A message to my Ex!

A message to my Ex!

Zuriel_cfc

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2017
Posts
4,104
Reaction score
9,116
Habari za siku nyingi? Naimani uko salama na unaendelea na majukumu yako ya kila siku. Mimi mzima kabisa wa afya ya mwili na akili..

Its been 5 months now since u went away, haikuwa rahisi kukubaliana na ukweli kwamba ulipita, umeenda, umeniacha! Japo mpaka leo sijaelewa sababu hasa ya kwenda bila kuaga, lakini wakati mwingine nahitimisha tu kwamba "HUKUNIPENDA"! aidha ulikuwa safarini ukahitaji kituo upumzike kidogo alafu uendelee na safari, ama ulikuwa na mategemeo fulani ukayakosa, yote heri nimeshukuru.

Muhimu tu ni kwamba nimekubali matokeo, nimesonga mbele. Nilifanikiwa kurudi mjini na kufanyia kazi moja ya malengo yetu tuliyokuwa tumepanga. Nimepata sehemu nzuri nimefungua mgahawa, nimeona nianze na hii kwanza alafu baadae niweke vinywaji. 😊😊. Si mkubwa bali kwa uwezo wangu naona ni hatua aisee. Pia ule ukarabati nimefikia hatua za mwisho, Mungu akinijaalia uzima nadhani mwezi ujao itakuwa nimemaliza kabisa.

Vipi wewe unaendeleaje? Umefikia wapi na mpango wako ule? Na ile mashine uliipata? Naamini Mungu wetu ni mwaminifu atakuongoza ukafanikishe kila ulilopanga, na kama tayari hongera sana sana!

Kitu nilichojifunza ni kusamehe, kukubali matokeo na kusonga mbele. Zaidi sana kuwaombea wengine. Nakushukuru kwa yote ambayo umenifunza, umenishauri na nakutakia kila lenye heri katika maisha yako na mahusiano yako mapya... uwe na usiku mwema.

Yours, Zuriel!

Screenshot_20190523-084427_Chrome.jpg
 
Hapo ndio utajua penye miti hapana wajenzi. Binti kama huyu unamuacha kwenye mataa hivi we mwanaume umerogwa au namna gani? Samahani nimepaniki mimi wakati mwenyewe ana amani
Kama ukipaniki ndio unatokwa povu laini namna hii, basi wewe ni waifu matirio and you are much better than Mwajuma long sandler's....teh
 
Back
Top Bottom