wamekosea lakini tusiwaache tuwe wamoja tukimaliza kupambana turudi mezani tukubaliane katika kutokubaliana.
 
Hili ni la kuwambia wanaofikiria kula tu na si maendeleo.

Mbowe alikuwa anamuogopa ZZK kuliko CCM. Ni ZZK tu aliyekuwa na uwezo wa kuongoza na kuridhi kiti. Kwa sababu ya kutoruhusu wengine washike chama matokeo yake walitengeneza zengwe ambalo hata sehemu moja huwezi ona uhusika wa ZZK ingawa ndo alikuwa anasakamwa.

Hayo tuache, kwa hili linatotokea ni mwendelezo wa hayo ya familia kuongoza chama. Kwa bahati mbaya imekuwa fedheha kwa baadhi ya wateule.
 

wewe endelaea kuchukia lakini sisi ndio tulioweka agano na sasa tunaliishi agano letu

"Hstukukaa kimya kwa watawala walioshindwa wa sasa, na hatuwezi kukaa kimya kwa wanaotaka kuwa wa kesho"MM
 
Mambo haya si ya leo. Kila wakati watu wengi wamelalamikia mfumo wa kifamilia ndani ya CDM. Wanachama wanaona ni mipango ya CCM kuvuruga chama. Sasa ni kweupe, tumechaguliwa anayetakiwa na familia, tusibaki kulalamika.
 


Ndiyo hapo wameshakosea?Sasa suluhu ni nini?Tuendelee kulumbana bila kuwa na suluhisho?Suluhisho ni lazima.Tukae chini tukubaliane,mgeni kaja sawa,mmemkaribisha,na mgeni amewapa masharti mmekubali,sasa wameona wamekosea njia waliyoitumia tuache MELI igonge mwamba?

Nasema HAPANA,Mbowe kaona wamekosea njia,amerudi nyuma kutafuta njia ya kuweza kufika,ametumia BUSARA kusema Dr.Slaa ameomba kupumzika amewaruhusu wao waendelee!!!!!!!!!!!!!!Watu wazima hatuulizi alisema lini,saa ngapi,mlikutana wapi,tunaelewa tunaona hatutakiwi tuambiwe tazamani huku.......nk nk.Ameona amekosea amechukua njia iliyo sahihi.

Wanachama tujadili nini tufanye?Ukiniuliza mimi nitakwambia kwa uhakika siyo Pro-Lowassa wala Team Lowassa,Lowassa afanye press conference aanze kujisafisha mwenyewe kwanza.

Wanachama tujitahidi kwa kila hali kuhakikisha tunapata wabunge wengi wengi ,siyo sababu tunahitaji sana rais,bali tunahitaji zaidi wabunge wa kwenda kuzuia MAGOLI YA MKONO BUNGENI.

MM yupo sahihi,twende mbele tutafute suluhisho,hawa CCM wako busy wanachochea kuni,uzuri KUNI tulizitia maji usiku,ni mbichi hazitawaka,wataishia kupata mafua na kuumwa macho.

PAMOJA TUNAWEZA iwe kauli mbiu yetu.
 
Pasco,

Sure!! Lakini kuna vitu ambavyo ni vya msingi sana kuvijuwa juu yake. Wasiwasi wa wengi umejikita katika mambo mengi sana na si kushinda tu.

1. Kikubwa ni sustainability of the project. Umekiri kuwa Lowassa hana uwezo kama Magufuli na UKAWA hawana uwezo kama CCM. Je Lowassa akishindwa atakuwa na uwezo wa kukaa ndani ya CDM na kukitangaza kwa mapambano kama akina Slaa na wengine walivyojitolea?

2. Ndani ya CDM nani anao uwezo wa kumkanya au kumuongoza Lowassa?

3. Lowassa atakubali kuwa kuongozwa na watu wengine akishindwa kupata urais?

4. Malengo ya Lowassa kuja CDM ni nini hasa? Lowassa anakuja na CDM kama kituo cha muda. Ana watu wake na washauri wake nje ya CDM, hao ndo atakamilisha mission zake. Ndani ya muda mfupi, ataamua kwenda alikotarajia. Na hili liko wazi. Hiyo 38% kama mtaji wake ndani ya CDM naonekana kama fiction tu. Hakika hautadumu ndani ya CDM.


Ukimsikiliza Lowassa kwa undani ni mtu mwenye kujiamini kupitiliza. Alianza na hayo akiwa ndani ya CCM katika harakati zake za kuwania urais. Hata majuzi ndani ya CDM ukiangalia kiundani ana maneo ya kijeuri sana na kejeli furani ambazo naziona si rahisi kukaa ndani ya CDM na kujenga chama.

Ninavyoona mimi, hao waliopo ni wa thamani sanaaaaa. CDM ijiangalie sana, hasa mfumo wao wa kiuongozi na kimaamuzi. Wasipo ruhusu demokrasia ndani yake, itarudi makumbusho si muda mrefu.

 
Nimeamini kweli CCM kiboko! Wameshindwa kumnunua Dr Slaa lakini wameweza kukinunua chama kizima na kuweka mgombea wao!!!
Mkakati wao bab kubwa da!
Sijui nimuamini nani tena kwa kweli
 

Mwana kijiji katika ubora wake
 
Mambo haya si ya leo. Kila wakati watu wengi wamelalamikia mfumo wa kifamilia ndani ya CDM. Wanachama wanaona ni mipango ya CCM kuvuruga chama. Sasa ni kweupe, tumechaguliwa anayetakiwa na familia, tusibaki kulalamika.

Usikate TAMAA bado tunaweza,hii changamoto ndiyo itakayotuelekeza kwenda tunakotaka.MM ametupatia ufumbuzi wa nini kifanyike,tukifanye ili twende mbele.

Askari akijeruhiwa halali hapo lazima atajisukuma na kujikaza sana atoke hapo aende mahali salama.
 

Achana na Pasco,shemeji yangu huyu ni kipenzi cha Lowassa na ndiyo maana ameweza kuja na jeuri eti hawa 10% fukuzia mbali,je anajua impact ya 10% ya chama cha upinzani?

Je.ni lini Pasco aliweza kupigania upinzani zaidi ya Lowassa?

Pasco yawezekana unamapenzi makubwa na Lowassa,je unafahamu utendaji wake wa kazi kwa undani?Unatuambiaje sisi tuliokuwa tunafanya naye kazi kwenye sekta za binafsi za kupeleka maendeleo kwa wananchi alikuwa anataka nini?

Je ,si huyu ambaye MIRADI ikienda kwake anauliza atafaidikaje nayo?Akiwa mbunge alidai hivyo akiwa RAIS atadai vipi?Muwekezaji akija lazima apewe kiasi gani atafaidika nacho,akija donor lazima aweke kiasi cha Rais kufaidika nacho.Pasco wapo tunaomjua Lowassa ambao ni watu wa kawaida sana tuliokuwa tunatekeleza miradi ya maendeleo.

Kwa uhakika kwabisa jeuri ya kusema eti afukuzwe tu,jamani Pasco hata wewe haujaona mchango wa Dr.Slaa kwenye medani za UPINZANI?

Kwa uhakika kwa kumfukuza huyo CDM mmeimaliza maana wala hakuna haja ya BAO LA MKONO mtakuwa mmeshajifunga wenyewe! Na CCM kila siku wanaota usiku na mchana Dr.Slaa aondoke hapo ili UPINZANI usahaulike.

Kwa Pasco waswahili wanasema "UKIPENDA BOGA PENDA NA MAUA YAKE"Sisi ndiyo maua na majani yake, na kule kwenu Pasco Mboga ya Maboga bila maua haijapikwa bado!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…